Wafungwa 142 kujadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole mkoani Kilimanjaro

Wafungwa 142 kujadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole mkoani Kilimanjaro

Joined
Feb 4, 2026
Posts
11
Reaction score
9
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, leo Februari 12, 2026, amefungua rasmi kikao cha bodi hiyo kitakachofanyika kwa siku mbili, kuanzia Februari 12 hadi 13, 2026, katika ukumbi wa Panama Garden Resort, mkoani Kilimanjaro.

Katika kikao hicho, jumla ya majalada 142 ya Wafungwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania yana tarajiwa kujadiliwa. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mheshimiwa Jaji Mstaafu John Mgetta, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, CP Nicodemus Tenga, akimwakilisha Katibu wa Bodi ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, wajumbe sita akiwemo Dkt. Juma A. Malewa, pamoja na Sekretarieti.

Kwa mujibu wa ratiba, kikao hicho kitajadili takribani ajenda kumi zinazohusu maombi na masuala mbalimbali ya Parole.

Parole ni utaratibu wa kisheria unaomruhusu mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka minne au zaidi kutumikia sehemu ya kifungo chake nje ya gereza kwa masharti maalum, baada ya kutumikia theluthi moja (1/3) ya kifungo chake, kuonesha mwenendo mwema na kuthibitika kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.

Simple blog post Instagram Post_20260212_144629_0000.png
 
Back
Top Bottom