Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Huyu jamaa ananyonyoka manyoya tu....
Hii ni dalili ya nini minyoo???
Huyu
IMG-20210203-WA0000.jpg
 
Mie nafugaga hii mijibwa ya uswazi (koko)
Yenyewe hayana gharama ya misosi maana yanakula chochote yanachokiona hata mavi ya walevi.!
Halafu wakiwa wengi huwa tunaua kisha tunawachuna na kuwapelekea wauza supu wa bar wao huchanganya na nyama ya mbuzi ili kuleta kale kaharufu ka kimbuzimbuzi kisha hupikwa supu na kuuziwa wateja.
duh!! Hatari sana mkuu
 
kwa uhitaji wa hao mbwa tajwa hapo juu na kwa kuongezea great dane
naweza kutoa connection moja ya hapa nairobi , kwa
breeder anaefahamika na kuaminika na kenya police,ni certified inshort,
anaweza kukufanyia delivery ya mpaka border na certificates kwa mbwa utakaehitaji
yupo sehemu inaitwa mirema kata ya githurai
 
Hebu tupe insta name yake tafadhali
kwa uhitaji wa hao mbwa tajwa hapo juu na kwa kuongezea great dane
naweza kutoa connection moja ya hapa nairobi , kwa
breeder anaefahamika na kuaminika na kenya police,ni certified inshort,
anaweza kukufanyia delivery ya mpaka border na certificates kwa mbwa utakaehitaji
yupo sehemu inaitwa mirema kata ya githurai
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
Mr Kuku mwingine
 
Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.

Jamaa alikuwa na GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.

Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.

Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).

Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).

Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.

Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.

Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.

Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.

Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.

Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.

Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.

Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions

Kukosa fahamu miezi mitatu si jambo dogo,pole sana kwa jamaa
 

Mbwa wa Joe Biden wafukuzwa White House​


Mbwa wanaomilikiwa na Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake Jill Biden wameondolewa Ikulu ya White House baada ya mmoja wao, kwa jina Major, kuripotiwa kumuuma ajenti wa usalama.
Screen-Shot-2021-03-09-at-16.02.18.png

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, mbwa hao aina ya ‘German shepherd’ wamepelekwa nyumbani kwa Biden huko Wilmington, Delaware.
Hii ni kutokana na ukali wa Major dhidi ya wafanyakazi wa White House.
Bw. Biden na familia yake walimuasili Major mwaka 2018. Alikuwa mbwa wa kwanza kutoka makao ya wanyama kuishi katika Ikulu ya Marekani.



Mbwa wao, Champ, ana miaka 13.

 
Nilichogundua mbwa ni passion bila hivyo huwezi . My dog ukitaka ugomvi mkubwa na mimi mpige au mfokee nikuone . Bado mdogo ana six months now nasubiri afike 8 nimpeleke training, ninempata toka kwa mtu ambae ana gsd wawili ajabu huyu katoka golden gsd but nampenda thats why nimemuita DAZZLER.
Nilikua nampa maziwa ya ng'ombe leo nimepata jibu why alikua anaumwa sana maana ilifika kipindi mpaka kula nilikua namlisha kwa kijiko huku akiendelea na dozi, ila nilipoacha kumpa mazima na dozi ilipoisha amerecover sana kumbe ni cases za minyoo dah, alikua akiharisha na kutapika kapigwa dawa za minyoo plus za magonjwa mengine Dr wake anajua zaidi, ana card la matibabu hivyo trend yote naifuatisha.
Mazoezi kila siku 3 za kwenye wiki nafanya nae walking ya km 2 mpaka 3 pia usiku kila siku yuko loose kuzunguka ndani ya nyumba.
Mbwa ana raha yake sana, gsd anacheza na watoto safi tu . Hakika kwa mm nikikuta mtu anapiga mbwa roho inaniuma sana , hata barabarani naepuka sana kugonga mbwa sana sana sana .
Chakula nampa champdog asubuh then jioni anakula nyama nampikia na unga wa dona(namix) . Nyama hizi nimeweka order buchani huwa wanauza zile chenga wakikata na mashine wana ongeza na mafuta plus utumbo pia na stake chache bei chee sana ni tsh elf 2 tu kwa kg. Kama kuna maboresho zaidi naomba mnijuze , namtunza tu kwa kulinda familia basi sitaki hata kuzalisha na kuuza , nimemuweka na mwenzie wa kiswahili ili asiboreke


Few years from now you may wish you should have started today...
unazuia vipi wasizaane?? vipi usafi maana mbwa kwa kuchafua mazingira wapo vizuri
 
Hapana mkuu, hawa mbwa wanafundishika na wana adabu sana kwa mmiliki/ mlishaji, tabia moja nzuri ya mbwa wote huwa hawamgeuki mlishaji, labda usijishughulishe nao kama Kingunge ni hatari sana.
kwani kingunge ilikuaje? Boerbol washawahi mgeuka dada mmoja hivi ndugu yangu
 
G.S Kupata pure kazi saaana na ni ghali mi nilipata Zambia, RW ndo nnae mpaka sahivi, GS Aliibiwa hawa watu unaotumia kuwapa train mbwa wengi sio waaminifu haswa wakikuta una pure breed, Fanya kila njia ujue jinsi ya kuwapa train we mwenyew, haya ma pitbull sijakutana nayo pure, nilipata crossbreed, yana nguvu sana ila sasa kama linanguvu halafu zito kuelewa la kazi gani sasa
vitu gani mbwa anafundishwa hasa na anatii kama huyo GS mnayemsifia?
 
Back
Top Bottom