Wafugaji wa kuku tuwe makini na chanjo, nyingi hazina ubora.

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,488
3,263
Nipo katika ufugaji wa kuku wa kienyeji na wa Malawi kwa muda mrefu. Ni mwaka wa pili sasa vifo kwa kuku vinaongezeka licha ya kutimza chanjo za Newcastle, gumboro na ndui kwa wakati mwafaka.

Jirani kanitonya, chanjo nyingi maduka ya pembejeo ni fake nilipo kuwa natumia chanjo toka VIC vifo vilikuwa vichache niliacha kwa urasimu. Taarifa ya 'mhusika hayupo' juma zima uendapo huko ni jambo la kawaida. Ni vema tukawa makini na maduka tununuayo hasa ukiwa na shaka na uadirifu wa mmiliki wa duka.
 
Ninanunua madukani lakini matokeo ndio hayo ya ongezeko la vifo.
 
Bei VIC na maduka ya pembejeo hazipishani sana. Newcastle ni sh 6000, gumboro ni sh 8000 na ya ndui ni sh 16000 kwa hapa nilipo.
Newcastle - 5000
Gumboro - 8000
Ndui - 14000
Kwa dsm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom