SoC03 Mapinduzi ya kijani kwa wakulima na wafugaji ni maendeleo endelevu

Stories of Change - 2023 Competition

Reginald paul

Member
Jul 6, 2023
5
4
Kilimo na mifugo katika taifa la Tanzania ni sekta muhimu sana kwa sababu inachangia takriban asilimia 40 katika Pato la taifa.

Pia kilimo ni uti wa mgongo wa nchi kwani takriban asilimia 80 ya watanzania wanategemea shughuli hizo Ili kukimu mahitaji yao ya kila siku ikiwemo chakula, malazi, makazi pia kuwasomesha watoto wao.

Wakulima wengi wamewekeza kwenye kilimo katika makundi mawili ambazo ni wakulima wakubwa(large scale farmers) ambao hawa ni wale wanaolima kuanzia ekari 5 na kuendelea na wakulima wadogo(small scale farmers) Hawa ni wale wakulima wanaolima chinii ya ekari tano, huku watu wengine wakinufaika na Ajira ndogondogo za hapa na pale kama vile upandaji wa mbegu, kupalilia magugu, upigaji wa viuatilifu pamoja na shughuli za uvunaji.

UJASIRIAMALI - kwa ufupi ni kitendo Cha mjasiriamali au mfanyabiashara kujianiri kwa kipato kidogo au kikubwa Ili kuondokana na umaskini wa kipato.

Kuna aina nyingii za wajasiriamali lakini hapa nitazungumzia zaidi mjasiriamali mbunifu, huyu ni yule mjasiriamali ambae amejiajiri kwenye mradi zaidi ya mmoja na ana uelewa juu ya kazi hizo na ana usimamizi mzuri Ili asipate hasara, ndani ya sekta ya kilimo na mifugo Kuna wajasiriamali wengi ambao wamejiajiri katika kilimo hususan maeneo ya vijijini pia wafugaji wengi maeneo ya vijijini wamejiajiri katika ufugaji hususan ufugaji wa kuku ambao ni ufugaji rahisi una gharama ndogo na unaweza ukaanza hata na mtaji mdogo.

Wataalam wa kilimo na mifugo(walioajiriwa na wasioajiriwa) wanachangia mabadiliko na maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo na mifugo Kwa kutoa elimu na ushauri juu ya kilimo na ufugaji wa kisasa.
Kama ijulikanavyo sikuhizi katika Kila kata Kuna mabwana mifugo na mabwana shamba ambao kazi yao ni kutoa elimu na ushauri kwa wakulima na wafugaji Ili waende kisasa jinsi ambavyo dunia ya Sasa inataka Ili mazao yao yaingie kwenye ushindani wa soko la kimataifa Kwa kutoa Pato la mazao ambavyo yamekidhi vigezo vinavyohitajika kwa mfano maharage ya njano grade 01 au Tumbaku grade 01.

Serikali sasa inatakiwa kuongeza wataalamu wa kilimo na mifugo angalau Kwa Kila Kijiji Ili kuongeza ufanisi katika idara hii ambayo ni muhimu sana Ili wakulima na wafugaji wafikiwe na huduma kwa muda sahihi jambo ambalo litachochea maendeleo makubwa sana na watashauriwa njia za kitaalamu kwa mfano njia za kudhibiti magugu shambani, njia za kudhibiti wadudu na magonjwa yanayoshambulia mazao mbalimbali pia Kwa upande wa mifugo watapata elimu juu ya namna ya kudhibiti magonjwa yanayoshambulia mifugo kama vile elimu ya ndigana kali na ndigana baridi, salabu (Foot and mouth disease) ambavyo ni magonjwa yanayojitokeza mara Kwa mara Kwa mifugo kama ng'ombe, mbuzi na kondoo, pia watapata elimu juu ya chanjo mbalimbali za kuku kama chanjo ya kideri na ndui.

Maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo(Agrovets and vetagros) nazo zinachangia mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo na mifugo kwani wakulima na wafugaji wamekuwa wakinufaika Kwa kupata huduma wanazozihitaji pia kupata elimu na ushauri juu ya kilimo na ufugaji wa kisasa, kama inavyofahamika wahudumu wengi wa vituo hivyo lazima wawe wamesoma kozi husika na wateja wote kwa asilimia 100 ni wafugaji na wakulima, huwezi kuta mtu yeyote anahitaji hardware yeyote anaenda kwenye Agrovets au mtu anahitaji huduma za kibenki anaenda kwenye Agrovets hapo hoja yangu ya msingi ni kwamba wateja ni wakulima na wafugaji kwa mantiki hiyo licha ya huduma wanazozipata pia watapata elimu na ushauri bora kabisa hatimae kuongeza maarifa na ufanisi katika shughuli zao.

Miaka ya nyuma enzi za mababu zetu wakiwa wanapanda mahindi kwenye shimo mmoja walikuwa wanaweka mbegu kuanzia 10 Hadi 15 wakiamini kwamba watapata faida kubwa jambo ambalo sio kweli na kuishia kupata faida ndogo na pengine hasara kabisa kwa sababu mbegu hizo hushindania rutuba ambayo ni kidogo Kwa sababu labda mkulima huyo hakuweka hata mbolea, lakini katika kilimo Cha kisasa unatakiwa kuweka mbegu 1 Kwa nafasi (spacing) ya 75cm*25cm na mbegu 2 Kwa spacing ya 90cm*60cm.

Makampuni mbalimbali zinazohusika na utengenezaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo nao wamekuwa wanachochea na kuchangia mabadiliko na maendeleo makubwa katika sekta hii na wakulima na wafugaji wengi wamekuwa wakinufaika kwa kiasi kikubwa.

Kwa mfano watengenezaji wa mbegu za mahindi na mbogamboga kama SEED-CO, PIONEER, AMINIKA na KIBO SEEDS ni baadhi ya watengenezaji na wasambazaji wa mbegu za mahindi za kisasa zilizotibiwa ambazo wakulima wanazitumia na kupata faida kubwa,pia Kwa upande wa mifugo kuna watengenezaji na wasambazaji wa dawa zinazotibu magonjwa yanayoshambulia mifugo kama BAJUTA CO LTD ni mfano bora kabisa na huwanufaisha wafugaji kupata faida kubwa na kukimu mahitaji yao ya kila siku.

HITIMISHO
Juhudi nyingi zinafanywa na serikali katika kusaidia vijana kujiajiri katika sekta ya kilimo kwa mfano kuanzishwa Kwa mradi wa BUILD A BETTER TOMORROW (BBT) chinii ya Block Farming kwa kuwapa mafunzo ya nadharia na vitendo vijana takriban 800 ni moja ya hatua kubwa tumepiga kama nchi chini ya wizara husika.

Serikali pia inatakiwa kuweka sheria madhubuti za kimkakati katika idara hii Ili wakulima na wafugaji wafanye shughuli zao chini ya sheria hizo, kwani wakulima wengi na wafugaji wamekuwa na dhana ya kupingana na wataalamu ambao wanawapa elimu na ushauri juu ya kilimo cha kisasa wakidhani kwamba wao ndio waelewa kutokana na kufanya shughuli hizo Kwa mda mrefu hivyo basi wawekewe kanuni na taratibu maalum Ili tupige hatua. MWISHO.
 
Back
Top Bottom