VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Katika Mkutano wa watanzania wapigania Katiba bora uliofanyika Viwanja vya Kibanda Maiti-Zanzibar,mambo yamekuwa mambo. CCM na Serikali yake imedhalilishwa,imeumbuliwa na kuchafuka. Hata Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar nayo iko hatarini kutawanywa na upepo mkali wa Katiba mpya. Mkutano husika ulihudhuriwa na kuhutubiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini.Lakini,Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar naye alikuwepo.Ni Ndugu Abubakar Khamis Bakari.
Huyu ndiye ninayemlenga. Akiwa jukwaani Kibanda Maiti leo,Ndugu Bakari amesema kuwa Waziri Mathias Chikawe (Katiba na Sheria) na Naibu Spika Job Ndugai ni waongo na wamelipotosha Taifa.Walidai kuwa Wazanzibari walisikilizwa wakati wa mchakato wa kuandaa Muswada wa Sheria ya Katiba mpya uliopitishwa 'kimagumashi' Bungeni Dodoma. Ingawa hawa hawakutajwa na Waziri Bakari,lakini mkumbo wa 'uongo' wa kuwasikiliza Wazanzibari ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd pamoja na Waziri Mkuu Pinda.
Balozi Idd alialikwa Dodoma(inasemekana na Waziri Mkuu Pinda) kwenda kutamka kuwa Zanzibar imesikilizwa na Muswada umeandaliwa ipasavyo. Akafanya hivyo.Akapigiwa makofi sana.Wapinzani wakabezwa na kuonekana wakorofi. Leo,Waziri ambaye ni mhusika wa kwanza wa masuala ya Sheria Zanzibar (Ndugu BAKARI) amepasua jipu. Amekanusha.Ametofautiana na Makamu wake wa pili wa Rais wa Zanzibar-Balozi Idd.Amesema Zanzibar haikuwahi kusikilizwa.Muswada ni batili!
Kukanusha maneno ya Balozi Idd ni kuuharibu na kuusawajisha msimamo wa CCM na Serikali yake kuwa Wazanzibari walisikilizwa(na kutoa maoni yao juu ya Muswada huo). Ni kuiumbua Serikali na chama. Ni aibu kubwa kwa chama na Serikali.
Kama maneno ya Waziri Bakari hayatakanushwa kwa ushahidi mujarabu,nategemea wafuatao wajiuzulu mara moja:Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Waziri Mkuu, Waziri Chikawe,Mwanasheria Mkuu-Jaji Fredrick Mwita Werema na wote walioshupalia kuwa Wazanzibari walisikilizwa.Halafu,Rais Kikwete hana haja ya kusaini Muswada huo uliopitishwa 'kiujanjaujanja'. Na kama Waziri Bakari amesema uongo leo Viwanja vya Kibanda Maiti-Zanzibar,basi naye ajiuzulu haraka.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam