MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,288
- 39,974
"He killed my ma, he killed my pa, but I will vote for him.".... kwa tafsiri isiyo rasmi inamaanisha "Alimuua mama yangu, alimuua baba yangu, lakini nitampigia kura"
Hiyo ni kauli maarufu ya wapiga kura wa Liberia hasa vijana waliokuwa wakimuunga mkono dikteta Charles Taylor mwaka 1997 kwenye kampeni za uchaguzi mkuu nchini Liberia mara baada ya kumalizika vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1996 nchini Liberia. Vijana waliimba huo wimbo na kweli kwenye uchaguzi Charles Taylor akashinda kwa asilimia sabini na tano (75%). Hawakujali kabisa mauaji yaliyofanywa na Charles Taylor kwenye vita vya kwanza.
Lakini mara baada ya kuingia ofisini kama Rais, Taylor alirudia tena ukatili wake wa siku zote. Waliokuwa wanaimba kumsifu wakati wa kampeni wakaanza kuwa wahanga. Safari hii akataka kuwafutilia mbali kabila la Krahn. Watu wa kabila hilo walifanyiwa kila aina ya ukatili ikiwemo kuuwawa kikatili. Wengi wao waliikimbia nchi. Kimsingi Charles Taylor akawa chanzo cha vita ya pili ya Liberia ya wenyewe kwa wenyewe. Hadithi yake ni ndefu mno ila Taylor alifikishwa the Hague kwa makosa ya ukatili dhidi ya binadamu.
Nikirudi kwenye dhumuni la uzi huu ambao nimeandika baada ya kushangazwa na jinsi karibu kila kona ya social media wafuasi wa CHADEMA wamejitokeza kumsifia Humphrey Polepole aliyejiuzulu ubalozi. Huwezi kukumbuka madhila waliyokutana nayo CHADEMA kwenye awamu ya 5 halafu ukamsahau Polepole. Bila kupepesa macho Polepole ni miongoni mwa ile inner circle iliyohusika na ukatili mwingi kwenye miaka yote ya utawala wa JPM. Ina maana CHADEMA washasahau yote yaliyowapata 2015 - 2020? Wana tofauti gani na wafuasi wa Charles Taylor? Wenyewe wanakwambia Polepole katubu.. 😔 😫 😩
Ifike wakati CHADEMA wakae chini na kutafakari wanachotaka kwenye siasa za nchi hii. Haiwezekani viongozi waandamizi wote waachane na agenda zao na kuanza kupost kuhusu kada wa CCM Polepole inashangaza sana.