Wafuasi wa CCM tambueni hili, Uongozi Bora si suala la chama, ni utashi wa kiongozi husika, Raisi awamu ya tano alizingua kuliko Marais wote wa JMT

...Ameandika Malisa GJ...

Ndugu yangu mmoja alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake. Lakini yeye anadai ni kesi ya kisiasa. Mwaka 2015 aliombwa kusupport kampeni za CCM akakataa lakini alifadhili kampeni za UKAWA. Anaamini hiki ndicho kilichomponza.

Mwaka 2018 alikamatwa na baadhi ya biashara zake kufungwa, na nyingine zikashindwa kujiendesha kutokana na makadirio makubwa ya kodi.

Baada ya kukaa gerezani miaka miwili akaona bora akiri ili atoke (the lesser evil). Wakati wa majadiliano na DPP akatakiwa kulipa zaidi ya 200M. Akakubali kufilisi biashara zake chache zilizobakia ili "kununua" uhuru wake.

Mwaka jana tulimtembelea gerezani mimi na Dr.Cyrilo. Tukamuuliza kwanini umeamua kukiri? Huoni itakuwekea doa? Kuna nchi utazuiwa kwenda kwa sababu ya "criminal record" ya uhujumu uchumi. Kuna fursa za biashara utashindwa kupata. Kwanini usingepambana ushinde badala ya kukiri.

Huku akilengwalengwa na machozi akajibu, nachotaka kwa sasa ni kuwa huru tu. Nikishatoka hiyo "criminal record" anaweza kuja Rais mwingine akaifuta, huwezi jua. Tukaagana, akarudi zake nyuma ya nondo.

Licha ya kukiri na kuwa tayari kulipa (plea burgaining) lakini bado hakuachiwa. Aliambiwa jalada bado lipo kwa DPP.

Wiki iliyopita amefutiwa mashtaka yote na kuachiwa huru, bila kulipa chochote. Siku anaachiwa wala hakujua kama angeachiwa. Ilitumwa "remove order" gerezani, akaenda mahakani bila kubeba chochote maana haikua siku ya kesi. Hata wakili wake hakuwepo.

Miguuni alivaa kandambili. Alipofika mahakamani akaambiwa, Jamhuri imekufutia mashtka yote na haina nia ya kuendelea na kesi. Akadhani ni mtego ili wamkamate tena. Akajaribu kutoka nje ya mahakama, lakini hakuna mtu aliyehangaika nae.

Akaita taxi, ikampeleka nyumbani. Mkewe akapata suprise ambayo hakuitegemea. Akaanguka, alipoamka akaanza kulia. Watoto walipomuona baba yao nao wakalia. Majirani wakaja na kumkumbatia, wakilia. Nyumba ikatawala machozi.

Hii nchi imepitia kipindi kigumu sana. Kuna jinsi Mungu anamtumia mama Samia kuponya majeraha na kuokoa mioyo iliyopondeka. Biblia inasema Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote (Mithali 14:34).!
Pumba kma pumba subili uone muda ndio mwl mzuri
 
Nadhan Wana CCM Kuna Jambo la kujifunza hapa, mnapochagua mtu wa kumpa kiti Cha Uraisi, zingatieni utashi wa mtu mwenyewe, sio kuleta mtu anayesimamia misimamo yake hata Kama haina tija, sio kuteuwa mtu ambaye atakomoa upande wa pili wa Vyama pinzani nakati wote ni wanadamu safar yetu ni moja.
Pamoja na yote, kama Mungu asingemtwaa JPM, jee unajua angefika 2025, angekuwa the best president this nation had ever had, angetuachia katiba mpya!.
Nisome hapa

Kiukweli kwa tangazo hili, rais Magufuli atabarikiwa sana, na Tanzania pia itabarikiwa, amini usiamini, this man might end up being one the best president this country has ever had, iwapo tukimpa kipindi cha pili, na akaamua kutuletea katiba mpya na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume huru zaidi na inclusive.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up! and God bless you.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!,
Mungu mbariki Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.

P
 
Pamoja na yote, kama Mungu asingemtwaa JPM, jee unajua angefika 2025, angekuwa the best president this nation had ever had, angetuachia katiba mpya!.
Nisome hapa

P
P..Mhe. JPM alikataa kuwa kwenye kampeni hakuahidi katiba mpya. Likumbuke Hilo.
 
'Hakika atukuzwe Mungu'
Hii kitu nimewaambia sana MATAGA hapa jukwaani, hakuna kitu kinaitwa ccm, bali ni msimamo na tabia binafsi za rais aliye madarakani. Na hao ccm wanachofanya ni kufuata mitazamo binafsi ya rais aliye madarakani na kulazimisha ionekane ndio misimamo ya chama.
 
...Ameandika Malisa GJ...

Ndugu yangu mmoja alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake. Lakini yeye anadai ni kesi ya kisiasa. Mwaka 2015 aliombwa kusupport kampeni za CCM akakataa lakini alifadhili kampeni za UKAWA. Anaamini hiki ndicho kilichomponza.

Mwaka 2018 alikamatwa na baadhi ya biashara zake kufungwa, na nyingine zikashindwa kujiendesha kutokana na makadirio makubwa ya kodi.

Baada ya kukaa gerezani miaka miwili akaona bora akiri ili atoke (the lesser evil). Wakati wa majadiliano na DPP akatakiwa kulipa zaidi ya 200M. Akakubali kufilisi biashara zake chache zilizobakia ili "kununua" uhuru wake.

Mwaka jana tulimtembelea gerezani mimi na Dr.Cyrilo. Tukamuuliza kwanini umeamua kukiri? Huoni itakuwekea doa? Kuna nchi utazuiwa kwenda kwa sababu ya "criminal record" ya uhujumu uchumi. Kuna fursa za biashara utashindwa kupata. Kwanini usingepambana ushinde badala ya kukiri.

Huku akilengwalengwa na machozi akajibu, nachotaka kwa sasa ni kuwa huru tu. Nikishatoka hiyo "criminal record" anaweza kuja Rais mwingine akaifuta, huwezi jua. Tukaagana, akarudi zake nyuma ya nondo.

Licha ya kukiri na kuwa tayari kulipa (plea burgaining) lakini bado hakuachiwa. Aliambiwa jalada bado lipo kwa DPP.

Wiki iliyopita amefutiwa mashtaka yote na kuachiwa huru, bila kulipa chochote. Siku anaachiwa wala hakujua kama angeachiwa. Ilitumwa "remove order" gerezani, akaenda mahakani bila kubeba chochote maana haikua siku ya kesi. Hata wakili wake hakuwepo.

Miguuni alivaa kandambili. Alipofika mahakamani akaambiwa, Jamhuri imekufutia mashtka yote na haina nia ya kuendelea na kesi. Akadhani ni mtego ili wamkamate tena. Akajaribu kutoka nje ya mahakama, lakini hakuna mtu aliyehangaika nae.

Akaita taxi, ikampeleka nyumbani. Mkewe akapata suprise ambayo hakuitegemea. Akaanguka, alipoamka akaanza kulia. Watoto walipomuona baba yao nao wakalia. Majirani wakaja na kumkumbatia, wakilia. Nyumba ikatawala machozi.

Hii nchi imepitia kipindi kigumu sana. Kuna jinsi Mungu anamtumia mama Samia kuponya majeraha na kuokoa mioyo iliyopondeka. Biblia inasema Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote (Mithali 14:34).!
Hii taarifa imenitoa majozi. Mungu ni mkubwa sana. Watanzania wenzangu, bila kujari itikadi za vyama vyetu, hili liwe fundisho, tusiruhusu nchi yetu kufanya makosa kama haya. Viongozi wanaochaguliwa kwa kura ni lazima waheshimu viapo vyao kwa maana ya katiba ya nchi. Hata hivyo tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupatia Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA. Mama Samia amewafuta machozi watu wengi sana katika kipindi kifupi sana.
 
Wasalaaaam!

Ni ukweli usiopingika kuwa, pamoja kwamba Rais Samia alikua Makamu wa Rais awamu ya tano, lakin hawakuwa kitu kimoja na Raisi wa awamu hiyo inangawa Rais Samia amejaribu kutuaminisha mara kadhaa akisema wao ni kitu kimoja!
Lakini kauli hiyo haiendani na matendo yake!

Kumekuwa na porojo nyingi eti Rais Bora ni yule anayetokana na CCM, ila kwa maoni yangu utashi wa Raisi husika ndio unatoa mwangaza wa ubora wa serikali anayoiongoza!
Mathalani, awamu ya tano ilikua ya kibabebabe, isiyosikiliza vilio vya wananchi kwa ujumla , ilitoa mamlaka kwa yeyote mwenye cheo kufanya akitakacho kwa wakat wowote mfano hai akiwa ni Makonda na Sabaya!
Lakini awamu ya sita imeonekana kuwa sikivu, inazingatia misingi ya utawala wa sheria, maovu yaliyofanyika awamu ya tano yanakatiliwa mbali huku Neema ikitangazwa haswa kwa wale waliodhulumiwa!

Nadhan Wana CCM Kuna Jambo la kujifunza hapa, mnapochagua mtu wa kumpa kiti Cha Uraisi, zingatieni utashi wa mtu mwenyewe, sio kuleta mtu anayesimamia misimamo yake hata Kama haina tija, sio kuteuwa mtu ambaye atakomoa upande wa pili wa Vyama pinzani nakati wote ni wanadamu safar yetu ni moja!

Mwisho kabisa!
Ashukuriwe Mungu anayejua mawazo ya watu, maana kwa akili ya kawaida sidhan Kama kungefanyika uchaguzi mngempendekeza Mama Samia kigombea kiti Cha urais, ila ni Mungu tu aliemjua toka mwanzo kuwa anaweza, na ameonesha dira kuwa Tanzania itakuwa na utawala unaozingatia misingi ya haki za Binadamu na sheria tofauti kabisa na mtangulizi wake!
Mungu alimfanya SSH kuwa makamu wa Rais kwa Makusudi yake. Tungehama nchi wengine.
 
Hii taarifa imenitoa majozi. Mungu ni mkubwa sana. Watanzania wenzangu, bila kujari itikadi za vyama vyetu, hili liwe fundisho, tusiruhusu nchi yetu kufanya makosa kama haya. Viongozi wanaochaguliwa kwa kura ni lazima waheshimu viapo vyao kwa maana ya katiba ya nchi. Hata hivyo tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupatia Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA. Mama Samia amewafuta machozi watu wengi sana katika kipindi kifupi sana.
....viongozi wanaochaguliwa kwa kura......Magu hakuchaguliwa kwa kura 2015
 
P..Mhe. JPM alikataa kuwa kwenye kampeni hakuahidi katiba mpya. Likumbuke Hilo.
Kwani aliahidi mangapi na mwisho wa siku alipindua uamuzi wake!.
  1. Aliahidi hafanyi kazi na wapinzani, what happened after?.
  2. Alitaka wazungu wa unga wanyongwe, hakunyonga hata mmoja!.
  3. Hivyo hata kama hakuahidi katiba, amini nakuambia, ilikuwa utuachie katiba mpya!.

P....Ni mpaka utupatie ushahidi wa unachosema bila hivyo utakuwa unatulisha kitu ambacho hakina ushahidi. Ila Kama aliwahi kutamka kwenye vikao vyenu vya Siri Basi tuambie. Vinginevyo.......
 
Pamoja na yote, kama Mungu asingemtwaa JPM, jee unajua angefika 2025, angekuwa the best president this nation had ever had, angetuachia katiba mpya!.
Nisome hapa

P
Pascal me ni mdau ninaefatilia Sana hoja zako, ILA kwa suala la Magufuli kuacha katiba mpya nadhan ulikua unaota ndoto mchana kweupe!
Umejisahaulisha ya kuwa Dalili ya mvua ni Mawingu , na huyo Bwana alikua na Dalili zote za udikteta na chuki kwa Vyama Pinzani?
Hiyo katiba mpya ingekuja vipi, Na Kati katiba iliyopo yeye na Ndugu yake Ndugai waliikanyaga Kama takataka huku wakijiwekea Kinga?

Muache Mungu aitwe Mungu, yeye huona mbali , mawazo yake si sawa na yetu, watu walikatishwa tamaa na awamu ya tano!
 
Kwani aliahidi mangapi na mwisho wa siku alipindua uamuzi wake!.
  1. Aliahidi hafanyi kazi na wapinzani, what happened after?.
  2. Alitaka wazungu wa unga wanyongwe, hakunyonga hata mmoja!.
  3. Hivyo hata kama hakuahidi katiba, amini nakuambia, ilikuwa utuachie katiba mpya!.
P
Alikua anamsubiri nani sasa miaka mitano zote? ni mpuuzi pekee ndiyeanaweza kuamini kua JPM alikua na nia njema na nchi hii; jamaa alikua na rohoo mbaya siyo kifani.
 
P....Ni mpaka utupatie ushahidi wa unachosema bila hivyo utakuwa unatulisha kitu ambacho hakina ushahidi. Ila Kama aliwahi kutamka kwenye vikao vyenu vya Siri Basi tuambie. Vinginevyo.......
Hakuna ushahidi wowote wala vikao vyovyote vya siri, bali mimi ni a good trends reader, nimekuwa nikimfuatilia Magufuli very closely, hivyo nikasoma trends zake nikajua, angetuachia katiba mpya.
Angalia tarehe ya bandiko hilo na uone hoja zake
P
 
Wasalaaaam!

Ni ukweli usiopingika kuwa, pamoja kwamba Rais Samia alikua Makamu wa Rais awamu ya tano, lakin hawakuwa kitu kimoja na Raisi wa awamu hiyo inangawa Rais Samia amejaribu kutuaminisha mara kadhaa akisema wao ni kitu kimoja!
Lakini kauli hiyo haiendani na matendo yake!

Kumekuwa na porojo nyingi eti Rais Bora ni yule anayetokana na CCM, ila kwa maoni yangu utashi wa Raisi husika ndio unatoa mwangaza wa ubora wa serikali anayoiongoza!

Mathalani, awamu ya tano ilikua ya kibabebabe, isiyosikiliza vilio vya wananchi kwa ujumla , ilitoa mamlaka kwa yeyote mwenye cheo kufanya akitakacho kwa wakat wowote mfano hai akiwa ni Makonda na Sabaya!

Lakini awamu ya sita imeonekana kuwa sikivu, inazingatia misingi ya utawala wa sheria, maovu yaliyofanyika awamu ya tano yanakatiliwa mbali huku Neema ikitangazwa haswa kwa wale waliodhulumiwa!

Nadhan Wana CCM Kuna Jambo la kujifunza hapa, mnapochagua mtu wa kumpa kiti Cha Uraisi, zingatieni utashi wa mtu mwenyewe, sio kuleta mtu anayesimamia misimamo yake hata Kama haina tija, sio kuteuwa mtu ambaye atakomoa upande wa pili wa Vyama pinzani nakati wote ni wanadamu safar yetu ni moja!

Mwisho kabisa!
Ashukuriwe Mungu anayejua mawazo ya watu, maana kwa akili ya kawaida sidhan Kama kungefanyika uchaguzi mngempendekeza Mama Samia kigombea kiti Cha urais, ila ni Mungu tu aliemjua toka mwanzo kuwa anaweza, na ameonesha dira kuwa Tanzania itakuwa na utawala unaozingatia misingi ya haki za Binadamu na sheria tofauti kabisa na mtangulizi wake!
Rubbish
 
Alikua anamsubiri nani sasa miaka mitano zote? ni mpuuzi pekee ndiyeanaweza kuamini kua JPM alikua na nia njema na nchi hii; jamaa alikua na rohoo mbaya siyo kifani.
Ubaya wake ni kwa vile alivyowabana wapiga deal. Sasa hivi wamekuwa wale wazuri, kuleni mpaka na miguu.
 
Back
Top Bottom