Hakuna ushahidi wowote wala vikao vyovyote vya siri, bali mimi ni a good trends reader, nimekuwa nikimfuatilia Magufuli very closely, hivyo nikasoma trends zake nikajua, angetuachia katiba mpya.
Angalia tarehe ya bandiko hilo na uone hoja zake
PElections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Wanabodi, Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha...www.jamiiforums.com
Big brain discuss ideas, fool mind discuss people😂😂😂😂😂😂😂Wasalaaaam!
Ni ukweli usiopingika kuwa, pamoja kwamba Rais Samia alikua Makamu wa Rais awamu ya tano, lakin hawakuwa kitu kimoja na Raisi wa awamu hiyo inangawa Rais Samia amejaribu kutuaminisha mara kadhaa akisema wao ni kitu kimoja!
Lakini kauli hiyo haiendani na matendo yake!
Kumekuwa na porojo nyingi eti Rais Bora ni yule anayetokana na CCM, ila kwa maoni yangu utashi wa Raisi husika ndio unatoa mwangaza wa ubora wa serikali anayoiongoza!
Mathalani, awamu ya tano ilikua ya kibabebabe, isiyosikiliza vilio vya wananchi kwa ujumla , ilitoa mamlaka kwa yeyote mwenye cheo kufanya akitakacho kwa wakat wowote mfano hai akiwa ni Makonda na Sabaya!
Lakini awamu ya sita imeonekana kuwa sikivu, inazingatia misingi ya utawala wa sheria, maovu yaliyofanyika awamu ya tano yanakatiliwa mbali huku Neema ikitangazwa haswa kwa wale waliodhulumiwa!
Nadhan Wana CCM Kuna Jambo la kujifunza hapa, mnapochagua mtu wa kumpa kiti Cha Uraisi, zingatieni utashi wa mtu mwenyewe, sio kuleta mtu anayesimamia misimamo yake hata Kama haina tija, sio kuteuwa mtu ambaye atakomoa upande wa pili wa Vyama pinzani nakati wote ni wanadamu safar yetu ni moja!
Mwisho kabisa!
Ashukuriwe Mungu anayejua mawazo ya watu, maana kwa akili ya kawaida sidhan Kama kungefanyika uchaguzi mngempendekeza Mama Samia kigombea kiti Cha urais, ila ni Mungu tu aliemjua toka mwanzo kuwa anaweza, na ameonesha dira kuwa Tanzania itakuwa na utawala unaozingatia misingi ya haki za Binadamu na sheria tofauti kabisa na mtangulizi wake!
Amechemka kidogo kwaajili ya furaha , huenda ni mwana chadema.