Wafu wapo wapi?

Masombogoto

Member
Sep 10, 2016
25
24
WAFU WAPO WAPI?

Karibu sana msomaji wangu, tujifunze kuhusu mada hii muhimu ambayo wengine wameipotosha kwa hadithi zao wenyewe na kuliacha neno la Mungu kando.

Ukiwa unasoma neno hili, ni muhimu sana uwe na biblia yako pembeni, ili ujiridhishe kwa yale niliyoyaandika hapa.

Kuna nadharia nyingi sana kuhusu kifo. Zingine zimeletwa humu JF na watu werevu, lakini bahati mbaya, hizo zote ni hadithi tu zisizo na msingi wa neno la Mungu.

Hebu tuanze pamoja.
Kaa na biblia yako karibu.

Uumbaji: Mwanzo 1;1-23 siku tano Mungu anaumba mtu.
Halafu pia kuna aina mbili za uumbaji
Kutamka ikawa (aya ya 24&25)
Kufinyanga (26&27)
Kwa upekee wa mwanadam, Mungu anaelezea zaidi ilivyokuwa katika Mwanzo 2:7, 21-23
Baada ya kumuumba mtu, mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Mwanzo 2:1-2

Kuna maneno makuu 3 ya msingi (kamusi ya TUKI 2004)
Uhai; ni kitu kinachowezesha kiumbe kuishi kwa kuendesha shughuli zake za kiwiliwili; kinyume cha ufu.
Kifo; ni tukio au tendo la kufikia mwisho wa uhai; mauti.
Mauti; ni hali inayomfanya kiumbe kukosa uhai

Kifo ni nini basi? Kifo ni kinyume cha kuumba.
Vitu vilivyotumika kumuumba mtu ni
Udongo (mavumbi ya ardhi)
Pumzi ya uhai

Mungu ndiye muumbaji.
Je, kifo kilisababishwa na nini?
Mwanzo 2:16,17 Mungu anampa Adam maelekezo ili asife
Mwanzo 3:1-6 Anguko la Adam na Hawa
Ufunuo 12:7-9 Nyoka ni Shetani

Ni nini kilitokea baada ya kuasi?
Mwanzo 3:7
Yalitokea yafuatayo:
Utukufu wa Mungu uliokuwa ukiwafunika ulitoweka
Wakajijua kuwa wako uchi
Wakatafuta mavazi yao wenyewe ili kuficha uchi wao
Mwanzo 3:8
Uhusiano/urafiki wao na Mungu uliharibika. Mungu akawa adui yao.
Wakaingiwa hofu
Wakamkimbia Mungu na kujificha.
Mwanzo 3: 9-16
Laana na maelekezo mapya yanatolewa

Fungu la 17-19
Visingizio vya Adam havikuepusha adhabu
Ardhi ikalaaniwa
Kama matokeo ya laana, miiba na mimeo mimgine yenye sumu ilitokea
Laana ya KIFO ikatangazwa. “Wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi”


NANI MKWELI? MUNGU AU SHETANI?
Mwanzo 2:16,17
Siku utakapokula matunda ya mti huo, UTAKUFA HAKIKA (kinyume cha uumbaji)
Mwanzo 3:4
HAKIKA HAMTAKUFA

NB: Kifo ni kitendo cha kufikia mwisho wa uhai

Je, baada ya kula tunda walilokatazwa, ni nini kilitokea?
Walipewa maelekezo mapya na hatimaye walifukuzwa.

Tukio la kwanza la kifo katika historia ya mwanadam, ni la Habili
Mwanzo: 4:1-7

Maneno aliyosema Shetani yaliweka msingi wa kile kinachojulikana leo kama IMANI YA MIZIMU.
IMANI YA MIZIMU ni mfumo wa imani au desturi ya kidini iliyojengwa juu ya kile kinachodhaniwa kuwa ni mawasiliano na roho za wafu. Falsafa yake ni kuwa roho ni kitu kinachoishi kwa kujitegemea nje ya mwili. Spiritualism, Oxford American Dictionary: Standard English-Swahili Dictionary 1997 Ed uk 524

UKWELI KUHUSU ROHO.
Kwa lugha ya kiingereza kuna maneno mawili tofauti yenye neno moja la kiswahili ambayo hayafanani maana.
Soul
Spirit
Yote yana neno moja la kiswahili. ROHO
Wengi huamini roho ni kitu fulani kisichoonekana ambacho pia hakifi (immortal) kinachoishi ndani yetu. Hivyo huamini mtu akifa, hiki kitu hutoka na huendelea kuishi nje ya mwili.

Kumbuka biblia imeandikwa kwa mara ya kwanza kabisa kwa kutumia lugha ya kiebrania na kigiriki (kiyunani). Mahali walipokuwa wakitaja ROHO (SOUL), walitumia neno la kiebrania ne’phesh au la kiyunani psy’khe’.
Haya maneno yamejitokeza kwenye maandiko zaidi ya mara 800 na walioitafsiri biblia wamekuwa wakitumia moja kwa moja kwenye aya au wakiweka kwenye tafsiri ndogo chini (rejea) (footnotes).

Kibiblia, neno roho (Soul) linapotumika kwenye maandiko humaanisha
watu/mtu (people)
Wanyama (animals)
Uhai (life) ambao mtu anao

Soul (watu)
1 Petro 3:20 ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. (A few people that is, eight souls, were carried safely through the water.
Kutoka 16:16 (according to the number of people (souls, footnotes)
Mwanzo 46:18, Joshua 11:11, Matendo 27:37 na Warumi 13:1 (aya zote hutumia neno souls (kwenye footnotes).

Saul (Wanyama)
Mwanzo 1:20 viumbe hai, Living creatures (soul, footnotes)
Mwanzo 9:10, Walawi 11:46, Hesabu 31:28 zote kuna maneno sauls (footnotes) ikimaanisha wanyama.

Soul (uhai wa mtu) life of a person.
Kutoka 4:19 .....waliokutaka uhai wako wamekwishakufa (“seeking your soul” footnotes)
Mwanzo 35:16-19 roho yake ikiwa inamtoka (“her soul was going out” footnotes)
Yohana 10:11 Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo (the fone shepherd surrenders his life (soul, footnote) in behalf of the sheep.
1 Wafalme 17:17-23, Mathayo 10:39, John 15:13, Matendo 20:10
Uhai wa mtu hutumiwa na biblia kama roho wa mtu (life of a person).

Hakuna sehemu yoyote wala fungu lolote katika biblia nzima inayoonesha kuwa roho (SOUL) haifi. Ila, biblia husema, roho (soul) inakufa. Ezekiel 18:4,20. Hivyo biblia husema mtu aliyekufa ni roho iliyokufa (dead soul) Walawi 21:11

ROHO PUMZI (SPIRIT)
Watu wengi hudhani roho (Spirit) ni neno sawa tu na roho (Soul).
Haya maneno ni tofauti kabisa japo kwa kiswahili ni neno moja.

Kwa kiebrania, neno roho (spirit) ni ru’ach au kwa kiyunani pneu’ma.
Biblia yenyewe inasema ni nini maana ya hili neno.
Kwa mfano, Zaburi 104:29 ....waiondoa pumzi yao, wanakufa. If you (Yehovah) take away their spirit (ru’ach) they die and return to the dust.
Yakobo 2:26 ....mwili pasipo roho (pneu’ma) umekufa. Without spirit, the body is dead.
Kiebrania, neno ru’ach inatafsiriwa sio tu kama pumzi (roho) bali pia kama nguvu (nguvu) (life force). Kwa mfano wakati wa gharika, Mwanzo 6:17, 7:15,22 .......niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, all the flesh that has the breath (ru’ach) of life.

Pumzi ya uhai ndiyo roho ambayo ni spirit sawa na ru’ach.
Mwili bila pumzi ni sawa na radio pasipo umeme.

MAHALI PEMA PEPONI
Kuna desturi mbalimbali kuhusu mazishi ya waliokufa.
Funeral Customs, World Book, Encyclopedia, F, Vol 7, 1965 ed,. Uk 482, 483
Mtu akifa, utukufu hautamfuata. Zaburi: 49:16,17

Kuzimu ni nini na ni wapi?
Ni kaburini. Zaburi 30:3. 89:48 na Mwanzo 37:35
Peponi ni wapi?
Ni paradiso, makao ya waliokombolewa watakapoishi baada ya ufufuo. Lika 23:43
Roho ni nini? (Spirit)
Ni pumzi ya uhai. Mwanzo 2:7 Ayubu 27:3 Zaburi 146:4 Mhubiri 12:7
Nafsi/mtu kamili Ezekiel 7:19 18:20, Ufunuo 6:9-11
Roho wa Mungu Isaya 63:10, 1 korintho 2:10,11
 
Jehanamu.

Bwana Yesu aliyekuwa akifundishwa kwa mifano, alitumia mfano kuwafundishwa wasikilizaji wake juu ya hukumu ya mwisho, yaani, Jehanamu. Lakini mahali alipopatumia Yesu kama mfano wa hukumu na ambapo baadhi ya walimu wa dini wamepahusisha na GEHENA. Hapa ni mahali ambapo palijulikana pia kama Tofedhi au bonde la mwana wa Hinomu. Hapo ni mahali ambapo mfalme Ahazi alifanya machukizo makuu mbele za Bwana kwa kuwateketeza wanawe motoni kama kafara na kuleta uasi mkuu katika Yuda Mambo ya nyakati 28:1-4.
Kutokana na maasi hayo, Bwana alitabiri kupitia kwa nabii Yeremia kwamba siku zinakuja ambapo mahali hapo hapataitwa tena kwa majina ya awali, bali pataitwa Bonde la machinjo wakati atakapowapatiliza wayahudi kwa sababu ya uovu wao Yeremia 7:30-34.

Mwanahistoria mmoja wa kiyahudi anaeleza kuwa, wakati Bwana Yesu akiwa hapa duniani, mahali hapo Gehena palokuwa ni dampo, yaani mahali ambapo takataka za mji zilikuwa zinakusanywa na kuchomwa. Sasa, kwa sababu ya takataka na uozo wa kila siku katika madampo, moto wake ulikuwa hauzimiki na pia funza wake walikuwa hawafi kutokana na uwepo wa mazingira hayo ya uchafu tuliyoyataja. Kwa hiyo, Bwana Yesu akatumia mfano huo (Marko 9:43-48) kuonesha jinsi ukali hukumu ya mwisho kwa waovu utakavyokuwa katika ziwa la moto na kuonesha kuwa moto huo utateketeza kila kilichomo na kuwa majivu. Lakini fikiria endapo takataka zitakoma kutupwa kwenye dampo. Je, moto utaendelea kuwaka bila kuwapo takataka za kuteketezwa? Au je, funza wanaweza kupatikana mahali ambapo hakuna takataka na uozo wa kudumu? La hasha.

Ni mahali hapo (Gehena) ambapo Yesu alipatumia kama mfano . Ndipo ambapo baadhi ya walimu wa dini wametafsiri kuwa ni mahali maalum huko ahera palipo makazi ya waovu baada ya kufa, au motoni, jambo ambalo sio kweli.

Kanuni iliyotumika kuumba ni;
Mavumbi ya ardhi + pumzi ya uhai = Nafsi hai

Ili mtu awe amekufa ni kinyume cha kanuni ya hapo juu.
Mavumbi ya ardhi - pumzi ya uhai (roho) = Maiti (mavumbi ya ardhi)

Je, mavumbi yalikuwa hai kabla ya Mungu kupulizia pumzi? HAPANA.
Je, ile pimzi ya uhai ilikuwa nafsi hai kabla ya kupuliziwa katika umbile la Adam (Mavumbi)? HAPANA.
Ni pumzi ya uhai, sio nafsi hai. Pumzi hii pia huitwa roho (spirit)
Ayub 27:3, 32:8 kinachotupatia uhai na akili ni pumzi ya Mungu ya uhai, ikitoka, humfanya mtu awe amekufa.
Kumbuka, Mungu alisema utakapokula matunda ya ule mti, UTAKUFA HAKIKA.
Ayubu 7:6-10 Maisha ni upepo
Zaburi 146:4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake
Mhubiri 9:5 Wafu hawajui neno lolote.

Aliyekufa, hajui chochote. Mawazo yake yanapotea. Jicho halitaona tena. Yeye hataonekana tena. Hatazuka tena kabisa. Hatorudi nyumbani kwake tena.

WAFU WANAKWENDA WAPI?
peponi
Jehanam
Toharani au
Kaburini.
Mwanzo 3:19 Kwa maana u mavumbi wewe, na mavumbi ni utarudi.
Ayubu 14:10-12 Mwanadam hulala chini, asiinuke tena.
Zaburi 104:29 kuyarudia mavumbi yao.
Zaburi 146:4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake.
Mhubiri 12:7 mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa.
Isaya 26:19 amkeni ninyi mnaokaa mavumbini.
Hosea 13:14 Nitawakomboa na nguvu za kaburi.
Daniel 12:2 waliolala katika mavumbi ya nci wataamka.
Yohana 5:25-29 walio kaburini wataisikia sauti yake nao watatoka.
1 thesalonike 4:13-15 hatutawatangulia waliolala mauti.
Mhubiri 3:19,20 wanadamu na wanyama wana pumzi moja. Anavyokufa huyu, ndiyo anavyokufa huyu.

Baadhi ya vifo vya watumishi wa Mungu.
Ibrahim. Mwanzo 25:8,9
Isaka. Mwanzo 35:29
Yakobo. Mwanzo 49:29-33
Musa. Torati 34:5,6
Waebrania 11:13-16

MIZIMU NA MIZUKA: NI ROHO ZA WAFU AU MASHETANI?

1 Samwel 8:4-9, 12:16-19, 9:15-17
Haukuwa mpango wa Mungu Israel kuwa na mfalme mwingine tofauti na Mungu mwenyewe. Lakini walipohitaji kwa nguvu, Mungu aliwapa.
Awali Sauli alikuwa mwema na mtiifu kwa BWANA.
Baadaye, akaasi. 1 Samwel 10:1, 7-9, 13:4,8-14 15:1-28
1 Samwel 25:1 Roho wa Bwana akamwacha Sauli.

Kumbuka, katika kitabu cha Kumbukumbu la torati 18:9-13 Bwana alikataza uchawi, kupiga ramli, bao, ubashiri, kuomba wafu n.k hivyo Mungu hahusiki na hayo mambo.

1 Samwel 28:3-14 Samweli (nabii) amekufa, wafilisti wanataka kupigana vita na Israel. Sauli akaenda kwa mwanamke mwenye pepo wa utambuzi.
Kumbuka kwa kufanya hivyo, ni kukiuka maagizo ya Mungu (torati 18:9-13)
Bwana alikuwa amemwacha Sauli. Hivyo alikuwa upande wa Shetani 100%

Zingatia yafuatayo.
Yule mwanamke alimtambua Sauli japo hakujitambulisha. Si ajabu kwa wenye pepo, waweza kukueleza mambo yako bila wewe kuwaeleza.
Mwanamke amnasema anaona mungu anatoka katika nchi (aya ya 13)
Alipoulizwa huyo mungu anafanana na nini? Alisema, ni mzee anazuka, naye amevikwa vazi
Sauli akatambua ni Samweli.
Inawezekana kabisa Sauli hakumwona huyo aliyezuka, ambaye mchawi alimwita mungu, lakini Sauli anamtambua kama Samweli.
Je, ni Samwel kweli? mungu anaweza kuzushwa na mchawi? Huyo mungu anatoka ardhini, je, MUNGU anaishi ardhini? Aliyezuka, ni aliyezungumzwa katika Yohana 12:31, 14:30, 16:11
Katika 2 Wakorintho 11:14 biblia husema, Shetani anaweza kujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Kilitokea nini baada ya mkasa huo?
1 Samwel 28:15-20

Mfalme Daudi anauguliwa na kufiwa na mwanaye. Ni nini alifanya?
2 Samwel 12:16-23
 
Wafu wako kaburini.
"Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mnele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa ALIFARIKI AKAZIKWA na kaburi lake LIKO kwetu hata leo". Matendo ya Mitume 2:29
 
Nitaleta aya tata ndani ya biblia kuhusu mada hii muhimu ya kifo, na maana zake.

Maana naona wengi wana hadithi zao tu zisizoungwa mkono na NENO LA MUNGU na bahati mbaya, watu wengi ndo wanapenda huo uongo kuliko ukweli.
 
Nitaleta aya tata ndani ya biblia kuhusu mada hii muhimu ya kifo, na maana zake.

Maana naona wengi wana hadithi zao tu zisizoungwa mkono na NENO LA MUNGU na bahati mbaya, watu wengi ndo wanapenda huo uongo kuliko ukweli.
Asante kwa mchango na changamoto lakini mimi huwa majaribu kuandika vile visivyosemwa na kujaribu kuinua hisia za utafiti kwenye ulimwengu mwingine nje ya maandiko matakatifu lakini ikiwa kuna kuwiana fulani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom