Wafaransa, waswisi vinara kuvaa soksi zinazonuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafaransa, waswisi vinara kuvaa soksi zinazonuka

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Nov 8, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  GENEVA

  UTAFITI uliofanywa na kampuni ya Uswisi ya Blacksocks umeonesha kuwa asilimia 66 ya wanaume wa kifaransa hubadili soksi zao kila siku, huku kila watu saba kati ya 10 wenye asili ya Uswisi ndiyo huvaa pea ya soksi safi kila siku.Inabanishwapia kuwa wanaume wa Kijerumani na Waingereza asilimia 78 huvaa soksi safi kila siku, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa watu 3000 katika nchi sita.
  Hiyo ina maana kuwa wanaume wa kifaransa au kiswisi ndiyo wanaoongoza kwa kuvaa soksi zinazonuka kuliko wajerumani au waingereza.
  Kwa ujumla, asilimia 77 ya wanawake na wanaume waliofanyiwa utafiti walibadili soksi kila siku, wakati asilimia 11 walisema hubadili baada ya siku moja au mbili.

  Asilimia nne huvaa soksi safi kila baada ya siku tatu, asilimia moja hubadili mata moja tu katika wiki.
  Uwiano wa kubadili soksi ulikuwa ukilingana na idadi ya soksi ambayo muhusika anamiliki.

  Wanaume wa kijerumani wameonekana kupenda kuwa na soksi, ambapo kwa wastani mtu humiliki hadi pea 24. Wanaume wa Austria huwa na pea 23, wakifuatiwa na Waswisi kwa pea 22

  Spoti Starehe | www.spoti.co.tz

  Kumbe hata Wazungu wananuka miguu Fangasi hahahahahahahahh
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ukifanywa kwa bongo sijui utakuja na majibu gani!
   
 3. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Wabongo wanaonuka itakuwa 98%
   
Loading...