Wafanyakazi Zain wamshitaki mwajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi Zain wamshitaki mwajiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Aug 5, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  na Amos Nyaigoti

  WAFANYAKAZI tisa waliokuwa waajiriwa wa Kampuni ya simu za mikononi ya Zain, wameishitaki menejimenti ya kampuni hiyo katika Mahakama ya Kazi jijini Dar es Salaam, wakidai fidia ya sh milioni 412, kama malipo ya stahili zao pamoja na malipo ya adhabu kwa kampuni hiyo.

  Wakizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kupitia wakili wao, Tundu Lissu, alisema kuwa wateja wake waliachishwa kazi kwa madai ya kuyumba kwa uchumi na shauri hilo linapingwa vikali na wafanyakazi hao ambao waliamua kuishitaki kampuni hiyo mahakamani.

  “Sheria inamtaka mwajiri mara tu anapofikiria kuwapunguza wafanyakazi wake ni lazima awataarifu kwa maandishi na kuwapa vigezo vya upunguzaji huo, ikiambatana na malipo yao, ambapo hilo halikufanyika,” alisema Lissu.
  Lissu alidai kuwa wateja wake walifukuzwa si kwa sababu za kiuchumi kama walivyodai bali chuki ya kumpuni kwa wafanyakazi hao, kwa kuwa mwaka jana Zain iliongeza asilimia 50 ya wafanyakazi.

  Alisema mapato ya kampuni hiyo yaliongezeka kwa asilimia 30 mwaka jana kama faida na kuifanya kampuni hiyo iongoze kwa mapato barani Afrika kwa kampuni zote za Zain.

  Alisisitiza kuwa wateja wake walifukuzwa kwa chuki kwani siku ya tukio, watano kati yao walikuwa wamepangiwa safari za mikoani na waliporipoti ofisini walipewa barua za kufukuzwa kazi, huku wawili kati yao wakipewa taarifa ya kufika makao makuu Dar es Salaam kutoka Iringa kwenye mkutano na walipofika walipewa barua za kufukuzwa kazi.

  Lissu alieleza zaidi kuwa wateja wake walituhumiwa kukiuka taratibu za ofisi ambapo kampuni ilishindwa kuthibitisha hilo na kumfukuza kazi mmoja wa watumishi hao.

  Wote kwa pamoja baada ya kupewa barua hawakuruhusiwa kuingia ofisini na malipo yao yalienda kulipia madeni yao katika Benki ya Kenya Commercial Bank (KCB) ambapo ni kinyume cha sheria za kazi. Wafanyakazi hao wanaiomba mahakama itoe tamko kuwa walifukuzwa kazi kinyume cha sheria, warudishwe kazini kwa nafasi zilezile na mahakama iamuru walipwe mishahara na malipo yote kwa kipindi chote walichosimamishwa kazi. Kesi hiyo namba 34/2009 imeahirishwa hadi Septemba 9, mwaka huu
   
 2. B

  Bata Senior Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  lol,kazi ipo.

  kulipa madeni yao KCB?nadhani ukiomba mkopo kuna mda maalum wa kurudisha pamoja na riba??sasa watawalipaje KCB na pengine mkopo ni wa miaka mitatu?hapo wamekosea.

  poleni sana kwa mlichofanyiwa .
   
 3. K

  Kachero JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni unyanyasaji na wana haki zote za kudai malipo yao,huwezi kumwachisha mtu kazi na usimlipe stahili zake.Kama ana deni benki hilo ni juu yake namna ya kulilipa sio kufanya mambo kenyeji hii inaudhi sana Ghrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sijui sheria italisemeaje, sema usikute Zain wajanja walisha wasainisha mkataba wa ajira wa ovyo ovyo wenye masharti ya kijinga kama haya ya mtu kutoka nyumbani kagombana na mkewe anafika anakufukuza kazi! ( si unajua zetu wabongo unaanguka sahihi kabla huja jiridhisha na yaliyomo kwenye mkataba?) Vinginevyo ina tiisha huruma sana, unafukuzwa kazi hata nauli ya dala dala unanyanganywa inaenda lipa mkopo?

  Huku ni kumalizana ki aina!
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  i think ZAIN will learn the lesson the hard way
   
 6. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Yaani hapa Zain hawatoki;nasema hivi hawatoki na kama wakitoka hakuna sheria itakayokuwa imetumika ipasavyo zaidi ya mkono wa mtu/watu wenye interest zao ndani ya kampuni wakaamua kucheza foul mpaka ndani ya mahakama.
  Yaani kama ningepewa hii kesi niitolee maamuzi yaani ni sawa na kusema Zain wamefulia zaidi kuliko kuoshea.
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Na itakuwa funzo pia kwa makampuni mengine yanayofanya mambo hovyo hovyo.
   
 8. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #8
  Aug 5, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza kwa kujua wakili gani awasaidie. Mbele ya Tundu Lisu kesi hii ZAIN hawatoki. Kwishnei!
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .

  Tuseme mbele ya sheria na sio mbele ya Tundu Lisu. Kwani Huyo Tundu atatumia sheria hizo hizo kutetea wateja wake.

  Suala linazungumzika linaweza kumalizwa hata nje ya mahakama. Sitaweza lijadili sana sababu shauri bado lipo mahakamani.

  Nasriyah
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  wapewe haki zao ndo hawa waajiri sijui kwa nini huwa wanaamua kujichukulia sheria wanazojua wenyewe
   
 11. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Let leave the matter to the court. Ukweli utajulikana huko huko kortini.
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ...kama vile unataka kumnyima uhuru wa kutoa maoni vile...!
   
 13. O

  OkSIR Senior Member

  #13
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Quote:
  [​IMG]

  Let leave the matter to the court. Ukweli utajulikana huko huko kortini.  ...kama vile unataka kumnyima uhuru wa kutoa maoni vile...!

  lazima wawepo.....usikate tamaa toa maoni yako kusaida watanzania wenzako.....
   
 14. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  maoni yoyote yatakayo toka hapa sidhani kama yatabadili sheria zilizoko sanasana tutakuwa tunasypath nao tu kama kweli tunataka kuwasadia watanzania wenzetu basi bora tuchangishane tuwalipie gharama za wakili na sio blah blah, habari ndio hiyo
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Sasa wanataka kipi, kulipwa fidia, kurudi kazini au both?

  Wanaweza kushinda the above lakini suala la kurudishwa kazini bado Muajiri akaamua kuwalipa na kuwatimua badala ya kuwa-reinstate (as per labour law). Let's Hope for the best!!
   
 16. N

  Nangetwa Senior Member

  #16
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  lets wait and see coz whatever is said or reported is not the correct test for making judgement mainly on matters which are pending in court. my experience with legal matters, my profession, has tought me that what matters is how one build his case with clear reference to legal position applicable in the matter. there is a lot in labour matters that may lead to dismissal of the case from technical to substantive issues. so my advice is let wait and see.
   
 17. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Yapo matunda makubwa tu ya zoezi hili la akina Tundu Lissu hata kama hawataweza kupata wanachokidai. Hii itapunguza mambo ya hovyo hovyo. Itajenga muamko na upeo tofauti kwa wafanyakazi na wananchi wanaonyanyasika pasipo kujua namna gani wanaweza kusaidika.

  Isitoshe, kuna wanasheria wengi tu wamelala wanasubiri "kuwezeshwa"; wanabaki kulalamika maslahi yao duni wakati opportunities ziko tele.
   
Loading...