Wafanyakazi wote kesho 31.10.2010 ndiyo zamu yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wote kesho 31.10.2010 ndiyo zamu yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Oct 30, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF,Ndugu wafanyakazi na wale wote wanaowategemea, kesho ndiyo siku tuliyokuwa tunaisubiri kwa hamu ya kumdhihirishia Kiwete kuwa Wafanyakazi si watu wa kubeza,kudharau,kutukana na kuwatisha hadharani. Kiwete ALIKATAA KURA ZETU KUWA HAZIHITAJI KWENDA IKULU maana hawezi kutulipa mshahara wa Tshs 350,000/=.Kesho lazima Mkwere tumshikishe adabu maana asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu.

  Tuko wafanyakazi zaidi ya 400,000. Kwa hesabu za haraka haraka kila mfanyakazi ana wategemezi wastani wa watu 10. Hivyo basi 400,000 x 10 ni sawa na KURA MILIONI 4. Hii inakaribia kama 25% ya wapiga kura wote. BADO WALALAHOI NA VIJANA WANAO KADIRIWA KAMA MILIONI 5+. Ukikokotoa hapa unakuta kwamba hesabu ya Wafanyakazi,Vijana +Walalahoi inakaribia kwenye MILIONI 9! JE, KWA IDADI HII YA KURA HATUJAMWEZESHA DR.SLAA KUTINGA IKULU ILI AANZE KUFANYA VITU VYAKE VYA KUTUPELEKA KWENYE TANZANIA YENYE NEEMA?

  Jamani tusije tukajidhalilisha wenyewe hiyo kesho. Nitashangaa na kusikitika sana kama DR.SLAA HATAZIPATA KURA HIZI WALAU HATA 3/4 YAKE(about 7m+) . Shime wafanyakazi wenzangu,vijana,walalahoi na wapenda maendeleo wa nji hii.

  CHAGUA DR.SLAA(DR. WA KWELI) KWA MABADILIKO YA KWELI.
   
 2. c

  chanai JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo ndo tunalolitegemea. kazi ya usiku wa leo ni kuendelea kuhimizana watu tukapige kura pamoja na wasaidizi na wategemezi wetu. Atajua kuwa wafanyakazi ni wa muhimu kwenye nchi hii
   
 3. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Its our turn. Jk alimaliza zamu yake siku ile alipotudharau na kutudhalilisha akiwa na wazee wa Dar (Sijui kati ya wale wazee nani ni mwajiriwa!). Tutamchagua Slaa akarekebishe mambo ikiwa ni pamoja na kupunguza mishahara ya wabunge na Rais
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna kanuni za kiuhasibu zinaitwa conservatism/prudence. Yaani unaassume woote watapiga kura, halafu woote watapigia CCM hadi Kikwete. Na hao vijana pia. Kiuhalisia CHADEMA walianza kampeni vizuri saana ila hapa mwishoni upepo umegeuka.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yaani nilisahau hili sie mbayuwayu wacha tukamuajiri rais wa awamu ya tano kwa manufaa yetu. Maani sie ndio waajiri wake. JK alisema yeye ndie mwajiri wetu na sie ndio mwajiri wake pia.
   
 6. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  safi
   
Loading...