Wafanyakazi wa Ndani: Je, Hausigeli Huyu Ana Kosa?

Hili suala ni nyeti na linahitahi uchambuzi yakinifu. tatizo tunategemea habari what we read na sometimes huwezi kupata flavour. Anyway nimesoma kwa makini na kufikia haya yafuatayo.

Binti ana makosa kwani amefeli duty of care kwa kichanga ambaye alikuwa anamtgemea100%. mtoto wa umri wa miezi 8 is helpless, hivyo wajibu wa kwanza ilikuwa ni kuhakikisha kuwa yuko salama at all times wakati huyu binti akiwa incharge no matter what.

Pili kama alikuwa na grievances na mwajiri wake na hata majirani wameproovu hivyo wangemshauri aende hata polisi au ustawi wa jamii kulalamika rather than kulipiza kisasi kwa mtoto mchanga.
comments: Polisi pamoja na mambo mengine waliatakiwa ama wanapaswa kumpeleka katika psychiatric tests ili kudetermine kama ana matatizo ukichaa au la. waweza kumhukumu kumbe ni mgonjwa wa akili.

3. mcsichana wa miaka 16 kwa sheria za Tanzania si halali kuajiriwa kama yaya. ni underage, hana mafunzo ya uyaya, kwa makosa yake inabidi yapelekwe katika Juvinale cases. maana angekuwa na miaka 18 hapo angeweza kuimbishwa kindumbwendumbwe kisawasawa na polisi na mahakama.

Wakati wana imterview ilitakiwa kuwepo na mtu mwingine kama kutoka ustawi wa jamii na sio polisi peke yake. kwani ni rahisi kubadili kauli kama alivyofanya ikiwa atatishiwa.

THerefore kosa analo tatizi ni means zitakazotumika ku process kesi ndiyo nina mashaka.

mwajiri wake inabidi naye atinge kizimbani kwa kumwachia mtoto kuwangalia mtoto mwingine.
 
Malaika mungu akulaze pema peponi

Wampeleke huyu binti wa 16 yrs kupimwa kama ni sane or not
inaweza kuwa mwajili wake walikuwa wanamtreat vibaya humu ndani

maana hii kitu sidhani ni pesa tu zimemfanya aue. mie naona wamwingie ili wajue y alifanya hivyo sio kusikiliza maneno ya watu tu aseme mwenyewe itasaidia kusave maisha ya watoto wengine

wanaweza wakawa walimpiga, hawakumpa chakula cha kutosha, mme alimutaka ingia or alimwingia or mwanamke alimfanya kama pumba na labda walikuwa wanamtukana pia kiasi cha yeye kuwalipizia

Background yake huyo binti ni ipi? Je walipomchukua ni wapi labda alihaidiwa elimu na etc

Maisha
 
naona wote mmechangia vizuri. kwa nyongeza tu hata mwandishi naye amekosea. kwa mujibu wa sheria za watoto mtoto chini ya miaka 18 akifanya kosa hatajwi jina bali tunasema jina linahifadhiwa. hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania hatujui haki za mtoto. kwa kweli kwa hili hata mahakama yoyote lazima itamlinda huyu mtoto.

kwa yule aliyetoa ushauri kuwa grievance za mtoto hausigeli zingepelekwa polisi sidhani kama ni practical. mtoto katoka dom hiyo polisi ataijua wapi? ataenda polisi saa ngapi wakati kichanga ndiyo hicho kinamganda na klia saa zote?

majirani walikuwa wapi wasimtetee alipwe mshahara?

mi nadhani huyu mtoto aachiwe huru arudi dom. adter all kifo hupangwa na mungu na yule mtoto mchanga aliandikiwa afe hivyo.

tuendelee kujadili
 
Nilimsokomeza khanga mdomoni asinipigie kelele`

2008-01-25 08:34:43
Na Devota Kabuta


Msichana anayefanya kazi za ndani, Tabu Isaya (16) ambaye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kumuua mtoto wa mwajiri wake, alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sinza Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo ya awali.

Msichana huyo ambaye alifikishwa mbele ya hakimu, Hilda Lyatuu wa mahakama hiyo katika maelezo yake alidai kuwa, aliamua kumweka mtoto huyo kipande cha khanga mdomoni kwa lengo la kumnyamazisha asiendelee kulia ili aweze kufanya kazi zake haraka.

Alidai kuwa, siku hiyo, Jumatatu Jan 21, saa 4:00 asubuhi, mama wa mtoto aliondoka nyumbani kwenda kazini na kumwachia vyombo vingi sana pamoja na kazi za kufagia uwanja na kufua nguo za mtoto na za kwake.

Alidai kabla hajaanza kazi hizo mtoto huyo alianza kulia na ndipo akaamua amwekee mdomoni kipande cha khanga kisha akamziba mkono mmoja mdomo na mwingine puani kama kwa dakika mbili hivi kwa lengo la kumnyamazisha.

Alidai alipomziba mtoto huyo alianza kutupatupa mikono na miguu kisha akanyamaza.

Alidai kuwa, alipoona amenyamaza alimtoa kipande kile cha khanga mdomoni, lakini alishangaa kumwona hapumui na ndipo alipogundua kuwa amekufa.

Alidai alichukua gauni lake na kuuviringisha mwili wa mtoto huyo kisha akachukua mfuko na kumweka ndani ya mfuko na kumbeba mgongoni.

Alidai alitoka na kwenda mpaka makaburi ya Manzese na alipofika alimtupa mtoto huyo sehemu yenye takataka jirani na makaburi hayo.

Alidai kuwa, alipomtupa aliondoka na kwenda kwa bibi wa mtoto huyo ambaye walikuwa wakiishi naye jirani na kumwambia kuwa mtoto ameibiwa na vijana wawili waliokuwa na mwanamke mmoja.

Alidai bibi huyo alimwambia amsubiri hapo nyumbani ili akamwite mama yake kazini.

Alidai mama yake alipofika huku akilia kwa hasira alimrukia na kuchanachana nguo alizokuwa amevaa na baadaye walimpeleka polisi.

Alidai huko polisi alisema anamtambua kijana mmoja ambaye alimtaja kwa jina la Rajabu wanayeishi naye jirani akidai pamoja na mwenzake ndiye aliyeshiriki kumwiba mtoto huyo.

Msichana huyo alidai polisi walimfuata Rajabu lakini licha ya kupigwa sana alikataa kuwa hakumwiba mpaka polisi wakaamua kumwachia.

Alidai polisi walimgeukia na kumpiga sana pamoja na kumbamiza ukutani na chini na ndipo alipoamua kuwaambia ukweli ili wasije wakamuua.

Alidai aliwaeleza kuwa mtoto huyo amemuua na kwenda kumtupa makaburini Manzese kutokana na hasira kwani alikuwa akilia na alikuwa na kazi nyingi, akaamua afanye hivyo amalize kazi kabla ya sasa nane ili mama yake atakaporudi asigombezwe.

Alidai aliwapeleka polisi na gari mpaka kwenye makaburi hayo na kuwaonyesha maiti ya mtoto huyo ambayo ilikuwa imebadilika na kuwa nyeusi.

Msichana huyo alidai kuwa, hakumuua mtoto huyo kwa kunyimwa mshahara kwani alikuwa akipewa mshahara wake kama kawaida isipokuwa aliamua kusema hivyo kwa kuwa walikuwa wakimhoji hoji sana.

Alidai mwajiri wake alimtorosha kutoka kwa wazazi wake mkoani Dodoma ili aje kufanya kazi kwake jijini Dar es Salaam kwa mshahara wa Sh. 20,000 kwa mwezi.

Alidai alimtorosha kwa kuwa baba yake alikuwa akitaka kumuoza kwa Mmasai wakati umri wake ulikuwa mdogo.

Alidai hapo nyumbani walikuwa wakiishi na mama huyo pamoja na mtoto aliyemuua lakini baba wa mtoto huyo alikuwa akija kulala mara moja moja.

Alidai mwajiri wake ana watoto wengine wawili ambao wanaishi Dodoma wilaya ya Kondoa.

Wakati huo huo, Joseph Mwendapole anaripoti kwamba Mama wa mtoto aliyeuawa kwa kunyongwa hadi kufa na msichana wa kazi za ndani, Asia Ali (28), amekiri kuwa hakuwahi kumlipa mshahara mfanyakazi wake tangu amchukue kutoka nyumbani kwao Dodoma.

Mtoto aliyeuawa ni Renaida Sebo aliyekuwa na umri wa miezi minane.

Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake Manzese Penisula, Bi. Asia alisema alimchukua msichana huyo mwaka jana kutoka kwa mama yake mzazi lakini hakukuwa na makubaliano ya kumlipa mshahara.

``Mama yake aliniruhusu kuja naye Dar es Salaam lakini hatukuzungumza kuwa nitakuwa namlipa mshahara, sasa nashangaa kama anasema sikumlipa mshahara kwa kuwa hatukukubaliana hivyo,`` alisema.

Alisema tangu waanze kuishi pamoja wamekuwa wakiishi maisha ya furaha na mtuhumiwa huyo hakuwahi kuonyesha chuki kwake wala kwa mtoto.

Alieleza kuwa siku ya tukio hilo juzi yeye alikuwa katika biashara zake Ubungo na ndipo alipojulishwa na ndugu zake kuwa mtoto wake ameibiwa.

``Baada ya kufanya unyama wake akaja kusema kuwa kaibiwa mtoto na majirani na ndugu wakaenda hiyo sehemu aliyoporwa lakini baadae iligundulika kuwa ni uongo,`` alisema.
 
Wakuu,

Hili jambo tumewahi kulijadili mara nyingi hapa, inaelekea wengi wetu tunanyanyasa wafanyakazi wetu wa ndani. Hatuwapi haki wanazostahili na bado tunawaachia watoto wetu tukitegemea watawalea kwa mapenzi yote.

Hii ni wake-up call kwa wengi wetu. Tunahitaji kutoa haki kwa wanaotutegemea kama vile sisi tunavyohitaji kutendewa haki na waajiri wetu pamoja na serikali.

Binafsi huwa nasikitishwa sana na unyanyasaji unaofanywa na hasa middle class wa Tanzania kwa wafanyakazi wa ndani.

Ndio tunahitaji wafanyakazi wa ndani lakini kwani lazima tuchukue watoto ambao wanatakiwa wawe shuleni? Lazima tuwafanyishe kazi masaa 15 kwa siku?
 
Hii, iunganishwe kule hoja nzito.. kwani ipo tayali inaendelea

Mkuu,

Sawa, lakini tungeweza pia kuiacha hapa na kujadili hata kwa siku maana hili ni tatizo kubwa kwa TZ.

Bahati mbaya wengi wetu hapa ndio tunaongoza kuajiri watoto wadogo na kuwafanyisha kazi masaa kibao kwa siku.
 
I think kama umesoma makini mistari niliandika with the help of Majirani hao aliokuwaakilalmika kwao kama raia wema wangefanya kitu but no one cared. mwisho ni sheria mkononi.'Pili kama alikuwa na grievances na mwajiri wake na hata majirani wameproovu hivyo wangemshauri aende hata polisi au ustawi wa jamii kulalamika rather than kulipiza kisasi kwa mtoto mchanga.'
 
Mtanzania,

Hakuna kitu ninachokilaani maishani kama ku-take advantage over mwingine kwa sababu ya uwezo........haina tofauti na UFISADI.

namuonea huruma huyu msichana......nafikri alifanya kitendo kile out of frustrations ambazo na sisi WANACHI.........."God Forbid" isije ikatufika siku moja
 
Pamoja na hoja zenu nzuri hapa kuna tatizo kila upande

1. Msichana hakupaswa kumaliza hasira zake kwa kachanga. Tena hasira mbaya ya kukatisha uhai wa mtu asiye na hatia.

2. Kama kweli ikithibitika kuwa na umri chini ya miaka 18, mwajiri pia ana hatia ya ajira mbaya ya watoto. Mara nyingi sisi watu wa vijijini umri wetu ni wa ku "guess" tu. Huyu bint anaweza kuwa na zaidi ya miaka 16 au chini yake. Sisi hatuna cha birthday kwa hiyo si rahisi kukumbuka umri wa mtoto. Siku ta kwenda kumwandikisha shule mzazi anaamua tu aseme mwanae ana miaka mingapi.

3. Taratibu za kisheria pia zimekiukwa. Huyu binti ni minor na anapaswa kulindwa.
 
MaMkwe, kwa kweli umeongea kitu muhimu sana hapo juu... Leo naona msichana amepelekwa mahakamani lakini inaonekana hawkuongelea swala la kwamba ni mtoto mdogo (less than 18yrs, only 16yr old).... Sijui sheria haswa inasemaje lakini kwa ufahamu wangu katika umri huo wa miaka 16 (ikithibitishwa) haiwezekani tumhukumu kama mtu mzima....

Najua kosa limetendeka na msichana huyu lakini jamani sheria inatakiwa imlinde pia!!
 
MaMkwe, kwa kweli umeongea kitu muhimu sana hapo juu... Leo naona msichana amepelekwa mahakamani lakini inaonekana hawkuongelea swala la kwamba ni mtoto mdogo (less than 18yrs, only 16yr old).... Sijui sheria haswa inasemaje lakini kwa ufahamu wangu katika umri huo wa miaka 16 (ikithibitishwa) haiwezekani tumhukumu kama mtu mzima....

Najua kosa limetendeka na msichana huyu lakini jamani sheria inatakiwa imlinde pia!!

Atalindwa na nani? Hata magazeti yameisha mhukumu. Kwenye jamii yetu watoto kama hawa ni expendable. Haikosi yuko rumande ya watu wazima, inawezekana akawa asusa ya maaskari. Mwisho wa yote atahukumiwa kifo na tutamsahau! Wako wapi hao mawakili mashujaa wanawake wasioogopa kukemea rushwa? Hamna maslahi hapa. Just another statistic. Shame on us all.
 
Back
Top Bottom