Wafanyakazi wa Ndani: Je, Hausigeli Huyu Ana Kosa?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,775
6,588
Hausigeli amnyonga mtoto wa bosi wake

2008-01-24 10:08:25
Na Joseph Mwendapole


Msichana anayefanya kazi za ndani maeneo ya Manzese, Dar es Salaam, Tabu Isaya (16), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kumuua mtoto wa mwajiri wake na kisha kuutupa mwili wake makaburini.

Sababu za Taabu kuchukua hatua ya kumuua mtoto huyo wa miezi minane inadaiwa kuwa ni hasira za kutolipwa mishahara ya miezi sita hadi sasa na mwajiri wake huyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi na kwamba mtuhumiwa huyo atafunguliwa mashtaka ya mauaji.

Jirani wa eneo alilokuwa akifanya kazi msichana huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema msichana huyo alikuwa akilalamika mara kwa mara kutolipwa mshahara kwa muda mrefu na mwajiri wake.

Alisema msichana huyo ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma na alikuwa akiishi na mwajiri wake maeneo hayo.

Alisema wakati wa tukio hilo, mama wa mtoto huyo, Bi. Asia Ali alikuwa katika biashara zake maeneo ya Ubungo.

``Mara kwa mara alilalamika kuwa halipwi mshahara na aliahidiwa kuwa mwezi Desemba mwaka jana angelipwa malimbikizo yake lakini baada ya kuona halipwi akawa anataka kurudi kwao Dodoma,`` alisema jirani huyo.

Alisema mazishi ya mtoto huyo yalifanyika jana mchana katika makaburi ya Ufi jijini.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow alisema awali, msichana huyo wa kazi alitoa taarifa za uongo kituo cha polisi cha Urafiki lakini walipombana walibaini ukweli wa tukio hilo.

Alisema awali, msichana huyo alidanganya kuwa aliporwa mtoto huyo na watu maeneo ya Manzese wakati akimpeleka hospitali baada ya mtoto huyo kuugua ghafla.

``Askari walitafakari kauli hiyo na kubaini kuwa ni ya uongo kwani mtu kupigwa na kuporwa mtoto mchana na watu wakishuhudia si rahisi. Hivyo walimbana na akasema ukweli kuwa hakuporwa mtoto huyo,`` alisema.

Alisema baada ya kumhoji zaidi, msichana huyo alibadili kauli na kusema kuwa mtoto huyo alifariki wakati akijaribu kumlisha chakula kwa nguvu na kwamba alimbana pua kwa muda mrefu.

Kamanda Rwambow alisema kuwa baada ya kumbana pua kwa muda mrefu mtoto huyo alifariki na ndipo alipokwenda kumtupa.

``Katika kutaka kupoteza ushahidi alimfunga katika mfuko na kwenda kumtupa,`` alisema kamanda Rwambow.

Hivi karibuni serikali ilipandisha mishahara kwa sekta binafsi, ambapo kwa watumishi wa ndani ulipanda na kufikia sh. 60,000 kwa mwezi.

Hata hivyo, serikali ilifafanua kuwa wale watakaolipwa sh. 60,000 ni wale wanaofanya kazi na kuondoka lakini wale wanaoshi na waajiri wao watakuwa wakilipwa sh. 20,000.

Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba mwajiri anashauriwa kumuongozea mfanyakazi wake mshahara zaidi ya huo uliopangwa na serikali.

SOURCE: Nipashe

Naona huyu mtoto ameishahukumiwa. Hivi haiwezekani ikawa anasema ukweli? Mara ngapi tumeona watoto wakilazimishwa kulipwa kwa kubanwa pua? Hivi madaktari na wataalam wengine hawawezi kutambua kama kifo hicho kilitokea wakati analishwa? Naona wameishamzika marehemu bila kufanya uchunguzi zaidi. Kuna haja ya kufanya uchunguzi zaidi na si huu wa kutegemea kibano!
 
Binti huyu anaihitaji msaada wa kisheria. Marehemu angeweza kufanyiwa Post Mortem ambayo ingebaini chanzo halisi cha kifo.
 
Habari hii inasikitisha sana hukumu aliyoibeba mtoto kwa makosa ya mzazi hakika itamrudia mtendaji (hausigeli) na mzazi wa mtoto. Mtoto roho yako ifike moja kwa moja kwa Mungu mwenyezi, amen.
 
its high time kuwe na certified nanies, walau wapitie kozi fulani ya basic child care na first aid. I believe mtoto huyo hakufa ghafla kwa kuchoke au aspiration ila alianza kuonyesha dalili za kupaliwa which means housegirl angekuwa na idea ya first aid angeweza kumsaidia kuondoka kwenye kupaliwa huko.
May the child's soul rest in perfect peace.
 
its high time kuwe na certified nanies, walau wapitie kozi fulani ya basic child care na first aid. I believe mtoto huyo hakufa ghafla kwa kuchoke au aspiration ila alianza kuonyesha dalili za kupaliwa which means housegirl angekuwa na idea ya first aid angeweza kumsaidia kuondoka kwenye kupaliwa huko.
May the child's soul rest in perfect peace.

Tatizo ni kuwa hausgeli keshaminywa na kupatikana na hatia ya kuua kwa kusudia. Maisha ya mtoto mwingine yanaangamia hivi hivi! Nakubaliana na wewe kuwa kozi ni muhimu na kama itashindikana hivyo kwa nini visirushwe angani vipindi ambavyo vitawafundisha namna ya kulea watoto? Mara nyingi katika jamii yetu tunakimbilia kumtafuta mchawi bila kufanya uchunguzi wa kina itakayoangalia kama kuna mitigating circumstances. Tujitahidi ili tuokoe maisha ya malaika hawa huko mbeleni.
 
mimi sikubaliani na hiyo heading ya gazeti ati housegirl kamnyonga mtoto baada ya kukosa mshahara! hawa wandishi sijui wanatupeleka wapi? jana wanaandika vingine leo vingine.
Fundi mchundo tushirikiane basi kuandaa hivyo vipindi vya kuelezea basic child care.
 
Bila shaka mtoto yuko kwa Mungu sasa. May the soul rest in peace. Hebu tuangalie upande mwingine wa shilingi, unaweza kuta ni kweli pia kwamba kwa hasira za kutolipwa mshahara huyo binti kaamua kumkomoa mwajiri wake considering the age (adolescent)aliona ndo suluhisho. Sitaki kumtetea wala kujustfy alichofanya but hii pia ni fundisho kwa waajiri coz hili swala la mahousegirl kutolipwa ni kawaida sana hapa mjini, wakati wanatafuta maid wanaahidi kulipa, then mazoea yanaanza ,mtu anakuwa halipwi kwa kigezo eti nakutunzia pesa then utachukua zote kwa pamoja. Siku ya kufukuzwa kama mbwa which is the way fo many only the lucky ones get even the transport fare, waajiri wanasahau kama mshahara alikuwa anatunza mshahara. Btw who doesnt know how to keep money? kama una roho safi si umfungulie account? hii inajenga chuki kwa hawa mabinti wanaona ni dhuluma na kwa kuwa wana shida wanavumilia ila hawapendi, when enough is enough hiyo ndo result. Hii ni changamoto kwetu wazazi na waajiri.
 
Hii habari kweli inaskitisha!

Hawa mahahousegirl saa ingine taabu tupu hakuna cha kumtetea acha sheria ichukue mkondo!

Nakumbuka kuna mmoja tulikuwa tunakaa nae, basi tukiwanchia mtoto na maziwa yeye hunywa maziwa na chakula cha mtoto! Basi afya ya mtoto ikaanza kuwa mbaya na yeye housegirl akawa ananawiri kila siku!

Hadi tulivyogundua tukamfukuza!
 
Mtoto kafa kwa mazingira ya kutatanisha, na akajaribu kuficha, kwa kusema uongo,
Baada ya kuua alipataje nguvu za kumviringisha kwenyemfuko wa rambo na kwenda kumtupa! kama hakuwa na nia hiyo au ku attempt before?
Sijui kwa nini hakukimbia baada ya kitendo hicho kama walivyo wengine?

Mungu amuweke mahala pema peponi.
 
mungu aulaze pema mwili wa marehemu.

ila hii habari ina mafundisho pande nyingi.

ni habari ambayo ikifanyia utafiti unaweza kuandika kitabu kikubwa cha kuonesha jinsi gani kila pande inavyohitaji kuangalia na kuangaliwa.
 
Hii habari kweli inaskitisha!

Hawa mahahousegirl saa ingine taabu tupu hakuna cha kumtetea acha sheria ichukue mkondo!

Nakumbuka kuna mmoja tulikuwa tunakaa nae, basi tukiwanchia mtoto na maziwa yeye hunywa maziwa na chakula cha mtoto! Basi afya ya mtoto ikaanza kuwa mbaya na yeye housegirl akawa ananawiri kila siku!

Hadi tulivyogundua tukamfukuza!

Lakini pia kuna waajiri ambao wanawatesa sana hawa watoto. Kisaikolojia ukimtesa mtu mnyonge na yeye hufika mahala anatafuta mnyonge wake. Bahati mbaya kwa hawa wasichana wa kazi wanyonge wao ni hao watoto wetu. Ninavyoona this is issue is more complicated kuliko jinsi polisi wanavyoliweka. Unatakiwa uchunguzi wa kina ila kujua hasa chanzo cha kifo cha mtoto maana inaniwia viugumu kuamini kwamba yule binti kweli alimua kudai mshahara wake kwa kumuua mtoto.

PS: Unaweza ukakuta kesi ya huyu binti ikaenda harakaharaka na akasweka ndani hivi karibuni wakati ile ya Dito ndiyo hivyo tena; tena hakuna hata mkubwa yeyote atakayeenda kutoa pole kwa wale wazazi!
 
tatizo ni pale kila mtu anapotaka kuwa na housegirl, yaani imekuwa kama fashion kuwa na "mtoto wa kazi" ilhali wengi wa "waajiri" uwezo wa kulipa mishahara hawana!!!. hii ni tragedy kubwa mno ktk pande zote husika, sisi kama wanajamii nadhani kila mtu kajifunza kitu flani kutoka hii story.

Hata huku USA, kuna watu wanaleta "watu wa kazi" toka bongo.......kisha huwafanyia visa, including kutowalipa mishahara, kuwafungia majumbani wasionane na watu wengine, hufanyishwa kazi hadi masaa 16 kwa siku na ushenzi mwingine mwingi tu ulokithiri. Wakidai mishahara yao hunyang'anywa pasipoti, na kuanza kutishiwa kurudishwa TZ mikono mitupu............yaani inasikitisha sana!!!!.
 
inatia huzuni sana lakini hii nichangamoto kubwa kwa wazazi wanaowanyanyasa hawa wasichana wandani.
mshahara nihaki yao lazima walipwe watunze wao wenyewe
siungi mkono alichofanya lakini iwe changamoto wanawake wengine huwa niwavivu hata kukaa nawatoto wao hivo kulazimika watoto wao kulelewa na housegirl.
unakuta mtoto anamjua nakumpenda zaidi housegirl kuliko mama mzazi.
lakini pia huyu msichana yawezekana aliminywa sana polisi hivo akalazimika kusema hata yale yasiyokweli ili asiendelee kuminywa
kwanza ikumbukwe kuwa msichana alikuwa chini ya miaka18 nanina amini kabisa alikuwa hana uzoefu wakutosha wakulea mtoto
kuna uwezekano mtoto alipaliwa nauji njia za hewa kweli zikaziba akafa lakini kutokana namaisha aliyokuwa anaishi kwamanyanyaso yakikatili kwakuogopa kipigo nakwaakili yake changa akaona suluhisho nikwenda kumtupa
wanasheria wamambo yakijamii walione hili siyo tu kwasababu mtoto amekufa nao waungane kumshutumu nakumhukumu huyu biti
mimi niko kinyume nahukumu hizo.
ninaamini wana JF wapo ambao niwanasheria hebu wasimame wamtetee huyu msichana.
ng`wananogu
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana.. wakati mwingine mazingira yanafanya mambo kuwa magumu.. na sidhani kama mtoto wa miaka hiyo 16 anaweza kuhukumiwa kwa kosa la kuua..
 
Naomba nipendekeze yafuatayo.
1. Binti wa miaka 16 bado ni mtoto na hajakomaa bado kimawazo kwa hiyo anatakiwa awe treated kama juvenile.
2. Kwa ninavyojua wanayotendewa maHausgeli, sitashangaa kama huyu binti pamoja na jukumu la kumlea mtoto alikuwa anaangalia usafi wa makazi, nguo za tajiri wake, kupika kwa ajili ya familia n.k. Huyu alikuwa anaenda kuchota maji, kwenda gengeni n.k. huyu alikuwa ndiye wa kwanza kuamka na wamwisho kwenda kulala. Hakuwa na likizo. Pamoja na haya huyu binti alitolewa kijijini, hatujui alikuwa na elimu gani. Hatujui alikuwa na uwezo gani wa kulea. Huyu nae alikuwa victim.
3. Inawezekana kabisa kuwa mtoto alikufa ghafla bila hata huyu hausgeli kuhusika. Kunakitu kinaitwa cot death(SIDS) na hakuna anayejua kwa nini kimetokea. Unadhani huyu mtoto angefanya nini? Amngoje mwenye mtoto amweleze? Nani atakayemwamini. Ndiyo maana alipanic na kujihami kwa uongo wa kijinga ambao inaelekea hakuupanga.
4. Inawezekana mtoto alifariki wakati mlezi akijaribu kumlisha kama alivyosema. wazazi na walezi wengi wana tabia ya kulazimisha mtoto kula na njia moja wapo ni hiyo ya kumbana pua hadi afungue mdomo. Baada ya kifo, mlezi alipanic.
5. Inawezekana mlezi alimuua huyu malaika kwa makusudi kabisa. Lakini hii vile vile itaonyesha immaturity ya hawa walezi wetu.

sasa bila kufanya uchunguzi wowote huyu mtoto atatupwa lupango ambako maisha yake yataharibika kwa njia yeyote. Hatakuwa na wakili wa kumtetea na jamii itamsahau maana ni expendable. Wako wengi alikotoka.

Mimi ningependekeza yafuatayo:
1. serikali iweke sheria za kulinda watoto ambapo wazazi watawajibika katika kuwawekea mazingira bora watoto wao.
2. Serikali ifanye mipango ya kuwasaidia single mothers na wengine wasio na uwezo. Njia moja ni kufanya kampeni ya kujenga vituo vya kulelea watoto ambavyo vitahudumiwa na watu waliopewa mafunzo ya ulezi. Wakina mama wenye kipato cha chini walipe hizo hela ambazo zingekuwa ni mshahara wa hausgeli bila kuangalia idadi ya watoto wake.
3. Pale ambapo haiwezekani kujenga shule. Baadhi ya akina mama wapewe mafunzo na wapewe leseni ya kuweza kuhudumia watoto wa jirani zake kwa malipo kidogo.
4. Serikali iimarishe idara ya ustawi wa jamii. hawa wapewe jukumu la kusimamia watoto WOTE na sio yatima peke yao. Idara ianze outreach program ambayo italenga hasa wale wakina mama wanaojiangaikia kimaisha au walioajiriwa kwa mishahara midogo.
5. Uwekwe utaratibu ambako statement kwa yeyote aliye chini ya miaka 16 haitakubalika bila kuwepo kwa wakili au mtu mzima ambaye mtoto ana imani naye.
6. Serikali pamoja na NGOs wafanye jitihada kuwaelimisha mahausgeli/bois na wengine kama hao kuhusu haki zao. Wapatiwe vilevile mahali wanapoweza kwenda wanapoona wanadhulumiwa haki zao.
Haya ni mawazo yangu ili roho ya malaika huyu isipotee bure.
 
JAMANI NAOMBA KUULIZA HILI SWALI KWA WANA JF MNISAIDIE!!! HAUSIGELI ALIYETAJAWA KWENYE HIZI HABARI MBILI ZA KWENYE GAZETI ALICHOFANYA NI MAKOSA? MAANA ALIKUWA ANADAI HAKI!! SOMA HABARI YOTE KABLA YA KUJIBU!!!

Hausigeli amnyonga mtoto wa bosi wake

2008-01-24 10:08:25
Na Joseph Mwendapole


Msichana anayefanya kazi za ndani maeneo ya Manzese, Dar es Salaam, Tabu Isaya (16), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kumuua mtoto wa mwajiri wake na kisha kuutupa mwili wake makaburini.

Sababu za Taabu kuchukua hatua ya kumuua mtoto huyo wa miezi minane inadaiwa kuwa ni hasira za kutolipwa mishahara ya miezi sita hadi sasa na mwajiri wake huyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi na kwamba mtuhumiwa huyo atafunguliwa mashtaka ya mauaji.

Jirani wa eneo alilokuwa akifanya kazi msichana huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema msichana huyo alikuwa akilalamika mara kwa mara kutolipwa mshahara kwa muda mrefu na mwajiri wake.

Alisema msichana huyo ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma na alikuwa akiishi na mwajiri wake maeneo hayo.

Alisema wakati wa tukio hilo, mama wa mtoto huyo, Bi. Asia Ali alikuwa katika biashara zake maeneo ya Ubungo.

``Mara kwa mara alilalamika kuwa halipwi mshahara na aliahidiwa kuwa mwezi Desemba mwaka jana angelipwa malimbikizo yake lakini baada ya kuona halipwi akawa anataka kurudi kwao Dodoma,`` alisema jirani huyo.

Alisema mazishi ya mtoto huyo yalifanyika jana mchana katika makaburi ya Ufi jijini.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow alisema awali, msichana huyo wa kazi alitoa taarifa za uongo kituo cha polisi cha Urafiki lakini walipombana walibaini ukweli wa tukio hilo.

Alisema awali, msichana huyo alidanganya kuwa aliporwa mtoto huyo na watu maeneo ya Manzese wakati akimpeleka hospitali baada ya mtoto huyo kuugua ghafla.

``Askari walitafakari kauli hiyo na kubaini kuwa ni ya uongo kwani mtu kupigwa na kuporwa mtoto mchana na watu wakishuhudia si rahisi. Hivyo walimbana na akasema ukweli kuwa hakuporwa mtoto huyo,`` alisema.

Alisema baada ya kumhoji zaidi, msichana huyo alibadili kauli na kusema kuwa mtoto huyo alifariki wakati akijaribu kumlisha chakula kwa nguvu na kwamba alimbana pua kwa muda mrefu.

Kamanda Rwambow alisema kuwa baada ya kumbana pua kwa muda mrefu mtoto huyo alifariki na ndipo alipokwenda kumtupa.

``Katika kutaka kupoteza ushahidi alimfunga katika mfuko na kwenda kumtupa,`` alisema kamanda Rwambow.

Hivi karibuni serikali ilipandisha mishahara kwa sekta binafsi, ambapo kwa watumishi wa ndani ulipanda na kufikia sh. 60,000 kwa mwezi.

Hata hivyo, serikali ilifafanua kuwa wale watakaolipwa sh. 60,000 ni wale wanaofanya kazi na kuondoka lakini wale wanaoshi na waajiri wao watakuwa wakilipwa sh. 20,000.

Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba mwajiri anashauriwa kumuongozea mfanyakazi wake mshahara zaidi ya huo uliopangwa na serikali.`Nilimsokomeza khanga mdomoni asinipigie kelele`

2008-01-25 08:34:43
Na Devota Kabuta


Msichana anayefanya kazi za ndani, Tabu Isaya (16) ambaye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga hadi kumuua mtoto wa mwajiri wake, alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sinza Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo ya awali.

Msichana huyo ambaye alifikishwa mbele ya hakimu, Hilda Lyatuu wa mahakama hiyo katika maelezo yake alidai kuwa, aliamua kumweka mtoto huyo kipande cha khanga mdomoni kwa lengo la kumnyamazisha asiendelee kulia ili aweze kufanya kazi zake haraka.

Alidai kuwa, siku hiyo, Jumatatu Jan 21, saa 4:00 asubuhi, mama wa mtoto aliondoka nyumbani kwenda kazini na kumwachia vyombo vingi sana pamoja na kazi za kufagia uwanja na kufua nguo za mtoto na za kwake.

Alidai kabla hajaanza kazi hizo mtoto huyo alianza kulia na ndipo akaamua amwekee mdomoni kipande cha khanga kisha akamziba mkono mmoja mdomo na mwingine puani kama kwa dakika mbili hivi kwa lengo la kumnyamazisha.

Alidai alipomziba mtoto huyo alianza kutupatupa mikono na miguu kisha akanyamaza.

Alidai kuwa, alipoona amenyamaza alimtoa kipande kile cha khanga mdomoni, lakini alishangaa kumwona hapumui na ndipo alipogundua kuwa amekufa.

Alidai alichukua gauni lake na kuuviringisha mwili wa mtoto huyo kisha akachukua mfuko na kumweka ndani ya mfuko na kumbeba mgongoni.

Alidai alitoka na kwenda mpaka makaburi ya Manzese na alipofika alimtupa mtoto huyo sehemu yenye takataka jirani na makaburi hayo.

Alidai kuwa, alipomtupa aliondoka na kwenda kwa bibi wa mtoto huyo ambaye walikuwa wakiishi naye jirani na kumwambia kuwa mtoto ameibiwa na vijana wawili waliokuwa na mwanamke mmoja.

Alidai bibi huyo alimwambia amsubiri hapo nyumbani ili akamwite mama yake kazini.

Alidai mama yake alipofika huku akilia kwa hasira alimrukia na kuchanachana nguo alizokuwa amevaa na baadaye walimpeleka polisi.

Alidai huko polisi alisema anamtambua kijana mmoja ambaye alimtaja kwa jina la Rajabu wanayeishi naye jirani akidai pamoja na mwenzake ndiye aliyeshiriki kumwiba mtoto huyo.

Msichana huyo alidai polisi walimfuata Rajabu lakini licha ya kupigwa sana alikataa kuwa hakumwiba mpaka polisi wakaamua kumwachia.

Alidai polisi walimgeukia na kumpiga sana pamoja na kumbamiza ukutani na chini na ndipo alipoamua kuwaambia ukweli ili wasije wakamuua.

Alidai aliwaeleza kuwa mtoto huyo amemuua na kwenda kumtupa makaburini Manzese kutokana na hasira kwani alikuwa akilia na alikuwa na kazi nyingi, akaamua afanye hivyo amalize kazi kabla ya sasa nane ili mama yake atakaporudi asigombezwe.

Alidai aliwapeleka polisi na gari mpaka kwenye makaburi hayo na kuwaonyesha maiti ya mtoto huyo ambayo ilikuwa imebadilika na kuwa nyeusi.

Msichana huyo alidai kuwa, hakumuua mtoto huyo kwa kunyimwa mshahara kwani alikuwa akipewa mshahara wake kama kawaida isipokuwa aliamua kusema hivyo kwa kuwa walikuwa wakimhoji hoji sana.

Alidai mwajiri wake alimtorosha kutoka kwa wazazi wake mkoani Dodoma ili aje kufanya kazi kwake jijini Dar es Salaam kwa mshahara wa Sh. 20,000 kwa mwezi.

Alidai alimtorosha kwa kuwa baba yake alikuwa akitaka kumuoza kwa Mmasai wakati umri wake ulikuwa mdogo.

Alidai hapo nyumbani walikuwa wakiishi na mama huyo pamoja na mtoto aliyemuua lakini baba wa mtoto huyo alikuwa akija kulala mara moja moja.

Alidai mwajiri wake ana watoto wengine wawili ambao wanaishi Dodoma wilaya ya Kondoa.

Wakati huo huo, Joseph Mwendapole anaripoti kwamba Mama wa mtoto aliyeuawa kwa kunyongwa hadi kufa na msichana wa kazi za ndani, Asia Ali (28), amekiri kuwa hakuwahi kumlipa mshahara mfanyakazi wake tangu amchukue kutoka nyumbani kwao Dodoma.

Mtoto aliyeuawa ni Renaida Sebo aliyekuwa na umri wa miezi minane.

Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake Manzese Penisula, Bi. Asia alisema alimchukua msichana huyo mwaka jana kutoka kwa mama yake mzazi lakini hakukuwa na makubaliano ya kumlipa mshahara.

``Mama yake aliniruhusu kuja naye Dar es Salaam lakini hatukuzungumza kuwa nitakuwa namlipa mshahara, sasa nashangaa kama anasema sikumlipa mshahara kwa kuwa hatukukubaliana hivyo,`` alisema.

Alisema tangu waanze kuishi pamoja wamekuwa wakiishi maisha ya furaha na mtuhumiwa huyo hakuwahi kuonyesha chuki kwake wala kwa mtoto.

Alieleza kuwa siku ya tukio hilo juzi yeye alikuwa katika biashara zake Ubungo na ndipo alipojulishwa na ndugu zake kuwa mtoto wake ameibiwa.

``Baada ya kufanya unyama wake akaja kusema kuwa kaibiwa mtoto na majirani na ndugu wakaenda hiyo sehemu aliyoporwa lakini baadae iligundulika kuwa ni uongo,`` alisema.
 
Naungana mkono na fundi mchundo hapo juu....jamani kitendo cha binti huyu kuua ni kitu kikubwa ila sasa...kwanini kimetokea.Inawezekana kabisa hakukusudia ila woga wa kifo kama binadamu yoyote huweweseka.....anachanganyikiwa ndicho kilichotokea kwa binti huyu mdogo ambaye hata darasa la saba sijui kama alimaliza.

Tuje kwa waajiri hawa jamani haya mtatizo ya house girls kuiba,kuua,kutoroka kwa asilimia 75 yanachangiwa na waajiri wenyewe...yaani ni kama fashion kutesa msichana wa kazi..ili uonekane kwa wenzio ni mkali na una msimama hii si sawa...mie naamini binadamu anapofikia wakati hata njia ya kufanya huwa anafanya maamuzi magumu sana...ambayo sio rahisi kuyaelewa kirahisi...mie nilikuwa na tatizo hilo la kula mpaka miaka mitatu nililishwa kwa kukabwa pua na mpaka nimekula..ila sasa mama ananikaba house akifanya vila mama anafanya ili niweze kula wakati mama hayupo ni kosa la kufukuzisha kazi mara moja..

Unaweza kuona tatizo hapo.....pole kwa binti na pole kwa familia iliyo fiwa ila ndio changamoto kwa wazazi wote wanyama wanao watenda wafanyakazi wao kama wanyama.
 
fundi mchundo mawazo mazuri hayo, ila kwa mazingira ya bongo kweli yanaimplentika?
nampa sana binti huyo pole kwa maswahiba hayo.
My observation ni kuwa yawezekana binti huyo na full of stress. Unajua bongo housegirl huyo mmoja anafua, anadeki, anaangalia mtoto, amuogeshe, amlishe, achote maji,awashe mkaa huku mtoto ndani analilia uji, huku rundo la nguo limejaa kufulia na baadae kupasi. Wanaface terrible situation na wanakuwa stressed kiasi cha kuweza kufanya chochote.
sijui sheria itaamua nini kwa mazingira kama haya.
 
Let us first analyse the age of the housegirl, she is 16, the action she took to silence the child was irrational, that should show the police that she is still an underaged child whose thinking capacity has not yet developed that much.

Our police as usual always use excessive force to obtain a confession which is inadmissible in the court of law. Banging a person against the wall is something beyond cruelty considerimng she is just 16.

Why would the employer/family friend take the child and subject her to slavery, she could have sound another person to do the cleaning and the minding of the child then.

The housegirl's reaction clearly shows how confused she was. One cannot just commit murder and expect people to buy your story just like that.

The housegirl needs a very good lawyer but as she is one of the unfortunate few she will be thrown in prison and the key thrown in the sea....had she been Dito.......
 
Mkuu Kinyau! Inawezekana tukiweka priorities zetu vyema.
Inabidi jamii iwe creative. Tukubali kuwa ule wakati ambapo kijiji kizima ndiyo kinalea mwana haupo tena. Ukweli ni kwamba tunaelekea kwa wenzetu wa magharibi, kila mtu kivyake vyake. Tukubali kuwa watoto wetu wanazaa katika umri mdogo mno na mara nyingi uwezo wa kuwatunza hao watoto hawana. Tukubali kuwa si watoto wote wanaolelewa katika familia za kiasili yani zenye baba na mama. Mara nyingi ni wakina mama au hata bibi zao ambao wanaachiwa mzigo huu. Na ili kumudu huu wajibu, inabidi wabangaize kwa kila hali. Katika yote haya tuwape watoto wetu kipaumbele wanachostahili. Serikali pamoja na serikali za mitaa inabidi ziwajibike kwenye hili. Nitatoa mifano.
a) Ninapozungumzia nursery si lazima iwe kama za ulaya. Panapohitajika ni sehemu salama ambapo watoto wanaweza kuhifadhiwa wakati wazazi wao wakihangaika. Chumba kimoja chenye ua kinatosha kabisa. Tunaweza hata kuanza na container ambayo itawekwa karibu na sehemu yenye vyoo au hata kuwekewa vyoo ndani yake kwa gharama nafuu. Tumejaliwa hali ya hewa ambayo kwa kipindi kikubwa watoto wanaweza kucheza nje.
b)Hawa wakina mama na wakina baba wakiwa organised wanaweza kupokezana siku za kusimamia hao watoto. Au wanaweza kwa kuchanga kile ambacho wangemlipa mfanyakazi wa ndani, wakamlipa mmoja wao afanye hii kazi. Wakina mama katika vitongoji vingi wameanzisha vyama vya kusaidiana kwenye harusi na misiba. Kwa nini hivi vyama visitumike kwenye hili?
c) Hapo zamani tulikuwa na wakina mama maendeleo kila mahali. Kwa nini hawa wasifufuliwe na waongezewe jukumu la kuhakikisha kuwa wazazi wanaelewa majukumu yao na kuyatekeleza?
d) Si vigumu kuanzisha vipindi kwenye redio na televisheni vitakavyolenga kwenye haki ya wakina mama na watoto wao.
e) Hawa hawa wakina mama maendeleo wanaweza kusaidia sana kuhakikisha kuwa hawa ma hausgeli/boi wanatendewa haki. Mama wa marehemu anadai kuwa kwa vile hawakukubaliana mshahara na hausgeli wake hakuona sababu ya kumlipa.
f) Serikali ikishirikiana na viongozi wa dini, wa jamii iwafungie kazi wale wote wanaozaa na mabinti zetu na kukwepa kutimiza majukumu yao. Kwenye utata kuhusu uzazi kuna DNA! Si wote wanaokwepa hawana uwezo. Wengi wana madaraka ya juu kabisa lakini kwa kiburi tu wakijua hakuna kitakachowapata hawaoni tatizo kuwaruka wazazi wenzao. Au kwa kutumia kutoelewa kwao, kuwahonga vihela mbuzi ili warudi kijijini kwao.
g) Huu ni wakati muafaka wa kuangalia kwa kina utendaji wa jeshi letu la polisi. Matumizi ya torture yanabidi yapigwe marufuku. Wawajibike kufanya uchunguzi unaoeleweka katika kila tukio. Mimi nimeishaingiliwa na wezi na polisi walipokuja wala hawakujisumbua kuchukua angalau 'fingerprints'! Wao wanakimbilia kwenye kula kwa kunihakikishia kuwa nikiwakatia kitu watawatia vibano wale ambao wanahisi au ambao mimi ninahisi wanahusika hadi watakapo'confess! Hii si haki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom