Wafanyakazi tunasema: Hatudanganyikiii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi tunasema: Hatudanganyikiii

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tonge, Aug 17, 2010.

 1. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JUZI SERIKALI IMETANGAZA KUONGEZEKA KWA KIMA CHA CHINI NA WARAKA UANONYESHA KUWA KIMA CHINI KIMETOKA KUTOKA TSH 135,000/= ALICHOTANGAZA JK SIKU ANAVYUNJA BUNGE HADI TSH 260,000/= AMBACHO NDICHO KILICHOPO KWENYE WARAKA MPYA WA WATUMISHI WA SERIKALI.

  KWA MAONI YANGU.

  1.) JK NA SERIKALI WAMETUDANGANYA KUHUSU KIMA CHA CHINI CHA AWALI HADI CHA SASA LAKINI BADO HAWAJAFIKIA KILE CHA TUCTA.
  2.) SERIKALI IMEAMUA KUTANGAZA HILO ONGEZEKO BAADA YA KUONA SERA MOJA WAPO YA CHADEMA KUWA NI KUREKEBISHA MASLAHI NA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI KWANI SERIKALI INA UWEZO HUO.
  3.) SERIKALI ILIKUWA INAJUA KUWA WANAO UWEZO WA KUTULIPA KIASI HICHO CHA KIMA CHA CHINI ILA WALITAKA KUZIFISADI HIZO HELA NA WAKATOA VISINGIZIO KIBAO KAMA ALIVYOVITOA JK SIKU YA MKUTANO NA MAKADA WA CCM WA DAR.
  4.) SERIKALI YA CCM ISHITAKIWE KWANI MUDA WOTE TUANAOMBA KUPANDISHIWA MSHAHARA HAWATAKI, SASA KAMPENI ZA UCHAGUZI ZINAKARIBIA NDIO WANAPANDISHA MSHAHARA, HII MIMI NAIITA RUSHWA WAKATI WA UCHAGUZI.:frusty:


  WAFANYAKAZI TUNASEMA "KUWA WAMETUNYANYASA SANA, WAMETUTESA SANA, WAMETUDHARAU SANA, WAMETUONEA SANA NA WAMEFISADI MALI ZA NCHI SANA BASI SISI TUNASEMA HATUDANGANYIKI NA ONGEZEKO LA MSHAHARA, TUTAMPA KURA MGOMBEA ANAYETUJALI NA ATAKAE TETEA MASLAHI YETU IKIWEMO MISHAHARA, NAYE NI DR SLAA.

  MUNGU KIBARIKI CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
  :amen:
   
 2. A

  Ashangedere Senior Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said mdau serikali ya tanzania chini ya CCM inastahili kabisa kushitakiwa hili ni kosa la jinai
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahakama bora kwa sasa kuanzia ni ile ya kura; hamasisha wafanyakazi mbu mbu mbu nao waelewe hivyo kuwa serikali uwezo inao ila huwa haiwatakii mema wafanyakazi; full sop; uchaguzi ukiisha na wakatolewa then washitakiwe kwa u haini na ufisadi
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,275
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama unataka kujua umafia wa CCM ndio huu, JK alisema hawezi kuongeza mishahara kwa vile serikali haina pesa alisema hata wafanyakazi wagome kwa miaka minane hawezi, hizi hela zimetoka kwenye fungu gani wakati bajeti ilishasomwa.

  Nakumbuka kuna mwaka tuliahidiwa nyongeza ya mishahara na waraka ukapitishwa ajabu hadi miezi tisa ikapita mshahara wangu ulikuwa haujabadilika, sasa hii sijui tutapewa mwezi wa uchaguzi tu halafu tuambiwe pesa imeisha.

  Wametufanya sisi watoto wao wa kudanganyiwa peremende tunawaambia walete hiyo mishahara ni haki yetu lakini................ mwaka huu hatudanganyiki.
   
Loading...