issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,788
- 5,217
Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria, walishangaza kwani walipohitimisha maandamano katika uwanja huo, walianza kutoka nje badala ya kukaa na kusubiri hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi na mgeni rasmi, ambaye alikuwa ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Badala ya kukaa na kusikiliza hotuba hizo, msururu wa baadhi ya wafanyakazi hao ulianza kutoka nje, hivyo kuwalazimu askari kuanza kuwazuia kwa kufunga geti walilokuwa wanalitumia kutoka.
Askari hao walifunga geti hilo na kurudi ndani kwa ajili ya kuimarisha ulinzi, huku wakiwaacha wafanyakazi hao wamesimama getini.
Hata hivyo, juhudi hizo hazikuzaa matunda baada ya wananchi kufanikiwa kufungua geti hilo kwa kuondoa chuma kilichokuwa kimetumika kulifunga na kuanza kusukumana kwenda nje kabla askari hajawazuia tena.
Baadhi ya wafanyakazi hao walisikika wakisema hawataki kusikia hotuba, hivyo ni bora wawahi usafiri wakaendelee na shughuli zingine.
Wakati hayo yakiendelea, baadhi yao walikuwa wametoka wakiwa wanarandaranda nje na wengine wakiwa wanasubiri usafiri kuondoka kana kwamba sherehe zimemalizika. Wakati hayo yakiendelea, Makonda alikuwa anaendelea kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa ndani, ingawa uwanja ulionekana kupwaya.
Hata hivyo, katikati ya hotuba yake, Makonda alionyesha kutoridhishwa na kile kilichokuwa kinaendelea getini.
Wakati huu mimi nazungumza hapa, kuna watu wanahangaika na geti kutaka kutoka badala ya kusikiliza ninayozungumza. Haya ndiyo yanayotokea hata ofisini, kuna watu badala ya kukaa na kufanya kazi wanatoroka halafu wanataka mshahara uongezeke,” alisema Makonda.
Katika hotuba hiyo, Makonda alitumia muda mwingi kuwaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli za kupambana na rushwa kwa kuhakikisha wanaweka nguvu zao kumwombea.
“Ni vyema wananchi wakatambua kuwa mapambano ya rushwa hayamsaidii mtu mmoja. Kwa bahati mbaya jitihada hizi zinazofanywa na Rais zimeanza kumletea maadui, hivyo kuna haja ya kila mwananchi kumwombea,” alisema.
Chanzo: IPP Media