Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Serikali ilipoanzisha mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya, tumeshuhudia baadhi ya watu hata waliopo Serikalini wakigeuka kuwa maadui. Yesterday nimeweka mada hapa nikieleza kusikitishwa kwangu kwa jinsi vita ya Madawa ya Kulevya ilivyomharibu Nape Nnauye mpaka akafikia hatua ya kuasi mwajiri wake. Tumeshuhudia pia viongozi wa Serikali wakizushiwa kashfa mbalimbali kisa tu kuwa frontline katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
Sasa limekuja hili la majangili wanaoliibia taifa letu kwenye sekta ya madini. Nakumbuka shauku kubwa ya Watanzania kumtaka Rais azame huko kwenye madini ambako ndiko mapato mengi yanapotea. Watanzania wazalendo walimsihi Rais kutoangalia sura ya mtu katika kulinda Raslimali za Taifa.
Hata hivyo, kwa sasa naanza kuona dalili za watu kugeuza mapambano dhidi ya wahujumu uchumi kupitia madini kama vita ya mihadarati. Wamejipanga kuhakikisha Serikali haifanikiwi katika hili kwa vile wanajua dhahiri kuwa kufanikiwa kwa Serikali ni anguko la Wapinzani.
Kwa upande mwingine, waathirika wa mapambano hayo wakiwemo ACCACIA na GGM, wameanza pilika za kupata watetezi kupitia majukwaa ya siasa na mitandao ya kijamii. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba wameshachelewa. Rais amechukua hatua stahiki kwa wakati muafaka.
CCM ya Magufuli hata mchanga utapanda thamani