Wafanyabiashara wote Moshi wamegoma

Wafanyabiashara wote Moshi wamegoma

Hili sakata sijui watalimaliza lini, marudio kila kukicha.
 
hawa wafanyabiashara watumie hizo mashine...wafanyakazi walipokuwa wanalalamikia PAYE wao walikuwa wanaona kama wafanyakazi wanakwepa kodi...sasa watambue kuwa EFD ndo PAYE yenyewe...wasikwepe walipe kodi...serikali inaendeshwa kwa kodi, kuweni wazalendo nyie wafanyabiashara.
 
Serikali hii imezidi ulegevu.Hawa watu wanatakiwa kutandikwa viboko na si kuwalealea kijinga.Hawana hoja ya mşingi na wamezoea kukwepo kodi huku wakituumiza walajı kwa bei kubwa za bidhaa na huduma zao.Nchi wafanyabiashara wengi wanakwepa kulipa kodi stahiki na sasa inaonekana kuzoeleka na kujiona hawapaswi.Wafanyakazi wanabanwa kodi na wananchi tunauziwa bıdhaa na huduma kwa bei kubwa ikıamınika kuwa sehemu itakuwa kodi.Hawa jamaa ni wahunı na majambazi sawa na mafisadi wa kısıasa, tusiwaunge mkono kabisa.

Wambie kwanza wakusanye kodi kwenye madini,kwenye makampuni ya simu,afu waje kudili na hawa wenye mitaji midogo,Mara ngapi umesikia serikali yako imesamehee kodi kwa wawezekaji mabilioni ya hela,afu inakuja kikimbizana na wenye mitaji midogo midogo milioni 3,4mpaka5.majuzimajuzi Sukari ilikuwa ikiingizwa nchini na wafanyabiashara 3 tu,serikali ikawaruhusu wasilipe ushuru,na kusababisha Sukari yetu kutouzika,serikali dhaifu ni ile inayoshindwa kukusanya kodi kwa matajiri,makampuni makubwa,na kikimbizana na wamachinga.nikuulize kwenye escrow zile bilioni zote walizogawana walikuwa wamelipia kodi,Najua ni mda tu,hata wewe utajitambua na kuamka
 
Mkuu bora ungekaa kimya.
Mashine hizi zinatumika dunia nzima, sio Tanzania tu.

Hujui Kitu wewe,nenda kenya hapo,ama Uganda wale wanaotumia machine hizo ni wale wenye mitaji mikubwa mikubwa tu,wanoingiza bidhaa toka nje,viwanda ,makampuni,nk.hapa kwetu wanataka hata Yule anayenunua mizigo humu humu nchini,awe na machine,wenye mitaji ya milioni 5,6,mpaka 7 wawe na machine.Nimbie ni ofisi ipi ya serikali ulienda kulipia chochote ukapewa listi ya machine.amka wewe
 
hawa wafanyabiashara watumie hizo mashine...wafanyakazi walipokuwa wanalalamikia PAYE wao walikuwa wanaona kama wafanyakazi wanakwepa kodi...sasa watambue kuwa EFD ndo PAYE yenyewe...wasikwepe walipe kodi...serikali inaendeshwa kwa kodi, kuweni wazalendo nyie wafanyabiashara.

Mkuu kodi mbona watu wanalipa,sema hatujui zinakokwenda sijui uswisi.machine hizo zinajua mauzo tu.hazijui matumizi hiyo ni changamoto kubwa sana
 
Serikali katika hili ijaribu kuwa serious maana hawa wafanyabiashara wakwepaji wazuri wa kodi huku wafanyakazi wanaumizwa. Kwakweli katika HILI, Tafadhali Mwigulu nyooka na hao wakwepa kodi perpendicular maana hatuwezi kujenga nchi kwa mtindo wa kijinga kukwepa kodi kiasi HILI.

Usilolijua .........
 
Siamini wachaga wanaweza goma wanavyopenda hela... tujuze Mushi..sa, yule mchaga pale karibu na posta kafunga kweli!
 
Hata hapa pande za Mwenge naona Misukule imefunga maduka. Nami leo nalingia mauzo make toka nianze biashara mwaka unusu sijawahi kuuza kama hizi siku wafanyabiashara wanazogoma(ga).

Watu wengine ujinga na elimu ndogo ndo vinawatesa. We mtu una kiduka hata mtaji wa m1 hakina. Unasikia ma-papa wa biashara wamegoma eti nawe unawasindikiza kwenye migomo yao! Ujinga mzigo. Mtu huna hata hakiba ya chakula cha wiki unagoma?

Mbaya zaidi kuna wauza magenge eti nao wamegoma kisa ni ukawa... hahahahaha... sa nikabaki najiuliza kwan mgomo wa wafanyabiashara una uhusiano gani na wanasiasa... jirani yangu akanijibu eti waliokua wakihamasisha mgomo ni akina mangi ndio maana baadhi ya watu wakautafsiri kuwa na mlengo wa kisiasa. Tehteh, ujinga mzigo.

Nipo na jirani yangu hapa mwenge tunapiga mzigo kam kawa. Naomba sana miujiza itokee wagome mwezi mzima labda nami naweza kufanya jambo la maana.

Kufanya kazi Clouds inabidi utetee kila kitu cha sisiemu na kujilimbikiza vyeo kibao... Kuna wakati ulijibatiza ni mfanyakazi wa taasisi flani ya serikali humu, leo umejibatiza mfanyabiashara wa Mwenge. Hongera sana..
 
Ndg Minja Rais wa wafanya biashara Tanzania amefutiwa dhamana na kupelekwa mahabusu. Hivyo MGOMO WA KUTOFUNGUA MADUKA UTAENDELEA hadi hapo atakapo achiwa huru.
 
Kufanya kazi Clouds inabidi utetee kila kitu cha sisiemu na kujilimbikiza vyeo kibao... Kuna wakati ulijibatiza ni mfanyakazi wa taasisi flani ya serikali humu, leo umejibatiza mfanyabiashara wa Mwenge. Hongera sana..

Una machine lakini ama unabwabwaja tu
 
Kufanya kazi Clouds inabidi utetee kila kitu cha sisiemu na kujilimbikiza vyeo kibao... Kuna wakati ulijibatiza ni mfanyakazi wa taasisi flani ya serikali humu, leo umejibatiza mfanyabiashara wa Mwenge. Hongera sana..

Ushanunua machine ya EFD ama unabwabwaja tu, wewe mwenye elimu hujui wenye elimu ndio waliotufikisha hapa,
 
*********************************
asante kwa kunifumbua macho, nilikuwa najiuliza hili swali ni kwa nn hapa bongo fremu haishikiki....naenda pale masika frem ya kawaida tu ndogo naambiwa laki tano kwa mwezi na wanataka ya mwaka amllbayo ni 6m....nikajiuliza nn nitakachouza kwenye hiki kifremu nipate hiyo hela irudi, jumlisha kodi tra, jumlisha mtaji wa bidhaa, jumlisha gharama za uendeshaji....ikabidi niwe mdogoooo

Hayo hayo unayojiuliza ndiyo yanayosababisha watu wanagoma ,wafanyabiashara wanatofautiana kuna Mzee Azam,Mengi,na wengine wakubwa wakubwa,hao machine kwao si issue.sasa mtu Ana mtaji wa sh milioni Sita unamwambia anunue machine,wapi na wapi.
 
hahaha umejuaje mimi nina elimu?? Post yangu wapi nimeandika neno elimu??

Samahani nilitaka kumjibu mwingine aliyesema wafanyabiashara elimu ndio inawasumbua ,wakati wenye elimu kibao wameajiriwa na wasio na elimu.samahani tena mkuu
 
Atiiiii wachaga Moshi wamegoma mmnh ndio nasikia Leo hii

wachaga moshi wagome KUFANYA BIASHARA? Wakigoma najiondoa jamii forums naapa.Migomo ya kufunga biashara ni kwa ajili ya vikabila visivyojitambua vya mikoa mingine visivyojua maana ya biashara ni nini.Moshi wagome chezea wachaga wewe huwajui.

Ulishawahi sikia hata maandamano ya fujo moshi? Hawataki kuharibu biashara maandamano yote ya fujo ni kwa makabila mengine.Mwanza kwa wasukuma,dar kwa wazaramo,Arusha kwa wamasai na wameru,KIGOMA kwa waha,mbeya kwa wanyakyusa,Iringa kwa wahehe n.k sio moshi.

Ni kweli maduka hapa moshi yamefungwa toka jana,na leo ni siku ya pili.Hakuna dalili za maduka hayo kufunguliwa
 
Hujui Kitu wewe,nenda kenya hapo,ama Uganda wale wanaotumia machine hizo ni wale wenye mitaji mikubwa mikubwa tu,wanoingiza bidhaa toka nje,viwanda ,makampuni,nk.hapa kwetu wanataka hata Yule anayenunua mizigo humu humu nchini,awe na machine,wenye mitaji ya milioni 5,6,mpaka 7 wawe na machine.Nimbie ni ofisi ipi ya serikali ulienda kulipia chochote ukapewa listi ya machine.amka wewe

Nini tatizo la hızo mashine?Zitakuongezea kodi unayotakiwa kulipa, ama zinaenda kukomesha uongo mnaofanya kukwepa kodi?Eti gharama kubwa, wale ambao walistahili kulalamika ukubwa wa gharama sio walio ki-mbelembele kugoma.Mashne zenyewe zinawasaidia ninyi pia tena sana msiibiwe na hao wafanyakazi wenu, lakn pia kuwa na kumbukumbu nzuri za biashara zenu.Mnapewa bure alafu mnalalamika???Mngekuwa mnauziwa???Hela mnayonunulıa sı mnarudishiwa?
 
Back
Top Bottom