Wafanyabiashara wote Moshi wamegoma

Wafanyabiashara wote Moshi wamegoma

mimi nashauri serikali wamfunge huyu jamaa tuone kama watafunga biashara kila siku.

kwa sababu kichwan ni box huelewi endelea kuongea tu. kwa taarifa tu maduka yakifungwa cku moja serikali inapata hasara ya billion Mia Tatu kwa mujibu wa wazir wako wa fedha ndugu malima
 
Wafanyabiashara Wapo sahihi sana ,sio wakwepa kodi ni walipa kodi wazuri tu na ndio maana unaona Serikali ipo.Swali dogo kwako ni hili "kodi ya Serikali inatozwa katika mauzo au faida?.

Nimekuuliza swali hili kwa sababu inawezekana kabisa haujielewi na umejiandikia tu kwa utashi wako

Mkuu haturumbani.Kodi nı za aina nyıngi lakıni tuzingatie hizi 2 ;VAT na kodi ya mapato.VAT ınatozwa kwa % kulingana na mauzo yaliyofanyika.Kodi ya mapato inatozwa kwenye faida kama vitabu vya mahesabu vpo.Nııshıe hapo kwanza.Kwenye VAT mfanya aliyesajaliwa kwa VAT ni kama wakala lakn mara nyingi sana wanafanya ujanja na hawaoneshı mauzo halisı aliyofanya na kwa hli wanatuibıa sısı walajı ambao kımsıngı ndıo tunaolipia hyo VAT.Na kuhusu kodı ya mapato,bila na takwımu halısı za mauzo na gharama za uendeshajı kadhali mtaji uliowekeza,faıda ınayotakıwa kukatwa kodi haıtajulıkana na hıı ınawafanya wakadirıwe kwa kuwahonga maafisa wa kodı ılı wawakadrıe kodı ndogo.EFD ıtasaıdia kwa kıas flanı.
 
nilishasema hawa CCM ni janga la kitaifa. hizi mashine litakua dili la wapiga pesa pale lumumba
 
Serikali hii imezidi ulegevu.Hawa watu wanatakiwa kutandikwa viboko na si kuwalealea kijinga.Hawana hoja ya mşingi na wamezoea kukwepo kodi huku wakituumiza walajı kwa bei kubwa za bidhaa na huduma zao.Nchi wafanyabiashara wengi wanakwepa kulipa kodi stahiki na sasa inaonekana kuzoeleka na kujiona hawapaswi.Wafanyakazi wanabanwa kodi na wananchi tunauziwa bıdhaa na huduma kwa bei kubwa ikıamınika kuwa sehemu itakuwa kodi.Hawa jamaa ni wahunı na majambazi sawa na mafisadi wa kısıasa, tusiwaunge mkono kabisa.

You are very naïve. Uko sahihi kwa upande mmoja japo umekosa ufahamu wa tatizo la msingi na matatizo mengine yaliyojitokeza mwaka huu kwenye mfumo wa kodi za nchi hii.
 
Wakuu ule Mwendelezo wa Wafanyabiashara Nchini kugomea Mashine za utoaji risiti EFD,Leo Unafanyika katika Mji wa Moshi.Pia wanataka Kesi iliyofunguliwa dhidi ya Mwenyekiti wao Taifa ifutwe.

Tokea Asubuhi Maduka hayajafunguliwa Mpaka Muda Huu Tofauti na siku Nyingine.

Kuna Taarifa Za Mikoa Mingine nako Wafanyabiashara wamegoma.

Duh, wasije tu wakaandamana kwenda kwa Lowassa.
 
Mkuu haturumbani.Kodi nı za aina nyıngi lakıni tuzingatie hizi 2 ;VAT na kodi ya mapato.VAT ınatozwa kwa % kulingana na mauzo yaliyofanyika.Kodi ya mapato inatozwa kwenye faida kama vitabu vya mahesabu vpo.Nııshıe hapo kwanza.Kwenye VAT mfanya aliyesajaliwa kwa VAT ni kama wakala lakn mara nyingi sana wanafanya ujanja na hawaoneshı mauzo halisı aliyofanya na kwa hli wanatuibıa sısı walajı ambao kımsıngı ndıo tunaolipia hyo VAT.Na kuhusu kodı ya mapato,bila na takwımu halısı za mauzo na gharama za uendeshajı kadhali mtaji uliowekeza,faıda ınayotakıwa kukatwa kodi haıtajulıkana na hıı ınawafanya wakadirıwe kwa kuwahonga maafisa wa kodı ılı wawakadrıe kodı ndogo.EFD ıtasaıdia kwa kıas flanı.

Umewahi kufanya biashara?au unasoma kwenye vitabu tu?ni rahisi sana kuongea unavyoongea kama hujafanya biashara za Kitanzania.

Hakuna mfanyabiashara wa mtaani anayekusanya kodi kwa ajili ya nyongeza kwa TRA, ukifanya hivyo utafilisika maana huwezi kumuuzia mteja kwa bei ya hivyo.

Vitu vyote unavyonunua maduka ya kawaida haya umeuziwa kwa bei isiyo ya nyongeza ya 18% ya VAT, umeauzia bei ya kawaida ili muradi apate faida.Akiuza kwa bei ya nyongeza ya VAT kwa hatauza.Hivyo usijidanganye hapo kuwa hiyo VAT kalipa mteja, hapana.Wateja wa Tanzania bado hawajaanza kulipa VAT, ni mfanyabiashara anajikata kulipa VAT.Ndio maana kucompansate hilo lazima acheze kidogo na risiti, vinginevyo atafilisika mapema sana.Hujawahi fika kwenye duka unanunua mzigo wa pesa ndefu alafu anayekuuzia anakwambia kama unahitaji niandike pesa kamili kwenye risiti basi timua zako, sikuuzii?ndio ujue kuwa VAT kwa Tanzania bado mteja hajaanza kulipa.

Hivyo kinachotokea ni mfanyabiashara anapunguza faia yake ndio anayoitoa TRA kama VAT.Ngoja usitoijua usiicheze.

Na kingine, nani kakwambia TRA wanafanya mahesabu ya VAT kupitia vitabu?hiyo ipo kwenye karatasi huko, in reality makadirio bado yanaendelea huko site, wakisoma mahesabu wakaona "wanavyofikiri wao tu" wanakadiria.So kuna mambo mengi kwenye haya.Wafanyabiashara wanajua zaidi.
 
Wakuu ule Mwendelezo wa Wafanyabiashara Nchini kugomea Mashine za utoaji risiti EFD,Leo Unafanyika katika Mji wa Moshi.Pia wanataka Kesi iliyofunguliwa dhidi ya Mwenyekiti wao Taifa ifutwe.

Tokea Asubuhi Maduka hayajafunguliwa Mpaka Muda Huu Tofauti na siku Nyingine.

Kuna Taarifa Za Mikoa Mingine nako Wafanyabiashara wamegoma.

Wafanyabiashara hawagomei mashine za EFD tu bali hata kiwango cha kodi mtu alicholipa mwaka jana kimeongezwa kwa asilimia 100.

Hakuna anayejua kigezo kilichotumika kupandisha kodi kiasi hicho!
 
Wafanyabiashara hawagomei mashine za EFD tu bali hata kiwango cha kodi mtu alicholipa mwaka jana kimeongezwa kwa asilimia 100.

Hakuna anayejua kigezo kilichotumika kupandisha kodi kiasi hicho!

Mkuu hapo umenena Hakuna biashara inayo kua marambili kwa mwaka wanatumia vigezo gani kufanya mambo hayo
 
Mkuu hapo umenena Hakuna biashara inayo kua marambili kwa mwaka wanatumia vigezo gani kufanya mambo hayo

Ndiyo shida ya watu kukaa maofisini na kufanya maamuzi bila kuelewa hali halisi!
 
kwa sababu kichwan ni box huelewi endelea kuongea tu. kwa taarifa tu maduka yakifungwa cku moja serikali inapata hasara ya billion Mia Tatu kwa mujibu wa wazir wako wa fedha ndugu malima
Pia analiona hili suala la EFD kama la wafanyabiashara lakini hajui kuwa yeye pia anaumia!

Serikali hii imezidi ulegevu.Hawa watu wanatakiwa kutandikwa viboko na si kuwalealea kijinga.Hawana hoja ya mşingi na wamezoea kukwepo kodi huku wakituumiza walajı kwa bei kubwa za bidhaa na huduma zao.Nchi wafanyabiashara wengi wanakwepa kulipa kodi stahiki na sasa inaonekana kuzoeleka na kujiona hawapaswi.Wafanyakazi wanabanwa kodi na wananchi tunauziwa bıdhaa na huduma kwa bei kubwa ikıamınika kuwa sehemu itakuwa kodi.Hawa jamaa ni wahunı na majambazi sawa na mafisadi wa kısıasa, tusiwaunge mkono kabisa.

hatupaswi kutumia nguvu kuwalazimisha. Mimi nashangaa kwanini mpaka sasa serikali haijatafuta suruhu ya suala hili. Watagoma hadi lini? Hiv kwanini serikali isitoe majibu ya kueleweka? Ukwepaji wa kodi upo hadi kwa wale wanaotumia EFD. Kwanini serikali isitumie mashine hizi kwenye mashirika yake? Mfano, NEMC, ERB, CRB na wengine wanapokea pesa nyingi lakini wanatumia vitabu vya risiti badala ya EFD. Kuna sehemu au kitu fulani serikali haitaki kukiweka sawa. Hata traffic barabarani wanapaswa kutumia EFD sio machinga tu!
 
Hata hapa pande za Mwenge naona Misukule imefunga maduka. Nami leo nalingia mauzo make toka nianze biashara mwaka unusu sijawahi kuuza kama hizi siku wafanyabiashara wanazogoma(ga).

Watu wengine ujinga na elimu ndogo ndo vinawatesa. We mtu una kiduka hata mtaji wa m1 hakina. Unasikia ma-papa wa biashara wamegoma eti nawe unawasindikiza kwenye migomo yao! Ujinga mzigo. Mtu huna hata hakiba ya chakula cha wiki unagoma?

Mbaya zaidi kuna wauza magenge eti nao wamegoma kisa ni ukawa... hahahahaha... sa nikabaki najiuliza kwan mgomo wa wafanyabiashara una uhusiano gani na wanasiasa... jirani yangu akanijibu eti waliokua wakihamasisha mgomo ni akina mangi ndio maana baadhi ya watu wakautafsiri kuwa na mlengo wa kisiasa. Tehteh, ujinga mzigo.

Nipo na jirani yangu hapa mwenge tunapiga mzigo kam kawa. Naomba sana miujiza itokee wagome mwezi mzima labda nami naweza kufanya jambo la maana.
 
wachaga moshi wagome KUFANYA BIASHARA? Wakigoma najiondoa jamii forums naapa.Migomo ya kufunga biashara ni kwa ajili ya vikabila visivyojitambua vya mikoa mingine visivyojua maana ya biashara ni nini.Moshi wagome chezea wachaga wewe huwajui.

Ulishawahi sikia hata maandamano ya fujo moshi? Hawataki kuharibu biashara maandamano yote ya fujo ni kwa makabila mengine.Mwanza kwa wasukuma,dar kwa wazaramo,Arusha kwa wamasai na wameru,KIGOMA kwa waha,mbeya kwa wanyakyusa,Iringa kwa wahehe n.k sio moshi.
Jitoe basi tuone acha kukurupuka Moshi hakuna duka lililofunguliwa hata moja.
 
Ndiyo shida ya watu kukaa maofisini na kufanya maamuzi bila kuelewa hali halisi!

Maneno mengine watu wananogesha tu mazungumzo kwamba kodi imeongezeka mara2 zaidi.Isıtoshe ktk biashara, mauzo yana-fluctuate.Hata hvyo kuna waliolipa kodi pungufu kulingana na mauzo au faida iliyotengenezwa.Wakati mwingne wenda mwaka jana walikadriwa na mwaka huu wakatumia EFD ambayo imeonyesha uhalisia wa mauzo kwa % kubwa na hvyo ku-double tozo ya kodı.Lazima tukubali mabadiliko na wote tulipe kodi stahkı au hata nusu yake.
 
hatupaswi kutumia nguvu kuwalazimisha. Mimi nashangaa kwanini mpaka sasa serikali haijatafuta suruhu ya suala hili. Watagoma hadi lini? Hiv kwanini serikali isitoe majibu ya kueleweka? Ukwepaji wa kodi upo hadi kwa wale wanaotumia EFD. Kwanini serikali isitumie mashine hizi kwenye mashirika yake? Mfano, NEMC, ERB, CRB na wengine wanapokea pesa nyingi lakini wanatumia vitabu vya risiti badala ya EFD. Kuna sehemu au kitu fulani serikali haitaki kukiweka sawa. Hata traffic barabarani wanapaswa kutumia EFD sio machinga tu!

Faida inayopatikana kwenye mashirıka ya umma ni kwa manufaa ya serikali hyohyo tofauti na mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom