Wafanyabiashara wadogo tukutane hapa.

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Kufuatia hali ngumu ya uchumi iliyoikumba nchi yetu Tanzania na kupelekea wengi wetu kufilisika na kufunga biashara ,na hali hii mbaya imetukumba siye wafanyabiashara wadogo tu, matajiri huwa si rahisi kufilisika .

Mimi niliamua kwenda Kenya mwaka jana kutafuta fursa za kibiashara baada ya mzunguko wa pesa kugoma kabisa Tanzania, sikuwahi kufika Kenya kabla lakini nilichojifunza ni kuwa wakenya kwenye ishu ya pesa hawataki mchezo kabisa, Nilifanikiwa na hadi sasa ninapata faida mara 10 ya nilivyokuwa napata Tanzania .

Roho Inaniuma Sana kukuza uchumi Wa Kenya na si nyumbani Tanzania ila hakuna jinsi maana mtaji ungekata Kama ningeendelea kubaki Tanzania.
Njooni Kenya wakuu msije mkaishiwa kabisa, hapa mzunguko wa pesa umenawili mno na wenyewe wanadai hakuna Siku itatokea mzunguko wa pesa ukawa shida,

Kwa Sababu wenye Nyumba Tanzania hawataki tuinuke kimaisha na walisema tutaishi Kama mashetani ,sasa sikutaka kuishi Kama Shetani nataka kuishi Kama malaika.

Maisha ni popote, na Kama hujaoa njoo uolee huku huku.
Naipongeza Sana serikali ya Kenya kwa kuinua uchumi,japokuwa ni maskini Kama sisi lakini serikali inahakikisha kuwa wananchi wanapiga pesa mitaani wanapojishughulisha.

Tatizo ukabila ndo unaigharimu Kenya, bila ukabila taifa hili lingekuwa mbali sana.
Sisi Tanzania hatuna ukabila ila hatuna mbele wala nyuma.
 
Twaja huko,uzuri wa wanasiasa wa kenya huwaga hawalewi madaraka na kuanza kunyanyasa raia,

pia kodi zao si za manyanyaso kama sehemu zingine
 
Twaja huko,uzuri wa wanasiasa wa kenya huwaga hawalewi madaraka na kuanza kunyanyasa raia,

pia kodi zao si za manyanyaso kama sehemu zingine
 
Asante kutushirikisha hizo fursa zilizopo huko ila naumia sana kuacha nchi yangu kwenda ugenini kusaka maisha.

Kama viongozi ndio tatizo basi waone aibu kama sisi ndio tatizo basi tulaaniwe milele
 
Twaja huko,uzuri wa wanasiasa wa kenya huwaga hawalewi madaraka na kuanza kunyanyasa raia,

pia kodi zao si za manyanyaso kama sehemu zingine
Njoo mkuu, hali ya maisha ilivyo Tanzania Kwa sasa ni sawa na kuzimu, Viongozi wana roho za kikatili Sana na hawana Upendo kabisa na watu hao, Kenya bila ukabila hili taifa lingekuwa habari nyingine.
 
Njoo mkuu, hali ya maisha ilivyo Tanzania Kwa sasa ni sawa na kuzimu, Viongozi wana roho za kikatili Sana na hawana Upendo kabisa na watu hao, Kenya bila ukabila hili taifa lingekuwa habari nyingine.

Ni kipi haswa napaswa kua nacho ili kukithi vigezo vya kumiliki biashara mjini Nairobi ili kuepuka kadhia kama iliyowapata ndugu zangu Msumbiji? Documents gani natakiwa zieka sahihi?
 
Ni kipi haswa napaswa kua nacho ili kukithi vigezo vya kumiliki biashara mjini Nairobi ili kuepuka kadhia kama iliyowapata ndugu zangu Msumbiji? Documents gani natakiwa zieka sahihi?
Hakikisha tu una passport iliyogongwa viza (ila mara nyingi hawawasumbui watanzania) ukifika Nairobi inategemeana unataka kufanya biashara gani hasa, uwepo wa fursa ni pale unapoweka biashara na kushuhudia mzunguko tofauti na ulikotoka.
 
Ni kipi haswa napaswa kua nacho ili kukithi vigezo vya kumiliki biashara mjini Nairobi ili kuepuka kadhia kama iliyowapata ndugu zangu Msumbiji? Documents gani natakiwa zieka sahihi?

Mkuu, hata siku moja hutawai fanywa na wakenya jinsi walivyofanya Msumbiji, hapa mitandaoni tu ndio uhasama na chuki huwa lakini on the ground mambo tofauti sana. Karibu kenya, fuata sheria na hutasumbuliwa na mtu.
 
Back
Top Bottom