KERO Wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Sumbawanga tunadhulumiwa na Katibu wa CCM Mufindi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nawakilisha kwa Uchungu Mkubwa sana ukiwa ndani ya moyo wangu kutokana na Dhulma tunayofanyiwa na Katibu wa CCM Mufindi bwana Clement Bakuli.

Soko la Sabasaba lilizuka baada ya sisi wahanga tuliounguliwa na moto katika soko la Mandela mwaka 2016 kupewa nafasi tuanzishe soko lingine. Tulianza kuchangia Ujenzi kwa kuandikwa kwenye vidaftari na kuonyeshwa vyumba vyetu.

Gharama kwa kipindi kile zilikuwa kati ya milioni 3 na 4, kwa bahati mbaya hatukuwa tukidai risiti lakini kila mtu anajua kuwa tulichangia kwa asilimia mia gharama za ujenzi.

Kampuni iliyosimamia jambo hili ni ya bwana Bakuli aliyekuwa kipindi hicho yupo katika ngazi za Chama hapa mkoani Rukwa. Siwezi kuelezea walipeana vipi tenda hiyo,ila tu kiwanja ni mali ya CCM. Mchakato mzima wa upatikanaji wa viwanja humu ndani ya soko ulihodhiwa na mwanae aitwa Jose ambaye hakuna asiyejua jinsi alivyouzia watu vyumba mara mbilimbili hadi Baba yake alipomtoa katika nafasi za kampuni yake. Baada ya kukaa miaka kama minne CCM waligawana vyumba na Mr Bakuli.

Tukapata bahati mbaya ya kubaki na Bakuli, kwani wenzetu walioenda CCM walipata nafuu ya kulipa chumba mwezi mmoja mmoja na bei hadi sasa ni 80,000/- na kurenew mkataba kwao ni bure.! kumbuka mizingwe yote hii tumetenganishwa na corridor tu na wenzetu yaani jengo ni moja
Maajabu ni kwa upande wa Katibu aliyebaki na nusu ya vyumba vyote vya soko:

Kwake kodi kwa sasa mkataba ni 150,000/kwa mkupuo wa miezi mitatu ambayo ni kinyume na Sheria ya Mwaka 2005, kifungu cha 26 sheria no 11 ambayo inasema 🙂Kodi itapangwa na kuongezeka kwa kuzingatia Thamani ya eneo linalopangishwa kwa kutegemea bei ya soko}, na sasa alitupa barua ya kusitisha ukomo wa mkataba, na kila anaeenda kurenew mkataba anatakiwa atoe milioni 2-3..sasa unajiuliza kwa sisi Maskini tuliounguliwa vibanda na sasa ndio madeni ya Mikopo tunaanza kuikamilisha ndio anataka kutunyang'anya vyumba.

Je, tuende wapi na Mayatima wetu? Mbona ndio kama mnatuunguzia soko tena.? Hili jambo la dhulma ya namna hii kilio chetu asikie nani? na ndio kura zetu mnataka octoba? na ndio huko Mufindi mmeanza miradi ya ujenzi wa vyumba? nao yaje yawakute kama yetu?


 
SISI WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SABASABA LILILOPO SUMBAWANGA TUNATOA MALALAMIKO KUHUSIANA NA NDUGU CLEMENT BAKULI AMBAE NI KATIBU MKUU WA CCM MUFINDI,ALIYEKUWA SUMBAWANGA, SOKO HILI LIMEPATIKANA BAADA YA KUUNGUA KWA SOKO LA MANDELA 30 OCT 2016. NA SISI WAHANGA TUKAENDA KUGAWIWA MAENEO SEHEMU YA SABASABA INAYOMILIKIWA NA CCM.

MARA AKAINGIA MR BAKULI NA KAMPUNI YAKE YA BEC LIMITED.TUKAANZA KUPIGWA MILIONI NNE NNE ZA BILA RISITI KWA ANAETAKA VYUMBA. TUKANUNUA KWA SABABU YA DHARURA ZA UHITAJI WETU. BAADA YA MIAKA KUPITA CCM IKAGAWANA VYUMBA NA MR BAKULI NA SISI KWA BAHATI MBAYA TUKAANGUKIA KWAKE.

JAMBO LA KUSHANGAZA NI KWAMBA WALIOPO VYUMBA VYA CCM WANALIPIA 80,000 KILA MWEZI. SISI TUNALIPIA 130,000 NA SASA ANAPANDISHA 150,000.




PIA CCM KURENEW MKATABA NI BURE.LAKINI KWA UPANDE WA MR BAKULI KURENEW MKATABA NI MILIONI 2.
JE SISI WENGINE AMBAO NI WAJANE NA TUNALEA MAYATIMA TUFANYEJE? NANI WA KUTUSAIDIA?/? NA DEAD LINE YA KURENEW MKATABA NI MWISHO WA MWEZI HUU.....TUNAOMBA KUSAIDIWA.TUPO ZAIDI YA WATU 85.

TUNAOMBA MR BAKULI AWEKE WAZI MAMBO YAKE YA KURENEW MKATABA IKIWA NI PAMOJA NA KUITISHA KIKAO NA SISI WAPANGAJI WAKE ILI TURENEW MKATABA BILA MALIPO KWA SABABU SIJUI NI SHERIA GANI ANAYOTUMIA YA KURENEW MKATABA KWA PESA.

PIA BEI AMBAYO WENZETU WA CCM WANALIPIA 80000 KWA MWEZI KWANINI SISI TULIPE 150,000 WAKATI NI CORRIDOR TU INAYOTUTENGANISHA. JE TUTAWEZA KUHIMILI USHINDANI WA SOKO NA WENZETU? NAMBA YAKE ZA SIMU NI: 0623627567
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…