Wafanyabiashara kudaiwa pesa za Mwenge

Wafanyabiashara kudaiwa pesa za Mwenge

Kikalove

Senior Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
163
Reaction score
36
Habari,

Jamani naomba msaada wetu, mitaa ya home tuna kitigo pesa kidogo, na nmekianzisha baada ya kukosa ajira juzi wamekuja watu wa serikali za mitaa wanadai pesa za mwenge eti 10000, daa mimi sina na tangu nikue hii ni mara ya kwanza kusikia hili.

Naomba mnijuze hii ni nini na kwa nini wanatuchangisha, na usipochanga nini kinatokea?
 
Na hicho ndo kichaka cha watu kupiga pesa,jamani wenye Mwenge wao waugharamie ndo wanajua faida yake,wananchi watachanga michango mingapi?Mara ujenzi Wa maabara Mara Mwenge na hakuna sheria yeyote inayolazimisha watu kuchanga pesa ya mwenge
 
Mkuu kama hauna elfu 10 we wape hats buku 5 tu.
Michango ya Mwenge wa Uhuru ipo tangu zamani.
Na mbio hizo huwa zinagharamiwa na serikali za mitaa kama wewe hapo ulipo.
 
Habari,

Jamani naomba msaada wetu, mitaa ya home tuna kitigo pesa kidogo, na nmekianzisha baada ya kukosa ajira juzi wamekuja watu wa serikali za mitaa wanadai pesa za mwenge eti 10000, daa mimi sina na tangu nikue hii ni mara ya kwanza kusikia hili.

Naomba mnijuze hii ni nini na kwa nini wanatuchangisha, na usipochanga nini kinatokea?

Kama kwa umri huo hujui maana ya mwenge basi we changia tu kuepusha shari. Kila nchi ina tamaduni zake na mwenge ni mojawapo na ni urithi wetu. Nakushauri toa.
 
kwani huo mwenge ni kwa manufaa ya nani au unafaida gani

nimetoka sasa ofisiya serikali ya mitaa, nimewajibu sina akaniambia kua mimi ni kiburi na sitaki kuchangia tu, wamenitaka niaandike kwa maandishi na nimefanya hivyo... na wamesema si nafanya biashara kwenye eneo lao tutaonana tu
 
Mkuu kama hauna elfu 10 we wape hats buku 5 tu.
Michango ya Mwenge wa Uhuru ipo tangu zamani.
Na mbio hizo huwa zinagharamiwa na serikali za mitaa kama wewe hapo ulipo.

ukweli mimi naomba kwanza watupe elimu kuhusu hicho kitu, kama si hivyo itakua ngumu kuchanga
 
Tena kama munaendelea kuchangia maabara acheni maramoja na hiyo michango muipeleke kwenye MWENGE.toa elfu kumi au hata zaidi ili Mwenge umulike nchi nzima hata kama kuna mgao wa umeme.
 
Kama kwa umri huo hujui maana ya mwenge basi we changia tu kuepusha shari. Kila nchi ina tamaduni zake na mwenge ni mojawapo na ni urithi wetu. Nakushauri toa.

najua kuhusu mwenge ila kuchangia tafadhari nahitaj elim
 
Mkuu kama hauna elfu 10 we wape hats buku 5 tu.
Michango ya Mwenge wa Uhuru ipo tangu zamani.
Na mbio hizo huwa zinagharamiwa na serikali za mitaa kama wewe hapo ulipo.

ndugu vipi wewe umeshachanga?
 
Mkuu kama hauna elfu 10 we wape hats buku 5 tu.
Michango ya Mwenge wa Uhuru ipo tangu zamani.
Na mbio hizo huwa zinagharamiwa na serikali za mitaa kama wewe hapo ulipo.

Wananchi tuna uchungu yaani tuchangie pesa ya mwenge wakati mafisadi wanaiba pesa nyingi hivyo
 
sio upole ndugu me sifaham ndo maana nipo hivi

Mkuu Mwenge una ratiba yake,mkoa nilipo Mimi bado tarehe hazijasogea ila najua itakua mwezi wa Julai.
Na nina miaka 6 sasa hua nachangia maana ni jambo LA wazi na Mbio za mwenge wa Uhuru zina maana kubwa sana katika taifa letu.
 
me nilishawaza kwanini huu mwenge usiwekwe kwenye jumba la makumbusho iwe ishara kwamba kuna kitu kama hicho kilishawahi kufanyika huko nyuma, hii itakuwa historian nzuri sana kwa taifa letu. Lakini hii biashara ya kuukimbiza kila mwaka na unavyo cost hela nyingi, binafsi ninaona ni matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na serikali.
 
Achana nao hao wezi mbona ss huku tarime hatujawahi kuambiwa kuchangia au kila wilaya na utaratibu wao.
 
Aisee hawa jamaa mm hta matendo yao cjayaelew.wamekuj ofcn na barua yao wakitak elf 50 baada yakuona lugha gongana na wawekezaji wakaanz kuongea kwa vitendo....
Hahahahaaaaa. ....kidg niache mbavu kwny kiti...
Wametok kapa hku wakilaumu kuwa tutaonana mbele ya safari.
Tupia kapuni hii nchi inahisa za wananchi nying sn ukianzia rich mooo....iptl...escrow. ...unapat kichomi kbs
 
kwa Tanzania ya Leo Mwenge hauna tija. Enzi za Nyerere Mwenge ulikamata mafisadi. Leo Mwenge unawakinga mafisadi wasikamatwe
 
Huo mwenge na kuchangia pesa za mafuta ya mwenge ilianzia wakati wa Nyerere.

Ni wakati muafaka tukaachana na hayo makosa ya Nyerere, yeye mwenyewe alishasema yeye si malaika na kuna makosa katika aliyoyafanya, basi tuyaache.

Nyerere mwenyewe baada ya kung'ang'ania sana, akaamuwa kung'atuka na kuwacha wengine walete mapya, sisi tunang'ang'ania tu.
 
Back
Top Bottom