Wafanyabiashara Kariakoo na Mateso ya Wenye Nyumba TRA, Ardhi Mko wapi?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,584
6,721
kukiwa kuna anaguko kubwa la uchumi lililosababishwa na wizara ya Ngeleja kwa kutukosesha huduma muhimu ya umeme, wanyabiashara wa majumba ya biashara (Frem) wameendeleza ubabe wao wa kuongeza kodi na kuzidi kuvunja maduka na kuyafinya mithili ya Choo cha Kulipia, kwa kweli heshima ya Nyumba /Duka kwa kariakoo haipo tena , unakuta mtu kajibanza ukutani kama mbu aliyekwepa kipigo, mbali na hayo wenye nyumba wakiona biashara inafana sana watatafuta namna ya kukuondoa huku wakishirikiana na madarari wa majumba ili watengeneze fitina, wenye nyumba huongeza kodi , unaposhindwa humuuzia mtu kwa gharama ya juu sana. Dalali hupata hela zaidi biashara ikiwa mezani.

Jinsi wanavyoiibia TRA, Wenye nyumba hushirikiana na wafanyabiashara ya majumba kuingia ubia wa kujenga ny,umba kwa mkataba wa miaka mitano au kumi, alafu utumia hati ya nyumba kukopea benki, nyumba huanza kujengwa nusu (yaani Ghorofa Moja tu) wafanyabiashara ndogo ndogo na kubwa huwai maduka kwa kutanguliza hela za miaka miwili, hakuna risti ya kupokea hela, baada ya kumaliza stegi ya kwanza, hupewa mikataba , badala ya kukuandikia ameokea million tano, anasema amepokea million 1 na laki 2 , alafu hukutoza with hliding tax hela ya million 5 lakini ulipa kama laki moja. hivyo kuna wizi mara tatu, yaani wa kutumia benki, wa kuiibia TRA na kukuibia wewe hela za w/tax.

Natoa wito kwa TRA, wakala wa Majengo wafike kariakoo wafanye Reseach waache kulalamika kuwa TRA haikusanyi kodi , kwa mtindo huu wa kupandisha kodi kiholela nani atapona? Je ni kweli serikali haina uzibiti wa viwango vya kodi.

Utafiti wa kina niliohufanya ni kwamba kwa kawaida wafanyabiashara wengi hukopa bank ya ACB na Access Bank, Benk nyingine kama CRDB
NMB, Bank M, NBC wao hawaangaiki na wafanyabiashara ndogo kwani wanamashariti magumu, wenyewe hutaka Hati ya Nyumba au Gari la Miaka Mitano tangu litengengenezwe. Hivyo basi hukuta wafanyabiashara wanakuwa na wakati mgumu sana kwa kukimbizana na mikopo, kodi za wenye nyumba na TRA,

Umeme ulivyoafilis wajasirimia mali.
Tangu mugawo wa umeme, wafanyabiashara wa nguo, salon, simu na vitabu wamepata hasara kubwa sana kutokana na muundo wa majumba ya biashara kwani majengo mengi ni undergrund mengine yako ndani hivyo kuna giza sana , kwa mugawo huu hujikuta wanashindwa kuuza, kunyoa kusuka, tunashauri kwa kipindi hiki cha ngawo TRA waende likizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom