Wafanya biashara wawili maarufu wakamatwa kwa tuhuma za kutumia viungo vya maalbino

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Wakulu,

Asubuhi nikiwa hapa duniani nimepata habari kuwa kuna wafanyabiashara wawili maarufu wa nchini wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na utumiaji wa viungo vya maalbino.

Ka nzi kanakopita pita kameniabarisha ya kuwa habari hii imeandikwa katika gazeti moja la kiswahili la leo.Ka nzi hako kamenusa na kunihabarisha kuwa mmoja ya watu hapo ni pedeshee mmoja maarufu mjini hapo mjini mwenye jina linalofanana na mtoto ng'ombe
na mwingine jina lake bado halijafahamika.Ila ka nzi kanaendelea kusaka habari hii na muda mfupi nitawa-update baada ya kuzungumza na kamanda wa polisi wa kanda maalum

Kuna mtu ana habari kuhusiana na hili.?
 
Unamaanisha NDAMA? waliopitia magazeti leo asubuhi watakuwa na taarifa kamili, ila akina sisi tunaotegemea vichwa vya habari tumezisikia kwa juu tu.
 
.........tumuimbie kizaizai eeee,......nikupende kama mutoto anavyomupenda mama yake ndama mutoto ya ng'ombe.....
Kama kweli wanahusika, basi tutasikia mengi saana kabla ya mwaka huu kwisha!!!!!
 
Uhuru wana Website?Mkulu naomba uscan hiyo habari na unitumie gembe-at-amiiforums-dot-com
 
.........tumuimbie kizaizai eeee,......nikupende kama mutoto anavyomupenda mama yake ndama mutoto ya ng'ombe.....
Kama kweli wanahusika, basi tutasikia mengi saana kabla ya mwaka huu kwisha!!!!!

tehe tehe.........Tumuimbie KizaiZai eee, .......Nikupende kama mutoto anavyomupenda mama yake ndama mutoto ya Mombe.....

Hii nimeipenda zaidi, ni kweli wanajihusisha....... Bado kuna Mawaziri nao wanahusika na haka kabiashara kachafu ...... ndo maana hawataki kuchukua hatua kukakomesha wala kuwajibika kwa sababu hiyo.......Tehe tehe Waziri kijana na Msomi... Sema Mzee Mengi.
 
kama ni kweli wamekutwa na hivyo viuongo wapewa kaadhabu kadogo na wao wanyofolewe viungo kama hivyo hivyo walivyokutwa navyo!
 
kizaizai na ndama mtoto wa ng'ombe!!! mapedeshee maarufu wanaoimbwa kwenye bend kila siku
 
kizaizai na ndama mtoto wa ng'ombe!!! mapedeshee maarufu wanaoimbwa kwenye bend kila siku

Mwanakijiji,

Am much more interest on this case,Hivi sheria inasemaje kuhusu watu ambao wanusika na kutumia viungo vya binadamu..

Hiii habari ni nene..wako wapi hawa watu mpaka sasa

Mkuu sanda matuta naomba details zaidi ili nifile vizuri hili suala
 
Ni lazima hawa ndugu zetu wenye matatizo ya ngozi tuwalinde kweli kweli kwani inaelekea hawa wanasiasa wetu wanategemea sana masangoma kwenye chaguzi, na chaguzi ndio zinaanza mwakani; tusipowawekea ulinzi wa kutosha watakwisha!!
 
Hili suala linalowaaibisha watanzania, bado kuna mtu alisema linakuzwa na vyombo vya habari. Hata kama ameuawa mtanzania mmoja tu, ni lazima uhai uheshimiwe. Sasa mapededje wako mtegoni, tutasikia listi ya waheshimiwa wa kura wanaohusika soon!
 
Yale yale ya Mzee Mengi mafumbo mafumbo tu... no names mnatupatia kweli!
 
mkuu masatu
nakumbuka siku naingia JF.MENGI NILIOKUWA NASOMA YALIKUJA KAMA
TETESI,MWISHO KWELI!!SASA M OMBI LANGU TUZIDI KUWAPA MOYO YOYOTE
ATAKAETOA TAARIFA IBAKI KAZI YETU SISI KUTAFUTA UKWELI HALISI LITATUSAIDIA SANA VINGINEVYO KUNA HABARI ZA KWELI WATU WATAOGOPA KUTUMA HUMU!!AMBAZO ZINGEZISAIDIA TAIFA LETU LA TANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hii mbona tulishai discuss kule kwenye "Watoto wa Mjini" karibu wiki sasa?
 
kweli kazi ipo... hawa jamaa hayo mambo ni kawaida kwao na wanatumia ujinga wetu kutekeleza uyama huo, inadaiwa hata uchunaji ngozi uliosumbua sana mbeya ulitokana na soko la huko kwao...maprofesa wote wanaoliza watu mijini kwa kuwapora mali baada ya kudanganya wangewatajirisha chuo chao kipo huko huko......
 
SAKATA la ununuzi wa viungo vya ulemavu wa gozi 'albino' jijini limechukua sura mpya baada ya wafanyabiashara maarufu jijini kunaswa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo akiwemo mganga wa kienyeji na kufanya idadi ya waliokamatwa kuwa watano.

Sakata hilo la kunusurika kutekwa watoto wawili wa familia moja Irine Stanclaus (10) na Gerald Stanclaus (4) wakazi wa Kipawa, jijini ambapo walinusurikwa kupelekwa kusikojulikana na watu wawili waliokamatwa ambao ni Juma Anthony Ndaigwa (26), mkazi wa Magomeni Makuti na Juma Mgai (21) 'Juma Chibuku', mkazi wa Msasani Macho.

Watuhumiwa hao walikiri kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya mauaji yaliyotokea ufukweni mwa habari ya Hindi, Morogoro, Kigamboni na Tandale.

Watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni mganga wa kienyeji, Kulwa Herman mkazi wa Mbezi Matangini, Dar es Salaam, wafanyabiashara maarufu wanaofahamika kwa majina Ndama Mtoto wa ng'ombe na Juma Ally 'Kizaizai'.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni kutokana na juhudi za polisi kufanya msako mkali kutokana na watuhumiwa kuwataja wanaoshirikiana nao kwenye suala la biashara ya viungo vya albino.

Habari kutoka vyanzo vyetu zinaeleza kuwa, hadi sasa idadi ya waliokamatwa kuhusiana na tuhuma za kushiriki kwenye biashara hiyo ni watano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema juzi kuwa, jeshi lake linaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo wanakamatwa.

Alisema kazi ya kuwakamata watuhumiwa imekuwa ngumu kutokana na watuhumiwa kukimbia nyumba zao hata hivyo juhudi zinafanywa kwa kushirikiana na wasamaria wema ili kuweza kupata taarifa walipokimbilia.

"Biashara hiyo imeingia Dar es Salaam hivyo tutashirikiana kuhakikisha wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo wanakamatwa, " alisema Shilogile.

Mama wa watoto hao Evodia Stanclaus alisema alipata taarifa za watoto wake kuwindwa na watu wawili waliokuwa wakirandaranda katika maeneo ya nyumbani kwake wakijifanya kutafuta simu ya mkononi yenye kamera.

Hata hivyo kwa ushirikiano na wananchi waliweza kuwakamata watuhumiwa hao baada ya jirani yake kusikia njama hizo zikipangwa kwenye simu ya mkononi na vijana hao kupitia dirishani na kutoa taarifa za siri kwa majirani wenzake.

Baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na kupata kipigo kikali vijana hao waliweza kuokolewa na polisi waliofika eneo la tukio.

Katika operesheni hiyo tayari mfanyabiashara anayesadikiwa kuwa ni raia wa Burundi mwenye asili ya Kiarabu anashikiliwa na polisi wakiwemo watu wengine watatu kutoka maeneo ya Kimara, Ubungo na Magomeni jijini.
 
Back
Top Bottom