asante sana mkuu..na hamna jinsi yoyote au dawa nyingine zaidi ya kukatwa sehemu uliyoumwa?wenyeji Wa hapa nilishuhudia wakimuua huku wakisema nilishatema Mimi,hana nguvu tena..ni kweli ukimuwahi kutema mate chini,mate yake hayana nguvu tena?
Ni kweli "Kifutu" (Kwa lugha ya kihehe kule Iringa tunamwita "Lipoma"). Ni nyoka mwenye sumu kali anayeweza kukusababishia kifo au ulemavu wa kudumu.
Kifutu akikuuma mara nyingi huacha meno yake hapo alipokuuma. Kifutu hutumia sana meno ya taya la chini la mdomo wake ili kuuma. Kwa sababu hiyo; inadaiwa anapotaka kukuuma huwa anajigeuza haraka na kulalia mgongo wake ndipo anauma na kuacha meno yake sehemu ya jeraha.
Kwanini aache meno baada ya kuuma?
Meno ya mbele ya kifutu ni madogo sana. Size yake ni sawa na mifupa midogo ya samaki. Meno hayo pia yamepinda kuelekea ndani, kwa lugha nyepesi tunasema yamelalia ndani kidogo. Mara tu anapokuuma na yeye mwenyewe kujivuta ili akuachie na aondoke au muhusika mwenyewe kuvuta mguu, mkono au mahala popote ambapo anahisi ameumwa basi hayo meno (au vijimeno kwa kuwa ni vidogo) hung'ooka au kuvunjika na kubakia sehemu ya jeraha alipokuuma.
Mara baada ya kitendo cha kukuuma tu kifutu pia hutema sumu. Meno hayo pia ambayo yanakuwa yamebakia sehemu ya jeraha yanakuwa na sumu ambayo itaendelea kumuathiri mgonjwa. Kama meno hayo hayatatolewa upesi basi mahala palipoumwa panaweza kuathirika zaidi na pengine hadi kuanza kuoza!
KUHUSU KUKATA SEHEMU ALIPOKUUMA:
Kuna mchangiaji mmoja ameshauri kwamba ni LAZIMA kukata sehemu alipokuuma. Mi nipo tofauti kidogo na nashauri kwamba Kama MENO YOTE yatatolewa mapema sehemu ya jeraha mara tu baada ya kuumwa hakuna haja ya kukata.
Kuna nyoka wenye sumu kali zaidi ya kifutu km TAIPAN wanauma lakini watu hawakatwi viungo. Ni suala la tiba sahihi na kwa wakati sahihi.
Kukata kiungo pia utakuwa umesababisha ulemavu mwingine. Kwa mfano; Kifutu amekuuma unyayo na ukaamua kukata unyayo tayari utakuwa na ulemavu wa unyayo na hivyo kukulazimu kuanza kuvaa viatu vya bandia ili uweze kutembea. Vile vile ukikata kidole au kiungo kingine chochote utakuwa umesababisha ulemavu katika mwili wa muhusika.
KWANINI SUMU YA KIFUTU HULETA MADHARA MAKUBWA?
>Watu wengi hawana uzoefu kuhusu tiba na huduma ya kwanza kwa mtu aliyeumwa na nyoka
>Watu huanza kumpa mgonjwa dawa PASIPO kutoa meno kwanza sehemu ya jeraha. Hii huleta madhara makubwa km vile kusababisha sehemu kuanza kuoza
Hospitali nyingi nchini Tanzania hazina watalaam na tiba makini za kutibu sumu ya nyoka. Madaktari wengi huanza kumpa tu mgonjwa dawa pasipo kuchunguza kama sehemu ya jeraha pameachwa meno yanayotakiwa kutolewa kwanza.
KUHUSU UHUSIANO WA KUTEMA MATE NA SUMU YA NYOKA:
Hili suala nimelisikia kwa watu wengi ya kwamba;
Ukimwona nyoka ghafla anza wewe kutema mate. Kufanya hivi kutamfanya azubae na ashindwe kukufanya kitu. Na hata kama ikitokea akakutemea mate au kukuuma basi itafubaza makali ya sumu ya yule nyoka kiasi kwamba haitakuwa na madhara makubwa.
Watu mbalimbali wanadai kwamba hata kwa wanyama wengine km vile kuku kanuni hii hutumika. Kuku akimwona nyoka halafu yeye ndiye akawa wa kwanza kumdonoa yule nyoka basi hata kama yule nyoka atamuuma huyo kuku hatadhurika! Hata km atadhurika itakuwa ni kwa kiasi kidogo na hawezi kufa.
Vile vile kwa wanyama wengine kama mbwa, paka, mwewe, bundi, nk wakianza wao kumshambulia nyoka basi sumu haitakuwa na madhara makubwa. Ndio maana unaweza ukakuta nyoka hata mwenye sumu kali kauawa na paka, bundi au mwewe.
Hizi ni hekima za wazee wetu na huenda zina ukweli ndani yake. Tusizipuuze