Ni kweli chatu hana sumu kali. Hata kama anayo basi ni kidogo sana na haiwezi kusababisha kifo labda awe amekujeruhi sana. Nadiriki kusema hivyo coz NILISHUHUDIA binamu yangu aliwahi kuumwa na chatu ilikuwa mwaka 2008 na alitibiwa tu nyumbani kwa dawa za asili na akaweza kupona.
Kuhusu mkojo ni kweli unasadikiwa kutibu sumu sumu ya nyoka. Kuna watu wengi wametoa ushuhuda kuwa mkojo uliwasaidia. Inasadikiwa kuwa ni mahsusi sana hasa kwa sumu ya nyoka wanaotemea mate; kwetu Iringa kuna nyoka ni maarufu kwa kutemea mate na tunamwita kwa lugha ya kinyalu: "Nyamwilu". Ni nyoka mweusi nadhani kwa lugha iliyozoeleka huwa tunamwita "Cobra" Inashauriwa km nyoka kakutemea usoni basi kojoa mkojo kwnye chombo na uunawe usoni. Kama wewe huna mkojo tumia hata wa rafiki yako utakayekuwa naye karibu.
Lakini pia kama nyoka amekung'ata unashauriwa KUNYWA huo mkojo ili kwenda kufubaza makali ya sumu ya nyoka.
ANGALIZO: Inashauriwa mkojo utumike tu kama ni huduma ya kwanza (first aid). Mtu kama kaumwa na nyoka hususani mguuni au mkononi:
Hatua ya kwanza, tafuta kamba au kitambaa na ufunge sehemu ya juu kidogo na jeraha.
Hatua ya pili, Mgonjwa anywe mkojo, wa kwake au wako
Hatua ya tatu, chanja sehemu palipong'atwa na ukamue ili kutoa damu yenye sumu. Kama mpo porini na hakuna hata wembe tumia hata miiba yenye ncha kali kutoboa toboa sehemu ya jeraha na kuikamua ili kutoa damu yenye sumu
Hatua ya nne, mpeleke mgonjwa hospitali au kituo chochote cha tiba kwa uchunguzi na matibabu zaidi.