Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,189
- 128,279
Iko tofauti kubwa kati 'harusi' na 'ndoa'.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
hao ndo wametambua hasa nn aaa ya ndoa c kma wengne ulimbuken umewajaa
Kaka umeua palepale nilipotaka kuua, kuna tofauti kubwa kati ya NDOA na HARUSI!..watu wanataka ufahari wa harusi, jamaa yeye hajaona umuhimu wa harusi, ni kufunga ndoa tu basi, after all ndoa ni ya wawili wengine ni wapambe tu, na ufahari ni kuwafurahisha wapambe; hiyo pesa ya kuwafurahisha wapambe hawana, na hata kama wangekuwa nayo ingewafaa na mambo mengine. Mimi ndoa yangu itakuwa simple kuzidi hiyo, nafunga ndoa nikitokea ofisini, nusu saa nimesharudi ofisini na mke wangu kaenda zake kazini, hakuna msafara hakuna kulewesha watu ukumbini hakuna complications!
Mimi nina mawazo tofauti kidogo jamaa nikiwaanaglia naona kama wamekosa umakini fulani. Sawa hatutaki gharama lakini hata huyo mpambe wa nyuma kavaa nguo za mazoezi na bwana harusi katia jeans sijui miguuni wamevaa nini. Nami sipendi pia gharama lukuki kwenye sherehe lakini nafikiri walitakiwa wafanye maandalizi kidogo kuanzia kwenye mavazi Sina maana ya shera za milions hapana bali nguo angalau yenye hadhi ya sehemu kama hiyo hapo ndiyo ningejua kuwa wamejipanda kukabiliana na jukumu la ndoa lakini hivi, hapana. Pia kwenye hiyo jumuiya ama jirani yao kuna uwezekano kuna mmoja mwenye gari ambaye angewapa usafiri bure. Huu ni mtazamo wangu
Na pia nikiri kuwa ndoa za namna hii nzaifangilia sana lakini si ki hivi. Kuna mshikaji wangu alio kwa yeye kwenda kanisani asubuhi na mkewe na wapambe wao na wazazi wa pande zote mbili. Ikapigwa misa yakatolewa mawaidha kutoka hapo wakapanda gari hadi home wakanya chai nzito na kufahamiana zaidi (wazazi wa pande zote mbili) basi. Bajeti 117,000/=. (walitumia nguo zao za heshima ambazo walipendeza - Siyo jeans na nguo za michezo ingawa nao walikuwa nazo)
Ndugu yangu ukipata mwanamke atakayekubali hilo...nitakupa hongera milioni!
Safi saana wamefanya kitu chema maana hata mimi yangu ilikuwa kama yao ila mimi hata wali haukuwepo eti. Ili kuwa mimi na mke wangu kaka yangu na kaka ya mke wangu kama mashuhuda zaidi ya miaka kumi na tuna watoto watatu mambo yako powa Jina la Bwana Libarikiwe.![]()
Padri Phidelisi Mwesongo akiwafungisha ndoa Charles Kanyema na Onoratha Pascal.
![]()
Ibada ya wanandoa hao ikiendelea kabla ya kurudi nyumbani kwa mguu.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
WANANDOA Charles Kanyema (29) na Bi. Onoratha Pascal (28) hivi karubuni waliwashangaza wakazi wa Manispaa ya Morogoro baada ya kwenda kufunga ndoa wakiwa wamepanda bodaboda na kurejea nyumbani kwa kutembea kwa miguu.
Ndoa hiyo iliyofungwa katika Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Mjini na kufungishwa na Paroko Msaidizi, Padri Phidelisi Mwesongo iligharimu shilingi 45,000 tu.
Gharama hizo ni pamoja na picha 5 kwa ajili ya kumbukumbu yetu na nyumbani tumenunua mchele na nyama kwa ajili ya sherehe ndogo, alisema bwana harusi Kanyema.
Alisema fedha hizo zilitokana na michango waliyochangiwa na wana jumuiya wenzao na hawakutaka mambo makubwa katika sherehe yao.
Mara baada ya kuwafungisha ndoa, Padri Mwesongo aliwataka wanandoa hao kutambua kwamba maisha ya ndoa ni magumu na yanahitaji uvumilivu ili ndoa yao iweze kudumu.
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe hiyo waliwasifu wanandoa hao kwa kutotumia gharama kubwa wakidai kwamba mara nyingi ndoa zilizojaa kila aina ya mbwembwe huwa hazidumu
HII NDIO NDOA ZILIZOBAKIA NDOA ZOTE NI FEKI NDOA ZA GHARAMA HAZIDUMU HONGERA NA NDOA YENU MUNGU AWABARIKI.