Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,830
KUZIMWA kwa intaneti wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kumelisababishia Taifa hasara ya dola za Marekani milioni 238, sawa na takribani Sh. bilioni 560, kwa mujibu wa ripoti mpya ya utawala wa kidijitali.
Takwimu hizo zimetolewa na Ofisa Sera na Teknolojia wa Tech, Media Convergency (TMC), Robert Majige, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Tanzania Internet Governance Series 2025 mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Majige amesema ripoti hiyo, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Internet Governance Tanzania Working Group (IGTWG), imechambua mwenendo wa utawala wa kidijitali nchini wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, na kubaini mafanikio katika miundombinu ya TEHAMA sambamba na changamoto zinazoikabili haki ya kidijitali.
Ameeleza kuwa kuzimwa kwa mtandao kitaifa kwa siku tano kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3, 2025, pamoja na kuendelea kwa vizuizi dhidi ya jukwaa la X tangu Mei 20, 2025, kumeathiri kwa kiasi kikubwa biashara za mtandaoni, mawasiliano ya kijamii na shughuli za kiuchumi kwa ujumla.
“Hii siyo tu hoja ya teknolojia, ni suala la uchumi na imani ya umma katika mifumo ya kidijitali,” amesema Majige.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hasara ya kuzimwa kwa huduma za intaneti kwa siku tano pekee kuanzia siku ya uchaguzi Oktoba 29 hadi Novemba 3, 2025, ilifikia dola milioni 72.3, sawa na Sh. bilioni 185.
Naya, Mkurugenzi wa TMC, Asha Abinalla, alisema ripoti hiyo ya mwaka 2025 iliyoandaliwa na asasi kadhaa zinazounda taasisi ya kufuatilia mwenendo wa huduma za intaneti nchini na kuratibiwa na TMC inaonesha wazi athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na kutatizwa kwa mawasiliano ya kidijitali.
Kutokana na hali hiyo alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uwiano kati ya udhibiti wa serikali, usalama wa taifa na ulinzi wa haki za msingi za raia katika mazingira ya kidijitali, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kujenga uchumi wa kidijitali unaojumuisha wote na unaoaminika.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Dk. Rose Reuben amesema kwa kiwango kikubwa shughuli za kiuchumi ziliathirika kwa sababu ya kuzimwa kwa intaneti wakati wa uchaguzi.
Amesema hali hiyo iliwasababishia hasara kubwa wajasiriamali hususani wanaofanya biashara zao kwa kutumia mitandao ya kijamii.