Wadau wa Maendeleo wanavyotufahamu vya ndani sana

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,304
24,191
Mahojiano na Mkurugenzi Mkazi- USAID Tanzania

Mahojiano haya yanadhihirisha jinsi wadau wa maendeleo wa Tanzania huwa wanajitahidi sana kutufahamua kihistoria, kitamaduni na kijamii ili waweze kufanya mashirikiano yenye mguso.

Tujiulize kwetu Tanzania tunapowapeleka mabalozi, wataalamu wa mikataba, wataalamu wa kushawishi n.k huwa wanakuwa na uelewa mpana kama wenzetu wadau wa maendeleo toka mataifa ya nje.

Nimesikiliza kwa kina mahojiano haya toka mwanzo mpaka mwisho na kubaini umuhimu wa kuwa na watu wetu waliobobea ili wakienda nje au kukaribisha wageni wawe wa sekta ya gesi, nishati, mashirikiano ya kimataifa, mikataba , kujieleza n.k waoneshe kweli wameiva na siyo wababaishaji wanaoweza kukosa weledi katika kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya nchi

READ MORE : Why we remain invisible in global community https://www.thecitizen.co.tz/oped/W...840568-3008286-format-xhtml-4g5ken/index.html
 
Diplomasia Yetu 3. :Je chuo cha Diplomasia Kurasini, Kinatosha?

Tuko katika nyakati za ushindani mkubwa wa kiucuhumi duniani. Tunahitaji kutafuta fursa zote zinazopatikana nje ya nchi, Je chuo cha Diplomasia peke yake kinaweza kutupatia wataalam wa kutosha kupigania maslahi ya Taifa nchi za nje?

Source: Lameck Kumbuka Jaston
 
Diplomasia Yetu 4

Nchi za magharibi huweka mbele raia wake huku wakijitahidi kutokosana na nchi jiran. Kuna umuhimu wa kutunga sera na sheria zinazomuweka mtanzania mbele Kwanza bila kumbagua mgeni. Hili ni kutokana na utandawazi hivyo ni muhimu kuwa makini katika maamuzi yetu

Source: Lameck Kumbuka Jaston
 
Diplomasia yetu 5: Diplomasia ya Uchumi na Ushindani usio na Tija.

Source: Lameck Kumbuka Jaston
 
Ingekuwa inawezekana, mtu akichaguliwa kuwa Rais, anapelekwa kwanza kwenye chuo cha uongozi na diplomasia kwa miezi 4, kisha chuo maakum cha uchumi miezi 2, ndiyo aje akabidhiwe uongozi.

Fieldwork ijumuishe kutembelea mataifa mbalimbali yaliyofanikiwa ili ajifunze kutoka kwa viongozi wao jinsi wanavyoongoza mataifa yao, ajifunze jinsi taasisi mbalimbali za kiutawala na uchumi zinavyotenda kazi, na jinsi mihimili mikuu mitatu ya kitaifa inavyohusiana, kushirikiana na bila ya kuingiliana. Hiyo ingesaidia sana kuepuka njia tunayoipitia sasa hivi.

Kipindi chote hicho cha miezi 6 anaendelea yule anayemaliza muda wake. Uchaguzi uwe mwezi wa 8, Rais mteule anaapishwa mwezi February.
 
May 16, 2019
Dar - es- Salaam, Tanzania
"Power to the people" - Epic interview with minister of Energy Tanzania

Source : Dr. Mumbi Show
 
May 30, 2019
Dodoma, Tanzania

Waziri Kabudi : Nasema Kamwe Hatutapiga Magoti, Tumeona Vioja Vyao

Source : Millard ayo
 
Ndio mana kelele za Tundu Lissu zimeishia hewani,wadau wanajua kila kitu kuhusu nchi yetu
 
LIVE | Balozi Kairuki afafanua nafasi ya Tanzania kidplomasia
Diplomasia ya uchumi na ushawishi : China na Afrika Je uwekezaji wa China Tanzania unavyozungumziwa ktk mitandao Tanzania unaakisi urafiki-mzuri wa kiuchumi na nchi za Kiafrika hususan Tanzania. Serikali ya awamu ya tano ina mkakati gani kunufaika na uwekezaji wa viwanda vya China nchini.

Source: Kwanza TV
 
19 June 2019
Tanzania USA business dialogue
Prof. Palamagamba Kabudi abainisha Visheni na mkakati mpya wa serikali ya Tanzania kushirikisha wadau wa maendeleo katika uwekezaji nchini Tanzania

Source : millard ayo
 
Ndio mana kelele za Tundu Lissu zimeishia hewani,wadau wanajua kila kitu kuhusu nchi yetu
Wanajua pia kuwa tuna viongozi wauaji na cwatekaji huku wakinukisha uzalendo fake na kutuibia eg 2.4 tln
 
Ingekuwa inawezekana, mtu akichaguliwa kuwa Rais, anapelekwa kwanza kwenye chuo cha uongozi na diplomasia kwa miezi 4, kisha chuo maakum cha uchumi miezi 2, ndiyo aje akabidhiwe uongozi.

Fieldwork ijumuishe kutembelea mataifa mbalimbali yaliyofanikiwa ili ajifunze kutoka kwa viongozi wao jinsi wanavyoongoza mataifa yao, ajifunze jinsi taasisi mbalimbali za kiutawala na uchumi zinavyotenda kazi, na jinsi mihimili mikuu mitatu ya kitaifa inavyohusiana, kushirikiana na bila ya kuingiliana. Hiyo ingesaidia sana kuepuka njia tunayoipitia sasa hivi.

Kipindi chote hicho cha miezi 6 anaendelea yule anayemaliza muda wake. Uchaguzi uwe mwezi wa 8, Rais mteule anaapishwa mwezi February.
Haiwezekani.

Pengine ungependekeza wanasiasa wetu wenye 'inclination' ya kuwa viongozi wajikite huko, na pawe na vyuo vinavyowaandaa katika maeneo hayo kabla ya kujitosa. Mimi nilidhani Kivukoni ilikuwa ni sehemu ya mpango huo, lakini sikumbuki kusikia hata siku moja Rais Magufuli kabla ya kuwania Urais aliwahi hata kuhudhuria seminar tu ya 'uongozi' kwenye nyanja yoyote ile!

Sijui. Kama aliwahi kupata mafunzo yoyote, basi sikupata habari hiyo. Pale Mlimani palikuwepo na somo la "Development Studies", lililohitaji mwanafunzi yeyote alisome bila kujali anafanya Kemia au Computer Engineering. Ni sehemu ndogo ya kuongeza uelewa wa kidunia kwa wasomi wetu nje ya fani zao. Sasa sijui kama naye alilisoma somo hilo.
 
Back
Top Bottom