Wadau wa JF Na Wanazuoni Wote Naomba Mtuelimishe Maana Au Tafsiri Sahihi Ya Maneno Yafuatayo Yaliyonenwa Na Okokwo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Wadau wa JF

Mpaka leo sijapata tafsiri sahihi ( Kisiasa, Kiuchumi & Kijamii) ya maneno yafuatayo ambayo yaliyotamkwa na Ndugu Okokwo

"I can not leave on the bank of the river and wash my hands with a spittle"

Mwenye uelewa mzuri basi naomba atuelimishe wengine
 
Wadau wa JF

Mpaka leo sijapata tafsiri sahihi ( Kisiasa, Kiuchumi & Kijamii) ya maneno yafuatayo ambayo yaliyotamkwa na Ndugu Okokwo

"I can not leave on the bank of the river and wash my hands with a spittle"

Mwenye uelewa mzuri basi naomba atuelimishe wengine
Spittle ni "mate mate" ambayo huwa yanajaa mdomoni hasa ukiwa umesikia hamu ya chakula. Sasa mtu ambae anaishi kando ya mto maana yake maji kwake sio tatizo.... Hivyo hawezi akaijisafisha mikono yake kwa kutumia mate wakati maji kibao yapo karibu yake yanatiririka kwenye mto, akitaka kuosha mikono yake atatumia maji ya mtoni.
Kiuchumi maana yake ni kwamba mtu ambae ana uwezo mkubwa kiuchumi hawezi kujibana bana kwenye mambo madogo madogo yanayohitaji fedha kumrahisishia maisha; kwa mfano hawezi kusafiri umbali mrefu lets say Dar hadi Mwanza kwa basi au gari atumie masaa 16 njiani (spittle), atapanda zake ndege au helicopter, dakika 30 tu yuko zake Mwanza, kwa sababu pesa (maji ya mto) kwake ipo ya kutosha.
Kijamii sasa ni kwamba kila mtu ana maji ya mto ndani yake ya kutosha, kwa maana ya uwezo wa kiakili kufanya chochote kile, hivyo anaweza kutumia uwezo wake huo kiakili kuweza kupata haja ya moyo wake badala ya kulalamika na kutumia mate kuosha mikono yake, wakati anaishi karibu na mto (ana ubongo wenye uwezo wa kufikiria na kutimiza makubwa).
Uzalendo Wa Kitanzania
 
Back
Top Bottom