Wadau wa filamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau wa filamu

Discussion in 'Entertainment' started by Jumakidogo, Oct 7, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Waandaaji wa filamu nyingi za bongo mnaboa sana, hivi hamjajua tu kuwa hadithi za filamu zenu nyingi hazivutii? Unaweza kuwa na kipaji cha kuigiza, halafu usiwe mtunzi mzuri. Kila mtu mungu kampa kipaji chake. Hadithi ndio msingi wa filamu bomba, nchi inao watunzi waziri wa hadithi waliobobea. Mfano Erick Shigongo, Beka Mfaume, Hussein Tuwa, Juma Kidogo, Sultan Tamba na wengineo. Mkiwatumia hawa, mnaweza kujikuta mnatengeneza filamu zenye viwango na ubora wa hali ya juu.
   
 2. A

  AZIMIO Senior Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hilo nalo neno
   
 3. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yaani huwa wananichefua sana vi maigizo vyao afu eti wanaita filamu.....
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280

  Hili jambo bana hata mimi niliwahi kulizungumzia zamani kidogo kwenye lile jukwaa la haya mambo! Niliwaambia wazi kwamba, hadithi ikiwa mbovu; hata ukimchukua mwigizaji toka Hollywood au Nollywood bado filamu itakayochezwa itakuwa mbaya tu coz' msingi wa filamu ni stori! Stori nyingi zinazozaa filamu zetu hazina mvuto; msuko wa matukio ni mbovu; no climax zones (kilele), na nyingi zinaishia baba mwenye nyumba kumbanjua house girl!!!! Hawana budi kufahamu kwamba si kila mtu anaweza kutunga stori kwa maana ya stori; na ni ngumu kidogo mtu kumfundisha kutunga stori kv ni suala linalohitaji inspiration zaidi ili kutengeneza best stori. Unaweza kumfundisha mtu kuigiza lakini ni ngumu kidogo kumfundisha mtu kutunga stori; sana sana utaishia kumpa misingi tu na mambo mengine ni mwenyewe anatakiwa kuwa key player. Therefore, nami naunga mkono kwamba hawa jamaa watafute watu wenye vipaji vya utunzi ikiwa wanataka kuwa na stori hai ambazo zinaweza kumfanya mwagaliaji filamu kuiangalia filamu husika mara kwa mara! Nazani hata mimi nipo tayari kusaidia ktk hili tena bila malipo!
   
 5. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  usiombe hadithi iyo akawa mtunzi ray utakomaje mana kabla hajasema kitu ushajua anataka kusema nn loh!....................
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Hivi umefanya utafiti kabla hujaandika uliyoyaandika au umekurupuka tu
  ili mradi nawe uonekane unajua kukosoa? Kwanza nakubaliana nawe kuhusu
  filamu za Bongo kuboa kwa kuwa kila mtu sasa anadhani kuwa anaweza
  kutunga wakati kuna watu waliopewa vipaji vya utunzi. Lakini sikubaliani
  kabisa na wewe kuhusu aina ya watunzi uliowataja kwa kuwa nawafahamu
  vizuri, Eric Shigongo amekuwepo kwenye game na ametunga hadithi
  kadhaa zilizotengenezwa movie (kama Fake Pastors, Froma China With Love)
  na hazina tofauti na hizo filamu zingine za Bongo zinazoboa. Sultan Tamba
  ndiye kinara wa kutunga hadithi za filamu nyingi ambazo hazina kichwa wala miguu...

  Beka Mfaume na Hussein Tuwa ni watunzi wazuri wa riwaya lakini hawana uwezo
  wa kuandika script kwani script ina misingi yake na hata hadithi zao zina mambo
  ambayo ili kuyafanikisha kwenye filamu zetu unahitaji kuwa na bajeti kubwa mno
  ambayo kwa soko la Bongo ni sawa na ndoto za mchana. Juma Kidogo hana tofauti
  na baadhi ya watunzi ambao hadi sasa wameshindwa kulipenya soko letu kwa kuwa
  ili filamu iwe bora kama unavyosema inapaswa kuwa bora katika mambo matano na
  si hadithi peke yake kama unavyotaka watu waamini. Pia ieleweke kuwa mtunzi mzuri
  bado hakukusaidii kuifanya filamu iwe nzuri kwa kuwa huijui misingi ya uandishi wa script
  (mwongozo andishi wa filamu)...

  Filamu nzuri lazima iwe imekamilika katika mambo haya: (i) Script nzuri, (ii) Waigizaji wazuri,
  (iii) Muongozaji mzuri, (iv) Wapigapicha wazuri, na (v) Mhariri mzuri. Katika haya utagundua
  kuwa ubora wa filamu hautegemei hadithi tu ambayo hata hivyo inapaswa ipate mwandishi
  wa script mzuri katika kuijenga (dramatise) na kuisuka (plot) katika namna ya kusisimua,
  kuvutia na wakati mwingine kuhuzunisha kutegemeana na kisa chenyewe.
   
Loading...