wadau wa filamu bongo fungueni macho nje ya mipaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wadau wa filamu bongo fungueni macho nje ya mipaka

Discussion in 'Entertainment' started by johnmashilatu, Apr 26, 2011.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  wadua wa jf
  niko katika mji wa osnabruck nchini ujerumani ambako kesho kunazinduliwa tamasha kubwa la sanaa linalokwenda kwa jina la 24th Eupoean media art festival. sanaa za aina mbalimbali zinashirkishwa

  katika tamasha hilo filamu kutoka maeneo mbalimbali duniani hupokelewa na baadaye kuchaguliwa zilizobora ambazo hupatiwa tuzo.

  waandaaji wanasema kuwa hakuna msanii au mwandaaji wa filamu hata mmoja kutoka afrika mashariki na kati am,bao wamewahi kushiriki katika tamasha hilo ambalo ushiriki wake ni bure

  wanachotakiwa kufanya wasanii wetu ni kwenda katika Home na kupata maelekezo ya kujisajili.

  bila shaka ujumbe huu utawafikia wasani wetu ambao hutumia muda mwingi kulalamikia kutofaidika na jasho lao,kumbe wanaweza kutumia njia nyingine pia kufaidi jasho hilo.

  Nawakilisha
   
 2. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu asante kwa kutuhabarisha. Unajua sisi wadau wa filamu tumezoea kufukiri ndani ya box tu. Tunadhani maonesho kama hayo ni ya Ulaya pekee. Tutafanyia kazi. Asante tena kwa taarifa.
   
 3. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Pole wee, Tanzania hakuna filamu. Hapa kuna home-made videos ambazo hutayarishwa na Kanumba, huigizwa na Kanumba, huwa directed na Kanumba, co-staring Kanumba, written by Kanumba, edited by Kanumba and Cameras by Kanumba. Wateja wake wengi ni akina mama wenye huzuni au wale ma house-maid pamoja na mabinti wa shule (form 2 and below ambao pia humpenda Marlow).

  Eti waje ulaya kuonesha nini? Be serious
   
 4. C

  Clego Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya hayo Filamu zenyewe zimetungwa na kuandikwa ndani ya wiki moja! Actor mmoja anauwezo wa kutoa filamu mpaka tatu kwa mwezi halafu anajiita Super Star!
   
 5. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huwa naogopa kusema uliyoyasema kwa kudhani nawaza hivyo peke yangu na watu wangenizomea, kumbe tuko wengi.
   
 6. FYATU

  FYATU JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 3,954
  Likes Received: 2,163
  Trophy Points: 280
  Akina Kanumba na wenzake wanajaribu kufanya kile kinachowezekana, na ndicho wanachofanya. Suala la filamu linahitaji kuwa na INDUSTRY. Na si rahisi kuwa hivyo bila support ya serikali. bahati mbaya tuliyonayo Bongo hakuna utashi huo badala yake kinachofanyika ni biashara kati ya kanumba na wadosi. Nilidhani badala ya serikali (TBC -shame on you) kuagiza TAMTHILIA iliyotafsiriwa kwa kiswahili kutoka china mngetafuta MWALIMU wa "ACTING FOR THE CAMERA" ili tupate waigizaji kama hao wa china ili tuwe na kazi zetu za maana. Waigizaji wetu wakipewa SCRIPT zinazotumiwa HOLLYWOOD wote wanatoka kapa na ndio maana Kanumba na Ray wanaandika wenyewe. SHULE KWANZA kama tunataka kuwa na FILAMU. Angalau upande wa CAMERA tuna watu kama ADAM JUMA namkubali huyu jamaa kwenye eneo hilo. wanachopigania wasanii wetu ni HATI MILIKI wanachowaza wao ni hela. Piganieni shule ya ACTING koz acting is not a joke kama mnavyofanya my friends. na nyie kina Kanumba mnapozichanga hela za wadosi tafuteni shule sio kununua magari. Mnamtegemea nani awetafutie shule ? Mdosi anachotaka ni hela dili yenu kwake ikiisha na urafiki unaisha mimi nawajua hawa jamaa.
   
 7. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Wewe ni fyatu ndio....lakini umeandika vitu vya msingi sana! Very good advice umetoa.
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Na filamu zenyewe ni ushuzi mtupu.
  yaani kila movie ni part 1 na 2, then ukiangalia cha kuweka part zote hizo ni ushuzi mtupu.

  Kwanza muda mwingi hupotea kwa kazi bure tu, yaani unaweza kukuta Kanumba anatembea kuanzia Mlimani City mpaka Mwenge huku Camera inamchukua tu.
  Ye anatembea mara achume jani atafune, mara apige teke kopo, then camera inamchukua tu huku instrumental inarindima tu...

  Yaani muda mwingi wa movie hupotea kipumbavu kabisa.

  sioni sababu ya hizo movie hata kuonyeshwa kwenye mabanda ya kuonyesha mapicha huku uswahilini, coz hazina viwango, ubora au mvuto.


  Huwezi kuifananisha movie yoyote ya hapa Tanzania na movie kama Tsotsi, au movie kama wit licht, au movie kama the white Masai.


  Kanumba, Ray na ushuzi wenzenu nendeni shule ili mfaidike na vipaji mlivyonavyo.
   
 9. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Au utakuta kale ka instrumental kana sauti kubwa kuliko hao waigizaji...yaani hawasikiki kabisaa... Lakin wanaongozwa na director kabisaaa, na shugghuli nzima ya editing huwa inafanyika...sijui ni vipi hawa watu jamani..
   
 10. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Haswaaa mkuu
   
 11. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi hizi ni filamu au michezo ya maigizo?
   
 12. Bosi Michembe

  Bosi Michembe JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh! Hii kali.. But ukweli ndio huo bongo filamu bado sanaaaaaaaaa.....
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pia Luga ni tatizo kubwa kwa wasanii wetu, hata kutembelea mitandao mbalimbali through internat hawana kabisa hiyo obi kabisa
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  so so so sad kwa kuja kuendela ni ngumu
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwakweli kama wasanii waTz wanampango wa kuitunza kazi yao wajiingize kwenye mauzo ya kimataifa kwani watakuwa na watakutana na challenge za kuwaelimisha
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mkuu Shine.

  Ebu tuambie ni kazi gani ziingizwe au unazungumzia upuuzi wa kanumba na Kagosi sijui Kigosi ?.Kazi zao zinatakiwa ziishie Manzese na Uswahilini Ulaya hawana muda mchafu.


   
 17. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi bure
   
Loading...