Wadau nguo zangu nyeusi suruali na shati zimepauka nitafanya nini zirudi kuwa mpya tena

gasgas

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
1,090
978
Habari za mchana kwenu.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ninahitaji dye kwa ajili ya kuweka kwenye nguo nyeusi zilizopoteza rangi ili zirejee katika rangi yake ya mwanzo.

Sifahamu kwa hapa Dar es Salaam wapi ninaweza kupata.

Nimeona zinauzwa Amazon, Ebay ila mchakato wa kuagiza utanigharimu hela nyingi sana na usumbufu wa hapa na pale kwa kuwa sinunui kwa jumla.

Hivyo naomba mwenye kufahamu namna ya kunisaidia ajitokeze.

Jioni njema
 
Habari za mchana kwenu
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ninahitaji dye kwa ajili ya kuweka kwenye nguo nyeusi zilizopoteza rangi ili zirejee katika rangi yake ya mwanzo.

Sifahamu kwa hapa Dar es Salaam wapi ninaweza kupata,
Nimeona zinauzwa amazon, ebay ila mchakato wa kuagiza utanigharimu hela nyingi sana na usumbufu wa hapa na pale kwa kuwa sinunui kwa jumla

Hivyo naomba mwenye kufahamu namna ya kunisaidia ajitokeze

Jioni njema


Ukiipata, tafadhali utujuze nasi pia ni wahitaji.
 
Sina uhakika kama inawezekana, labda tungoje wataalamu wa Mavazi watuambie.
 
Karibu kwa ushauri bado nazipenda na zimewahi kupauka kabla ya muda shubaaaamitt!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom