tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Katika kupita Ifakara Mkoani Morogoro wilaya ya Kilombero nilienda mpaka mto Kilombero smbako kuna daraja lililozinduliwa na Rais Magufuli mwaka Jana.
Wakati Niko upande wa wilaya ya Kilombero kibao Cha daraja kimeandikwa Daraja la Magufuli au Magufuli Bridge na ulivuka upande wa wilaya ya Ulanga kibao kimeandikwa Mgulungulu Bridge au Daraja la Mgulungulu.
Nilijaribu kuwauliza watu Kama wanna hivi kujua Kama wanajua maana ya Mgulungulu lakini wote walikuwa hawajui.
Sasa Kama Kuna mdau anajua maana ya hilo neno na kwanini kuna vibao viwili ktk daraja moja na majina tofauti?