Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 45,278
- 37,073
ni muhimu sana kumaliza weekend kwa kua bize kwenye nyumba za ibada au mahali pako pa siri kumshukuru Mungu kwa namna alivyokupigania wiki nzima iliyoisha, na kumuomba baraka na neema zake tena katika kazi na majukumu ya wiki inayokuja.Habari za jioni wana-JF,
Nimeona nije hapa jukwaani kuandika haya machache, huenda kuna wanaopitia hali kama yangu au waliowahi kuivuka wakashare nami namna ya kukabiliana nayo.
Mimi ni mtu ninayependa sana kuwa busy na majukumu yangu. Kipindi cha nyuma, nilikuwa na vitu vingi vilivyonipa burudani na kunichangamsha; nilikuwa mpenzi mkubwa wa kusikiliza Music [emoji444], kuangalia filamu, na hata kutoka mara moja moja. Upande wa pombe nilishaamua kuacha kabisa huko nyuma.
Hata hivyo, siku hizi mambo yamebadilika kabisa. Kila Ijumaa inapoingia , kwangu inakuwa ni mwanzo wa stress na boredom ya hali ya juu.
Yale mambo yote yaliyokuwa yananipa furaha mwanzo (muziki, muvi, mitoko) sasa hivi vimepoteza ladha kabisa, nikijaribu kuvifanya nahisi upweke na muda hauendi.
Hata upande wa mahusiano umekuwa na changamoto sana, kwani imekuwa ngumu kukutana na watu wenye uelewa na ukomavu wa akili unaoenda sawa na mimi.
Kimbilio langu pekee limebaki kwenye kazi. Hamu yangu kubwa kila weekend inakuwa ni kutamani Jumatatu ifike haraka ili nirudi kwenye majukumu yangu ya kila siku, kwa sababu huko ndiko akili yangu inapotulia.
nadhani huu ndio unapaswa kua ustaarabu muhimu zaidi wa kumaliza weekend, na Mwenyezi Mungu awabariki sana wadau wa JF wote 🐒