Ushahidi ni mwingi juu ya wazungu kuchukua biashara hii kwa kiasi kikubwa
Fika Arusha na uliza mamlaka zinazo husika utajua ukweli haya si madai pekee hata last week yalikuwa kwenye gazeti la Mwananchi ni hatari .
Tatizo siyo wazungu kuchukua biashara.Kama wazungu wanachukua biashara kwa kufuata sheria sioni tatizo.Kama sisi wenyewe tunalala na hatufuatilii wazungu watachukua tu, after all tupo katika free market economy.Tusianze kuleta racism katika kutetea incompetence yetu wenyewe.Kitu ambacho hujaonyesha na ukikionyesha nitaku support ni kama wazungu wanatumia njia za mkato au rushwa.Ukionyesha hivyo nitakuwa wa kwanza kuku support.
Juu ya Mwenguo hili ni sawa la Siasa na biashara .Mwenguo hakatazwi kufanya biashara ya Utalii wala nini .Lakini uaminifu wake utakuwa wapi ? Abatakiwa kutoa maamuzi huyu je anaweza kutoa maamuzi ya kuimiza kampuni yake ?
Kwanza hii siyo siasa, ni uongozi wa shirika la umma.Tatizo ni kuwa hata kama ingekuwa siasa unachoongelea ni miiko ya uongozi ya Azimio la Arusha ambayo ilitenguliwa na Azimio la Zanzibar, ambalo nalo rais Kikwete ametoa kikauli controversial cha kuli reverse bila kutumia kikao chochote cha chama, kwa hiyo reversal hiyo inakosa credibility.
Kama kuna issue specific inayoonyesha hawa watu wame abuse positions zao za TTB kupata an unfair advantage then ilete hapa tui discuss, lakini huwei kuwazuia watu kupata kipato cha ziada just because wao ni ma directors wa TTB.Hawa watu ndiyo wanatakiwa kuwa mifano kwa watanzania wanaotaka kufanya biashara ya utalii as long as hawatumii vyeo vyao kupata advantage.
Kuna school of thought inayosema sababu moja ya rushwa ni kwamba professionals wanategemea kazi zao tu na hawana extra source of income.Kama tutaruhusu watu professionals (non politicians) kufanya biashara tutawapa mwanya wa kupata extra income na kuondoa vishawishi vya rushwa kazini.Of course hii itafungua mwanya wa abuse of position, lakini jibu si kufunga mlango kwa wote bali ni kutafuta specific cases of abuse of position, then hold those people accountable.Tusilete mambo ya mtego wa panya unaokamata waliokusudiwa na wasiokusudiwa.
Kitendo hiki kama tuna kikubali basi Mkapa asinyoshewe kidole kwamba alifanya biashara akiwa Ikulu .Unasemaje nalo hili ?Ushahidi wa hawa jamaa kufanya biashara nitaumwaga hapa soon.
Prudence inaweza kufanya watu kama marais wasijishughulishe na baishara kabisa, kuondoa any possibility ya maswali kuhusu uadilifu.
Tatizo la Mkapa siyo so much kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu (Azimio la Zanzibar liliondoa huu mwiko wa uongozi wa CCM, ndiyo maana kina Msekwa na wengine wengi walikuwa board members Vodacom etc) bali tatizo ni kwamba Mkapa alichukua hela (Deep Green) na mashirika (Kiwira) kinyume cha sheria, alichukua tu, hakununua au kushindania katika tender.
Je maadili ya kazi je ?Sijajua sheria ya ajira inasemaje ila siamini inaweza kusema kwamba ukiwa mkurugenzi bado unaweza kuwa na kampuni ya huko huko ambako ualipwa pesa ya walalahoi.Hili si kutangaza Kaka .Ni swala la maslahi binafsi na wakati wa kufanya maamuzi na ku dominate hata contacts zote .Je ni haki ?
Usituambie unachoamini, tuambie unachojua.Lete facts sio speculations.Kama hata hujui maadili ya kazi yanasemaje kuhusu hili utawezaje ku accuse conflict of interest?
Hizi kazi si kazi za kisiasa, ni kazi za utendaji.Whats next, mtasema engineer wa serikali asiwe na ki workshop chake mtaani kwa sababu itakuwa conflict of interest?