Wadau, huyu mshikaji yuko viipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau, huyu mshikaji yuko viipi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Manyanza, May 21, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Habari za week end wadau?
  Naomba tusaidieni kimawazo kwa hili;

  Kuna mshikaji wangu, nimemsoma ana tabia fulani ambayo nashindwa kuielewa lakini kwa kuwa nimeileta hapa jamvini nitasaidiwa kimawazo... jamaa nilikutana naye kama miezi sita iliyopita nilikuwa na tatizo na simu yangu na yeye ni customer care katika kampuni ya Airtel, baada ya kufika pale alinisaidia tatizo langu nikaondoka, mida ya jioni nilipita Bar kupata moja moja bahahti nzuri tukakutana nae basi tukaendelea kukata maji tukabadilishana namba za simu tangu hapo tukawa tunawasiliana.

  Kuna kipindi alisafiri kwenda Arusha alipokuwa kule alinipigia simu anashida na kiasi cha pesa kama Laki Moja nikampatia alikaa kama mwezi na siku kadhaa akarudi, matokeo yake hakuniambia chochote akanyamaza tu, na mimi sikumuuliza chochote.

  Siku nyingine tena tulikuwa tunapata moja moja alikuwa na demu wake, akawa ameishiwa cash akaenda Bank lakini karibu ATM nyingi za jirani zilikuwa hazifanyi kazi akanipiga tena mzinga nikampa elfu 50, akaondoka na demu wake.

  Siku iliyofuata akanilipa sh elfu 30 akasema nyingine atanipa siku inayofuata, matokeo yake hatukuonana karibu wiki mbili, na nilipokuja kuonana nae hakusema chochote.

  Tukaenda kupata nyama choma na lager kama kawa siku hiyo alilipa bili yote yeye, baada ya hapo mimi nikaenda zangu home na yeye akaenda zake kwake. Last week ijumaa usiku nikamkuta Bar yupo na demu wake nikajoin nao tukapiga lager na nyama choma baadae akasema twendeni club, tukaenda club.

  Baada ya kufika club demu wake akawa anataka wine, na yeye hakuwa na cash ya kutosha maana tulikuwa tayari tupo fiti kichwani na mimi sikutaka kumwangusha nikampa elfu 25 akachukua chupa ya wine kwa ajili ya demu wake. Ilipofika time ya kurudi home akalipa taxi, kila mtu akaenda zake home, kesho yake asubuhi nikamtumia sms nikamkumbushia hela zote ninazomdai hakunijibu akakaa kimya hakujibu kitu.

  Leo mchana demu wake kanipigia simu anaomba shiling elfu 35 kaambiwa na jamaa yake achukue kwangu akirudi jioni atanirudishia na mimi nikampotezea, nikamwambia sipo around mpaka jioni. Nimekaa jioni nimepigiwa tena simu nikamwambia nipo kwa washikaji nitamcheki.

  Wadau, tukiwa kama familia moja hapa JF hasa jukwaa hili naomba ushauri wenu maana jamaa simuelewi, ni miezi sita nimejuana nae lakini ana tabia ya kukopa na huwa harejeshi halafu kitu kingine yeye ni mfanyakazi kampuni ya simu Airtel ina maana hana rafiki au jamaa anaofahamiana nao?
   
 2. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Dah! Una moyo mkuu! Kifupi sioni kama ana tabia njema! Si mstaarabu kuwa nae makini...ikibidi keep distance
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa wifi yangu,,mbaya zaidi anafikia hatua ya kumtuma demu wake bila yeye kumpigia kwanza rafiki yake aongee naye ndo amwambie demu wake akachukue hela.....disrespectful!! kwa ufupi uwe unamwambia huna hela.....si utakuwa umeepuka kutolipwa bali utaepuka ugomvi na hasira zisizo na lazima!pole!
   
 4. s

  shosti JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  jamaa na demu wake wote vimeo,ila nawe ulikuwa mrahisi sana
   
 5. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  labda unajionyesha mtu wa mapene,halafu sio mchoyo...next time mwambie huna sio kila mara akitaka unampa hata mtoto mdogo akililia pipi ukimpa ndio utakuwa mchezo wake kulilia tena na tena....
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wise Lady na Michelle asanteni kwa mawazo yenu asanteni, kweli unachosema Michelle ni sahihi waka
  ti mwingine nikifikiria huwa napandwa na hasira sana lakini huwa na maintain mahusiano yasiharibike lakini kweli jamaa anakera ile mbaya na inawezekana huko ofisin wameshamchoka wenzake.
   
 7. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nipo simple sana na sina tabia ya kujionyesha kabisa.. asante kwa mawazo yako!
   
 8. s

  shosti JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  tatizo sio kujionyesha ila kuna watu wameumbwa hawana haya,halafu kama si tabia zako unaweza jikuta unamkopesha tu kwa bumbuwazi
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Umjue mtu miezi 6 na kumkopa hela halafu hajarudisha unamkopa tena? Be brave, akurudishie hela zako na acha kuwasiliana nao!!
  Wanapenda vya bure hao, hata aibu hawana..
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kweli BJ nahisi mshikaji hana aibu kabisa na tabia yake ya kukopa ni sugu.. naendelea kupata mawazo ya wadau halafu nitayajumuisha nitapata solution.
   
 11. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kijana acha utan na hela, mmbanie ka ni urafiki uishe, ila pesa zako akulipe.
   
 12. k

  kisukari JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  watu wengine wapo hivyo.halafu siku ukimnyima,na urafiki unaisha au anakukasirikia bila sababu.huyo anaku use kwa manufaa yake,achana nae
   
 13. M

  Maega Senior Member

  #13
  May 21, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama vile namjua huyo jamaa maana kuna jamaa mmoja namfaham anafanya kazi hiyo hapo hapo Airtel ana tikadi hizo hizo
   
 14. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yawezekana mkuu!
   
 15. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Pole sana mpendwa

  Kumbuka wema usizidi uwezo..
  sasa hao wanachukua advantage yako..
  sababu wameshagundua Una moyo wa kutoa.. huyo si rafiki dear mpotezee..
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mkuu mpotezee kibingwa mdai chako na mwambie wazi urafiki ufe hakuna urafiki wa aina hiyo mkuu maana naona anataka kubenefit kutoka kwako
  Na kama ni mtu mstaarabu hawezi kumtumia msichana wake kuja kukuomba pesa wewe wakati hajakuambia kama mshkaji wako alipaswa akuambie kwanza kuwadem wake ana shida na yeye hana pesa anaomba umsaidie na sio dem wake aje direct kwako
  Mdai chako na mpotezee mazima
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa pole sana;

  Pili jua kwamba inawezekana hata huko anakofanyia kazi washamchoka na ndo maana hana rafiki wa kumwambia matatizo yake maana sio siri huwezi ukawa mfanyakazi wa kampuni kama Airtel na usiwe na marafiki.

  Tatu mkuu dai chako na umteme maana sidhani kama hapo kuna urafiki ni urafiki wa someone kubenefit kutokana na urafiki huo na hapo ni yeye anafaidika kutokana na k uwa na urafiki na wewe. Muhimu mwambie akupe pesa zako zote kisha mteme kiaina.

  Tatu sio ustaarabu kumtuma dem wake kwako umpe pesa wewe kama angekuwa ni mshkaji mwenye busara angewasiliana na wewe kwanza akuombe kuwa hali kwake sio nzuri na dem wake anataka pesa then wewe umpe jamaa pesa ampe dem wake na sio vingine.

  Kumtuma dem wake kwako wakati hata mawasiliano ya kirafiki hakuna sio ustaraabu. Mambo yakiwa ovyo kati yetu wanaume tunamaliza kiaina bila hata madem zetu kujua sasa yeye anajianika wazi kuwa anakopa pesa mbona mshkaji sio mstaarabu kabisa.
   
Loading...