Wadau hawa wa elimu wamepotelea wapi?

hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
1,356
1,437
Salaam alaikum,

Zamani kabla ya 2010 kurudi nyuma huko tulizoea kuona vitabu vya namna mbalimbali kwa maudhui moja. Namaanisha somo husika kwa darasa fulani linakuwa na matoleo kibao ya vitabu (waandishi na wachapaji)

Hii ilikuwa inasaidia wadau kuchagua vitabu wanavyoona wao vitawasaidia na nakumbuka ikawa inaleta ushindani fulani kwenye maendeleo ya elimu yetu. Kwa vyovyote vile mabadiliko tuliyopiga katika elimu yetu inaonesha wale waandaaji wa vitabu vile wamesaidia sana mpaka kufika hapa tulipo

Sasa cha ajabu kumekuja utaratibu huu wa kwamba vitabu vyote vinaandaliwa (uandishi na uchapaji) na Taasisi ya Elimu Tanzania ndo basi tena sijawahi kuona tena vikitolewa vitabu tofauti na hivyo vya Taasisi ya Elimu Tanzania

Mashaka yangu (au niseme swali langu) ni kama hawa watu wamezuiwa kuandaa vitabu hivyo au nini? Maana kwa zama tulizonazo sasahivi naona kama wangeendelea ingeleta tija zaidi lakini siyo hii ya kila kitu kutolewa na Taasisi ya Elimu.

Binafsi naona hata mvuto ule umepotea sasahivi siyo kama enzi zile unakuta mtoto asipoelewa kitabu hiki anakwenda kuelewa kwenye kitabu kile kingine. Kwa mfano nakumbuka enzi tunasoma ilikuwa mtu mwenye vitabu vya Oxford ndiye mjanja na hata bei zake zilikuwa juu kidogo kulinganisha na wengine. Kwa wale wa Lugha nakumbuka vitabu vya English vya kampuni moja kutoka Kenya vilikuwa vinauza sana. Sasa hivi hawa Tanzania Institute of Education watakavyoandika ndo hivyohivyo mtoto itabidi akomae anataka, hataki ni wao wameshaandika.

Nitataja mifano ya wachapishaji wa zamani (2008 kurudi nyuma) kabla kuja hii Taasisi ya Elimu Tanzania
Mture Educational Publishers
Educational Books Publishers
Oxford University Press (T) LTD
Macmillan (Aidan Publishers)
Ben and Company LTD
Wizara ya Elimu na Utamaduni

Kulikuwa na wengine kwajili ya shule za private mfano Adamson na Mwanzo Educational Publishers. Sijui na wao kwa sasa mwendo ni huu huu masikini (pamoja na sekondari). Yaani kama kwa mwendo huu ni hivi hivi mpaka advance dah mbona itakuwa tumeshikwa pabaya sana

Kwa upande wa Sekondari sikumbuki sana ila kuna jamaa kwa jina DT Msabila alikuwa na vitabu konki sana pamoja na "Institute" mbali na hao vitabu vingi tulikuwa TUNANYAMBALIKA tu. Hiyo institute sijui ilikuwa Institute of Education au vipi ila nachokumbuka tu ni kwamba kuna vitabu vya Biology tulikuwa tunaviita hivyo maana viliandikwa pale juu
View attachment 2032800View attachment 2032802View attachment 2032801View attachment 2032803View attachment 2032804View attachment 2032807View attachment 2032805View attachment 2032806View attachment 2032808View attachment 2032811View attachment 2032812View attachment 2032813View attachment 2032814
 
Back
Top Bottom