Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,504
- 911,249
Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM
Saturday, 22 January 2011 20:24
Waandishi wetu
SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya CCM kubariki kampuni ya Dowans kulipwa na serikali, wasomi, wanasiasa wa watu kada mbalimbali, wamelaani hatua hiyo na kusema chama hicho kimeasaliti Watanzania.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wananchi hao walisema tofauti ya msimamo kuhusu Dowans, kati ya CC na UVCCM, ni ishara tosha kuwa malipo hayo yana utata mkubwa na kwamba yanahitaji ufafanuzi wa kina kabla ya kutolewa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Dk Bashiru Ally alisema tafauti hiyo ya msimamo inaonyesha kuwa ndani CCM hakuna uelewano na kwamba malipo hayo yakifanyika chama hicho kitabanwa na wananchi.
Kimsingi nakubaliana na tamko la vijana wa CCM kuhusu Dowans pamoja na Bodi ya Mikopo ambayo tayari Rais Kikwete ameshaiundia kamati, lakini walichoamua Kamati Kuu ndio msimamo wa Serikali kwani zaidi ya asilimia sitini ya wajumbe wa mkutano huo ni mawaziri na mwenyekiti wao ni Rais, alisema Dk Ally.
Alisema ingawa deni hilo litalipwa, CCM ijiandae na hasira za wananchi ambazo zitakishukia chama hicho siku za usoni.
Dk Ally ambaye ni mtaalamu wa Sayansi ya Siasa alisema msuguano ulioonyeshwa na Kamati Kuu ya CCM, UVCCM na baadhi ya mawaziri katika sakata hilo, inaashiria hata kwenye kikao cha kamati hiyo wajumbe hawakuafikiana kuhusu hukumu hiyo.
Mfanyabiashara wa Arusha, Evance Mremi, alisema kitendo cha CCM kukubali kuilipa Dowans ni udanganyifu unaofanywa na watu wasiolitakia mema taifa.
Mremi alieleza kuwa kilichofanywa na CCM, kimekwenda kinyume na matarajio ya wananchi wengi na kwamba kitendo hicho kinaashiria kuwa nchi iko kwenye utawala wa kijeshi.
Watanzania hatupendi kulipa deni hilo linaloonekana wazi ni la udanganyifu, hawa wanaotulazimisha, wana maslahi nalo kwa kuwa hayo si matakwa ya Watanzania, alisema mfanyabiashara hiyu.
Mbeya
Mwenyekiti wa mstaafu wa CCM mkoani Mbeya, Allan Mwaigaga alisema kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM kuhusu suala la Dowansa ambao umezaa makundi mawili yanayopingana ambayo ni lile la viongozi na la wanachama.
Alifafanua kuwa kutokana na mgawanyiko huo, viongozi wa taifa hawasikilizi maoni ya wanachama wala wananchi kwa ujumla.
Viongozi wa chama taifa walikuwa na nafasi ya kushinikiza ili wamiliki halisi wa Dowans wafahamike, lakini matokeo yake wamebariki malipo hayo bila hilo kufanyika.
Ufike wakati tuwe na uzalendo na nchi yetu, chama ndicho kinachohubiri amani na upendo hivyo kinatakiwa kuilinda na viongozi kuwa wawazi na wa kweli kwa wanachama na wananchi wake, alisema.
Mwaigaga alisisitiza kuwa suala linalogusa wananchi linatakiwa kushughulikiwa kwa umakini badala ya kufanyiwa ubabaishaji kama masuala ya mchezo wa mpira wa miguu.
Naye mkazi wa Mwanjelwa, Zawadi John, alisema CCM ilipaswa kuwaelimisha wananchi kuhusu Dowans na siyo kutoa maamuzi.
Kilimanjaro
Mwanasiasa mkongwe, Peter Kisumo aliunga mkono msimamo huo uamuzi wa kusitisha malipo hayo hadi shauri lililowasilishwa mahakamani na wanaharakati litakapotolewa uamuzi.
Nimefurahishwa sana kwamba Kamati Kuu ilisema kwamba inangoja maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na raia mmoja na wanasema ingawa nchi ilikosea, lakini wanatambua kuna raia anapinga mahakamani hilo jambo,alisema Kisumo.
Kisumo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa maelezo ya Kamati kuu yako kiutu uzima zaidi kwamba mkataba wa Dowans ulisainiwa na Tanzania kama nchi na kama mahakama za kidunia zinasema nchi ilikosea, inaweza kujitetea.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi na wanachama wengine wa CCM wakiwamo wenye nyadhifa za juu wanauona msimamo huo wa Kamati Kuu ni sawa na CCM kujichimbia kaburi lake kwa kuwa imeshindwa kusoma alama za nyakati kabla ya kutoa tamko hilo.
Siamini kama Chiligati ndivyo alivyotumwa na wajumbe wa Kamati Kuu chini ya Rais Kikwete kusema hayo kwa sababu hakuna Mtanzania yeyote anayekubali malipo hayo yafanyike isipokuwa kikundi cha watu wachache, alidai kigogo mmoja wa CCM.
Mjumbe mmoja wa Kamati ya Siasa ya CCM wilayani Mwanga aliyeomba jina lake lihifadhiwe alisema anaamini yaliyotabiriwa kwamba huenda CCM ikafa mikononi mwa Kikwete ndicho kinachoweza kutokea mwaka 2015.
Wakati wa kampeni hapa tumepata tabu sana na suala la ufisadi, halafu leo Kamati Kuu inatuongezea mzigo mwingine wa kujieleza kwa wananchi kuhusu Dowans. Sielewi kama viongozi wetu wanaitakia mema CCM, alisema.
Mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa miongoni mwa wanaCCM wa kada ya kati, aliwataka viongozi wa kitaifa kutafakari kwa kina sababu za Watanzania kuichukia CCM kiasi cha kuonyesha hasira zao kwenye uchaguzi uliopita.
Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Mrema alisema hawezi kutoa maoni yake kwa sasa kwani kuna nyaraka muhimu za utafiti anazisubiria ndipo atoe msimamo wake juu ya Dowans.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) ambaye alikuwa mmoja wa wabunge wapambanaji wa ufisadi, alisema anachokiona ni kwamba chama chake kimekata mawasiliano na wananchi na hakijui hasira yao.
Mimi nadhani CCM wamekata mawasiliano na Wananchi wanaowaongoza kwa hiyo hawajui walivyo na hasira na Dowans, bora wangenyamaza tu wakaiacha serikali ikaacha isubiri hadi hiyo tuzo isajiliwe mahakamani, alisema Kimaro.
Kimaro ambaye ni mfanyabiashara mashuhuri nchini alisema kitendo cha chombo cha juu kama Kamati Kuu kujiingiza katika sakata la Dowans bila kueleza kwa kina nini kilitokea hadi wabariki malipo hayo ni sawa na kujitundika kitanzi.
Mimi naishauri CCM na serikali watembee vijijini wapiti kwenye vijiwe vyote si vya mkoa Kilimanjaro tu bali nchi nzima ndiyo wataona watu walivyo na hasira na Dowans kuliko hata shida walizonazo za kimaisha, alisema Kimaro.
Tanga
Rashid Mfaume, ambaye alijitambulisha kuwa ni muasisi wa CCM anayeishi jijini Tanga, alisema mtindo wa uendeshaji CCM hivi sasa ni hatari kwa kuwa kila mmoja ana uwezo wa kuzungumza analolitaka bila kusubiri mamlaka husika.
Umoja wa Vijana wa vijana wa CCM juzi walitoa maelezo yenye kupinga Dowans isilipwe hatujakaa sawa Kamati Kuu, inatoa msimamo ulio tofauti. Je, huu ni uendeshaji wa chama uliokuwa ukisimamiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere? alihoji Rashid.
Dotto Ali mkazi wa Manundu wilayani Korogwe alisema kabla ya UVCCM kutoa tamko la mambo nyeti kama ya Dowans hadharani, kulitakiwa kuwa na utaratibu mawasiliano na mkubwa wake ambaye ni CCM kujua msimamo wake badala ya kuwakaanganya wananchi.
Katibu wa TLP Mkoa wa Tanga, Rashid Amir,aliwapongeza vijana wa UVCCM kwa kuonyesha hadharani hisia zao juu ya kuchukia malipo ya Dowans na mikopo ya wanafunzi na kwamba wameonyesha kuwa na uchungu na nchi yao.
Vijana wa UVCCM wamevumilia hadi wamechoka wakaamua kutangaza msimamo wao kama watoto wa walala hoi. Vijana hao wameona jinsi jahazi linavyokwenda mrama, lakini bahati mbaya bado wakubwa zao CCM hawawajali wananchi,alisema Rashid.
Calistus Shekibaha aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Korogwe Mji kupitia Chadema aliwashauri vijana hao wa UVCCM kukihama chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani au waanzishe chama chao cha siasa ambacho kitakuwa na huruma kwa wananchi.
Alisema CCM haina utamaduni wa kusikiliza changamoto wala mawazo yaliyo tofauti na vigogo wake, hivyo hakuna haja kwa vijana wenye mwelekeo wa maendeleo kuendelea kubaki huko.
Hawa vijana wa UVCCM ni wanamapinduzi, wanauchungu na nchi yao,wanaona jinsi mambo yanavyokwenda kombo na kubwa zaidi waliona joto ya jiwe wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu uliopita hivyo wameamua kuwa
wakweli, alisema.
Arusha
Wakizungumza katika mahojiano maalum, Calist Lazaro, Jonathan Lymo na mratibu wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Arusha,(ANGONET), John Bayo, walisema, CCM itakuwa inajimaliza yenyewe kuunga mkono malipo ya Dowans.
Lazaro ambaye ni Kada wa CCM, alisema haiwezekani kampuni ya Dowans kulipwa kwani ilipewa kazi ya kufua umeme na kampuni hewa ambayo ilithibitishwa na Bunge la Tisa
"Kwanza hawa viongozi wangu waseme, tunamlipa nani na kwa nini, na kama kweli watalipa basi CCM inakufa," alisema Lazaro ambaye alikuwa mgombea wa udiwani Kata ya Sokoni kupitia CCM.
Lymo alisema, Kamati Kuu ya CCM, ilipaswa kuheshimu maoni ya wananchi walio wengi kwa kuonyesha kuchukizwa na kutaka kutumiwa vibaya fedha za umma.
Naye Bayo, alisema ANGONET, itasikitishwa kama Dowans ikilipwa kwani tayari ilithibitika mbia wake ni kampuni hewa na hivyo hata wao, uhalali wao una utata.
"Haya ni matumizi mabaya sana ya fedha za walalahoi, kutoa Sh94 bilioni kwa kampuni ya ujanja ujanja, ni aibu kwa taifa letu...sio busara kabisa kulipa," alisema Bayo.
Imeandaliwa na Burhani Yakub, Daniel Mjema, Musa Juma, Godfrey Nyangoro, Neema Myovela, na Brandy Nelson,