Wadaiwa bodi ya mikopo kitanzini. Kuanza kukatwa 15% kutoka kwenye mshahara

Niliikuwa najaribu kupata picha, kwa mtu anayeanza kazi kwa mshahara wa 500000 halafu akatwe 120000 ya bodi ya mikopo then abaki na 380000.Yaani graduate mzima alipwe hiyo. Ni nani atakayekuwa tayari kujipeleka. Mshahara hawajaongeza lakini makato wanataka wakate mapema. Hii ni kuwaweka watumishi waishi maisha magumu yale ya shetani yaliyoahidiwa.
 
Kabla ya kupandisha kutoka aslimia 8 kwenda 15 nilikuwa nalipa 163, 000 Tsh ikiwa asilimia 15 nitalipa kama 300, 000 Tsh, ukijumlisha na 150,000Tsh ya wife "bado hajapata kazi" so inabidi nimlipie kwa mwezi itakuwa ni kama 450,000tsh. Hii no hii
 
1479279835360.jpg
 
Mlivyoambiwa mnapaswa sasa kuishi kama mashetani hamkuelewa tu? Tunajenga "uchumi wa viwanda" and money counts a lot to us.
 
ye hawa jamaa ivi hakuna kitu kinachoweza wazuia jana nlinunua vocha ya 6000 niongee na jamaa nje ya nchi asee kwanza VAT ilikuwa ya ajabu zaid ya 800 tsh so ikabaki 5000 na point kathaa sasa tunaelekea wapi hata kama ni ukusanyaji wa mapato sio kihivi maisha yashakuwa mabaya
 
Dawa ya deni ni kulipa mlipoambiwa mchague El mkaambiwa watasamehe Madeni yote ya nyuma mkakataa msilalame acha tuisome Namba hakuna namna nyingine sasa tutaishi kama mashetani kama ilivyohaidiwa hahahahhaah kidding
 
Duuuh yaan bora mliosoma mapema maana hii ni hatari. Jamani lakini ikumbukwe hata wao wamepita kwenye hatua hizo Sasa mbona wanaumiza wenzao kiasi hiki?
Wewe lipa mkopo ndugu, kwani hukuambiwa kama ni mkopo.
Na kama uliona kulipa kazi basi usingekopa ungejilipia 100%.
Kumbuka umesoma kwa hela ya serikali ambayo ni kodi ya watanzania wote hata Mimi ambaye sijaenda chuo na sina mtoto au ndugu chuo kodi yangu imetumika kukupa maisha halafu unaleta longo longo
Hutaki wenzio nao wafaidike..?
 
Back
Top Bottom