Wadada watumishi wasio na ndoa hivi mna nini?

Wadada watumishi wasio na ndoa hivi mna nini?

Maisha hayana formula waache wachague maisha wanayoyapenda wao.
 
Wanawake wengi wanapenda wanaume walio na kila kitu waliofanikiwa hawataki ku"hustle" pamoja na mwanaume waje kufanikiwa pamoja wao hawataki kupata shida hata kidogo ndio maana hawatulii kila sehemu anachezewa anatupwa kule na huku miaka inaenda akija kustuka kashakuwa kibibi kwenye kioo hajiangalii mara mbili mbili kama zamani
 
Kuna kaka nilifanya nae kazi mwenyeji wa Bukoba (Mhaya). Alinieleza alipomaliza shule, post yake ya kwanza ilikuwa DSM. Hakumfahamu mtu yeyote Dar, aliishi guest mpaka akapata chumba, alianza kununua vitu vidogovidogo. Kanisani alikutana na binti wa nyumbani, roho yake ilimpenda sana. Walianza mawasiliano, alimtamkia binti nia yake, siku aliyomkaribisha binti nyumbani, binti alimuuliza kwa dharau sana, yaani unanioa unilete kwenye chumba?

Toka pale mawasiliano yao yalikufa. Ile hali ilimpa ari kaka ya kuanza kuuliza bei ya kiwanja, alinunua kiwanja akajenga. Alikwenda nyumbani likizo akapata mchumba kule baada ya kufunga ndoa alimleta mke DSM. Kazini mambo yalikaa vizuri alinunua kiwanja cha pili. Akalijenga nyumba ya kupangisha. Alipoanza kutafuta mpangaji, huwezi kuamini alipigiwa simu na yule dada mchumba wa kwanza anatafuta nyumba. Jibu unalo mwenyewe uso wa dada ulikuwaje.
....kisa kizuri japo mi jibu sina.
......weka picha nigelezee!
 
Hahahaaa kuna ka ukweli fulani, ukishaona drama kwa mwanamke basi ujue wewe sumio type yake.
daaah.... Hii ni kweli kabisa yan.
Afu wengi wanataka mwanaume wamkute ndani kuna seti ya sofa , kitanda safi , flat screen, n.k. Wakikuta ndani kwako kuna kiti kimoja cha plastic na meza ya plastic na mziki ni pc yako ulotoka nayo chuo na vispika vyake ndo utaskia izo drama .....ooh nishamtambulisha kwetu ........
 
Si kila binti ataolewa na ndo maana wako wengi sana
Wengine wapo kupendezesha dunia
Wengine wapo kuhudumia jamii
Wengine wapo kwa ajili ya biashara
 
m
Mimi kazini kwetu kuna wadada kama watano hivi wanaishi kwa hizo drama. Wanaishi kwa ndoto za kuolewa na wafanyakazi wa bank, TRA n.k huku wakitukataa walimu wenzao. Sasa na sisi tumeamua kuachana nao huku tukiamini baada ya muda mfupi tutawaita single mums
mm ni mwalimu natarajia kuoa mwanajeshi,hapo nakubaliana na hiyo issue kweli IPO kwa wengi,wapo wachache sn wenye kujua maisha ni nini
 
sasa wenye ndoa na machozi kila siku hawana stress. Unachovalue wewe sio kila mtu anavalue. jiamini ishi maisha ya kujiamini sio kusukumwa na hisia za watu. Yawezekana unafikria wanastress we ndo unazo zinakutafuna kwa sababu ya kuwa mfungwa wa mawazo yako.

Yawezekana wamekukataa una kiwango tafuta viwango kwanza acha kulumbana na watu
Ni sawa tumekataliwa lakini kwa sababu ambazo zisizo na mashiko hasa kwa mtu ambaye ni msomi. Kwa nini umkatae mtu kisa kazi yake haina kipato kikubwa mfano mwalimu wakati ana elimu ya kutosha tu.
 
Maisha ya sasa ni mbwa kala mbwa.

Hakuna formula.
 
Back
Top Bottom