Wadada/wanawake mtanisamehe kidogo kwa hili.

Wadada/wanawake mtanisamehe kidogo kwa hili.

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
Simkashifu mtu ni ujumbe tu, pia amepata kusema mdau wa masuala ya wanawake
(Lu-Patie!).

"Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao!"
........................................

Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi wa kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto wa kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja, anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu a.k.a mshamba.

Una mpuuza Na kumdharau mtu eti kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira, ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu ambae ni baba fulani na ni mume wa Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa.
Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanawake?

Umegombana Mara ngapi na Huyo HB wako kisa usaliti na bado upo nae??
Wanaume wangapi wenye pesa mvuto na kila kitu ndani lakini wamekutumia na kukuacha?
Lakini bado hujifunzi aina ya mwanaume wa kuwa nae?

Acha kujidharau u mrembo onesha kwamba unajipenda kuanzia MAVAZI NA KAULI !
Achana na marafiki washenzi wasio na mchango wowote kwenye maisha yako zaidi ya kukuharibia mwelekeo wako kwa ushauri mbaya wanaokupa,

Ni marafiki zako au ndugu zako wangapi waliolewa na wanaume wa kawaida lakin Leo wana mafanikio?
Kwa nini usiwaige wao? kwanini unaiga maisha ya watu maarufu nakuishi maisha ambayo sio yako?..
Weka uzuri pembeni simama imara kama MKE na MAMA bora wa kesho.
Mtie moyo mmeo, mchumba wako ajisifu kuwa Na wewe, si kila mara dharau Na kumbeza!!

Kifupi hakuna mwanaume anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya au kupata, Encouragement matters most kwa wanaume wengi!
 
Hakika neno moja lafaa sana kwa mwenye hekima na busara kumwezesha kung'amua mema na mabaya so big up chief
 
Kwahiyo wasubilia waje! Haya endelea kusubilia

Hujambo lakini
hahaha yaani nianze kuwasubiri kabisaa !!! nime mu Alert mtoa mada ili ajiandae kumwagiwa shombo ... mimi siwezi acha kulala na kuwasubiri wao ...

mimi mzima kabisa hofu kwako .. mrembo
 
hahaha yaani nianze kuwasubiri kabisaa !!! nime mu Alert mtoa mada ili ajiandae kumwagiwa shombo ... mimi siwezi acha kulala na kuwasubiri wao ...

mimi mzima kabisa hofu kwako .. mrembo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nilizani nawe unawasubilia, ila watakuja tu,

Mie sijambo kabisa
 
Huu tushausoma sana humu, asante kwa kuwakumbusha
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nilizani nawe unawasubilia, ila watakuja tu,

Mie sijambo kabisa
hahaa vyema sana" kama haujambo nafurahi kusikia hivyo ..

watakuja ndio na dose yake Ataipata
 
Kila mtu ana life style yake aliyoichagua so usimpangie mtu maisha ya kuishi, unaweza olewa na mwanaume kapuku leo mkasaidizana kuzisaka pesa ila baada ya kuzipata asikuone tena wa maana akawaona wa maana hao wadangaji na kuzifuja huko
 
Back
Top Bottom