Wadada wanavyojiweka mbali na ndoa

Wadada wanavyojiweka mbali na ndoa

Uta
Kama mnavyojua wakuu kwamba mwanaume kila siku ni muwindaji na hasa akiwa hana ndoa. Hapa simaanishi kuwinda swala bila shaka naeleweka vyema!
Basi bwana....
Wiki iliyopita nikiwa kwenye mishe mishe za kutafuta mkate wa kila siku nikajikuta nipo kwenye usafiri wa uma naelekea kijichi.
Wakati wa kurudi kwenye gari nilikaa siti moja na binti mmoja, kwa kumwangalia alikua na umri wa miaka 20/22 hivi. Basi hapo ndipo bandiko hili lilipozaliwa.
Mimi ni muumini sana wa mavazi ya kusitiri kwa wadada, na kiukweli nimekua nikiwaamini sana na kuwachukulia kuwa ni wastaarabu wanawake wa aina hiyo ya mavazi. Gauni au sketi ndefu, mtandio n.k
Nikajiingeza nikapata namba. Kilichofuata na stori za hapa na pale, kutakiana hali na ahadi za kuonana. Sikua na haraka. Alinivutia sana na kwa muda mchache nikajiona nipo karibu sana na suala la kuuaga ukapela. Nilijidanganya!
Katika kumshawishi shawishi ili japo akubali tukutane siku moja akakubali, nikasema yes! Kaingia. Tukapanga siku ya kukutana ili tuweze kuongea zaidi. Siku zilipokaribia kuna kuna siku akaniambia kuwa kwa sbb hana kazi suala la nauli huwa linaweza kuwa changamoto kwake kwa hiyo siku ikifika akiomba nauli kama nitaweza kumtumia hata elfu 3 ya nauli atashukuru, nikasema usijali siku hiyo hiyo nikatuma elfu kumi. Sikutaka kumpoteza.
Hapo ndipo nilijua rangi zake. Akawa anachelewa kupokea simu, mara yuko busy na hatimae akawa hapokei kabisa simu.
Baada ya tukio lile nimeona kuwa wanauma tuna mitihani sana katika kufikia kupata wanawake wa maisha yetu.
Ile pesa haukuniuma sana bali niliumia kumpoteza yule binti na zaidi naumia kuona kuwa sisi wanaume tuna mtihani mkubwa katika kutimiza hili lengo.
Kwa waliofanikiwa kila la kheri.
Duh, kumbe bado uko nyuma Mkuu hujui aina hii mpya ya utapeli wa wadada wa mjini! Shtuka hatutumagi tena nauli bali aje na nauli yake mambo mengine yafuate
 
Kusema ukweli wanawake wa kuoa ni kuanzia miaka 28. Huyu anakua kuna umbwe flani kashalipata na anakua anataka ndoa kweli sio kwenda kujaribu
 
Pole sana rfk, hizo style ulizotumia kupiga verse nadhani si rahisi kumpata msichana, na pesa ukatuma haraka haraka.Next time hata kama una hamu ya kuoa basi usionyesha kuwa na haraka sana, kuomba appointment siku hiyo hiyo na baadaye kutuma pesa,yeye kaomba 3000/- wew ukatuma 10,000/-,kupata number hiyo ilikuwa ni hatua kubwa ya kwanza ili angalau usome mienendo yake kupitia mawasiliano kabla ya kukutana rasmi.
 
Kama mnavyojua wakuu kwamba mwanaume kila siku ni muwindaji na hasa akiwa hana ndoa. Hapa simaanishi kuwinda swala bila shaka naeleweka vyema!
Basi bwana....
Wiki iliyopita nikiwa kwenye mishe mishe za kutafuta mkate wa kila siku nikajikuta nipo kwenye usafiri wa uma naelekea kijichi.
Wakati wa kurudi kwenye gari nilikaa siti moja na binti mmoja, kwa kumwangalia alikua na umri wa miaka 20/22 hivi. Basi hapo ndipo bandiko hili lilipozaliwa.
Mimi ni muumini sana wa mavazi ya kusitiri kwa wadada, na kiukweli nimekua nikiwaamini sana na kuwachukulia kuwa ni wastaarabu wanawake wa aina hiyo ya mavazi. Gauni au sketi ndefu, mtandio n.k
Nikajiingeza nikapata namba. Kilichofuata na stori za hapa na pale, kutakiana hali na ahadi za kuonana. Sikua na haraka. Alinivutia sana na kwa muda mchache nikajiona nipo karibu sana na suala la kuuaga ukapela. Nilijidanganya!
Katika kumshawishi shawishi ili japo akubali tukutane siku moja akakubali, nikasema yes! Kaingia. Tukapanga siku ya kukutana ili tuweze kuongea zaidi. Siku zilipokaribia kuna kuna siku akaniambia kuwa kwa sbb hana kazi suala la nauli huwa linaweza kuwa changamoto kwake kwa hiyo siku ikifika akiomba nauli kama nitaweza kumtumia hata elfu 3 ya nauli atashukuru, nikasema usijali siku hiyo hiyo nikatuma elfu kumi. Sikutaka kumpoteza.
Hapo ndipo nilijua rangi zake. Akawa anachelewa kupokea simu, mara yuko busy na hatimae akawa hapokei kabisa simu.
Baada ya tukio lile nimeona kuwa wanauma tuna mitihani sana katika kufikia kupata wanawake wa maisha yetu.
Ile pesa haukuniuma sana bali niliumia kumpoteza yule binti na zaidi naumia kuona kuwa sisi wanaume tuna mtihani mkubwa katika kutimiza hili lengo.
Kwa waliofanikiwa kila la kheri.
Mkuu kuliko utume nauli bora umfuate.Ndio upendo wa dhati
 
Sema ukweli hela ndo imekuuma
 
Nilishazirudisha nyingi sana hizo

Ni hivi nilikuwa nikituma nauli nakupigia kukusikilizia

Ukianza story sijui mama ake mama kaja

Sijui baba karudi katapi

Mimi faster huduma kwa wateja tigo wairudishe nilikuwa narudisha mpaka mkono

Halafu namtumia txt ya kum-mind nilikuwa naoga matusi ila pes imerudi
 
Mi nilishawahi kufahamiana na mtu siku mbili tu, siku ya tatu ananiomba elfu 30 ya saluni.....nikatoka ndukii sikugeuka nyuma tena
 
Back
Top Bottom