mr vata
JF-Expert Member
- Jan 30, 2017
- 465
- 617
Kama mnavyojua wakuu kwamba mwanaume kila siku ni muwindaji na hasa akiwa hana ndoa. Hapa simaanishi kuwinda swala bila shaka naeleweka vyema!
Basi bwana....
Wiki iliyopita nikiwa kwenye mishe mishe za kutafuta mkate wa kila siku nikajikuta nipo kwenye usafiri wa uma naelekea kijichi.
Wakati wa kurudi kwenye gari nilikaa siti moja na binti mmoja, kwa kumwangalia alikua na umri wa miaka 20/22 hivi. Basi hapo ndipo bandiko hili lilipozaliwa.
Mimi ni muumini sana wa mavazi ya kusitiri kwa wadada, na kiukweli nimekua nikiwaamini sana na kuwachukulia kuwa ni wastaarabu wanawake wa aina hiyo ya mavazi. Gauni au sketi ndefu, mtandio n.k
Nikajiingeza nikapata namba. Kilichofuata na stori za hapa na pale, kutakiana hali na ahadi za kuonana. Sikua na haraka. Alinivutia sana na kwa muda mchache nikajiona nipo karibu sana na suala la kuuaga ukapela. Nilijidanganya!
Katika kumshawishi shawishi ili japo akubali tukutane siku moja akakubali, nikasema yes! Kaingia. Tukapanga siku ya kukutana ili tuweze kuongea zaidi. Siku zilipokaribia kuna kuna siku akaniambia kuwa kwa sbb hana kazi suala la nauli huwa linaweza kuwa changamoto kwake kwa hiyo siku ikifika akiomba nauli kama nitaweza kumtumia hata elfu 3 ya nauli atashukuru, nikasema usijali siku hiyo hiyo nikatuma elfu kumi. Sikutaka kumpoteza.
Hapo ndipo nilijua rangi zake. Akawa anachelewa kupokea simu, mara yuko busy na hatimae akawa hapokei kabisa simu.
Baada ya tukio lile nimeona kuwa wanauma tuna mitihani sana katika kufikia kupata wanawake wa maisha yetu.
Ile pesa haukuniuma sana bali niliumia kumpoteza yule binti na zaidi naumia kuona kuwa sisi wanaume tuna mtihani mkubwa katika kutimiza hili lengo.
Kwa waliofanikiwa kila la kheri.