Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,474
- 40,473
Ndoa sio ya kila mtu, ndio maana wengine wanazeeka wakiwa singo.
kwa kutumia uzi huu, kwa wale wadada wanaotaka kuolewa inabidi wajitathmini kama hizi sifa wanazo, kama hawana wajitahidi kujifunza kabla jua halijazama.
Sifa zenyewe ni hizi hapa:-
kwa kutumia uzi huu, kwa wale wadada wanaotaka kuolewa inabidi wajitathmini kama hizi sifa wanazo, kama hawana wajitahidi kujifunza kabla jua halijazama.
Sifa zenyewe ni hizi hapa:-
- Asiwe na marafiki wengi; marafiki wengi huwa ni vimeo, ukiwaomba ushauri watakupoteza kwa kufikiria ujana; wanaweza kukushauri uwe unamnyima mpenzi wako mtarajiwa tendo la ndoa na ukifuata ushauri wao, unapotea mazima.
- Awe anapenda kupika kuliko kununua nuna vyakula tayari ambavyo vimepikwa mfano chipsi, nyama choma n.k
- Awe na uwezo wa kutafsiri kesho kuliko sasa
- Awe anapenda kufanya shughuli za nyumbani, kama kupika pika, kufua, kufanya usafi n.k bila kutegemea kutumia kijana wa kazi
- Awe na sifa ya kupenda kufunga kanga akiwa nyumbani
- Akitembelewa haruhusu mgeni wake kuondoka bila kula chakula chake alichopika
- Akimtembelea mpenzi wake wa kiume anapoishi atajitahidi kumfanyia usafi wa nyumba, kufua, kukupikia n.k
- Akiwa na mpenzi wake muda wote wanakuwa na furaha, na anakuwa sio mjuaji wa maneno mengi.
- Aombi ombi hela hovyo, ukimuambia sina atakuvumilia, na wakati mwingine atakushauri tufanye hili au lile ili tupate hela.
- Anakuwa na mawazo ya kubana matumizi ili mfanye mambo ya maana.
- Anapenda kushiriki ibada katika dini yake
Kama yupo humu mwenye hizo sifa na amefikisha miaka 40 hajaolewa, anyooshe mkono juu tumshauri cha kufanya.