Wadada tutete kidogo

Wadada tutete kidogo

Unakuta unawaza mpaka unazimia kununua vitu vya gharama sio nzuri sana ila sio mbaya ili ujiweke safi ila nani mbaya sana kama ni kila saaa ni manunuzi yasio na msingi.
Ila humu watu huwaona wenzao ni malaya laiti wangejua maisha yao halisi wangetokwa na machozi ila humu watu hujiona hujudge kila mtu ila hawajui kitu kimoja shida sio ya kila siku.
 
Aisee, ahsante kwa kutushtua kutoka usingizini, tumeamka sana ,tutapiga kazi. Handbags 20?? Hayo ni matumizi mabaya sasa
Kuna mmoja juzi nimeona kwake kwenye corridor ameweka shelf ya kama 3×2M imejaa viatu kila aina, hand bag ukiangalia alipozitundika unaweza anzisha duka la mabegi!!!! Nilimwambia haya ni matumizi mabaya ya hela zako akachukia. Wadada mna kazi sana.
 
Umeanza kazi mjini mwaka wa tatu unaishi kwenye chumba na sebule. Chumbani una dressing table ina perfume kama zote kuanzia Coco Channel, Christian Dior, Estée Lauder nk, make up za MAC na Iman,

Handbags 20+ kuanzia Michael Kors, Calvin Klain, DKNY ec. Viatu pair 20+ kuanzia high heels, sandals, flats

Ni muumini wa da Mange kuwa utapata mwanaume mwenye pesa, anaejenga ghorofa Bagamoyo.

Unahitaji maombi uamke kutoka kwenye huo usingizi.

Hii ni thread kwa ajili ya "ke" tu, huo ni ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia.🤣🤣

Pia Weka na thread kwa ajili ya "me".
 
Muhimu ni kufanya kitu kinachokupa furaha. Tatizo tumezoeshwa kufuata vitu ambavyo Jamii inataka. Kimojawapo ni kujenga,yaani kujenga imekuwa kielelezo cha mafanikio kwenye maisha.
 
Kuna mmoja juzi nimeona kwake kwenye corridor ameweka shelf ya kama 3×2M imejaa viatu kila aina, hand bag ukiangalia alipozitundika unaweza anzisha duka la mabegi!!!! Nilimwambia haya ni matumizi mabaya ya hela zako akachukia. Wadada mna kazi sana.
Amechukia kwasababu hela ni zake,anatumia apendavyo iweje wewe umwambie ni matumizi mabaya ya pesa zake?
 
Muhimu ni kufanya kitu kinachokupa furaha. Tatizo tumezoeshwa kufuata vitu ambavyo Jamii inataka. Kimojawapo ni kujenga,yaani kujenga imekuwa kielelezo cha mafanikio kwenye maisha.
Wewe huoni threads humu watu waliokwama wanauza nyumba zao? Kimfaacho mtu chake
 
Back
Top Bottom