Wadada msikubali kurubuniwa

Wadada msikubali kurubuniwa

Na ukijafanya mwema kwa kutoa ushauri wa kidwanzi mbususu utaisikia redioni.
 
Sina mengi ya kusema

Dada zangu mliokomaa hivi majuzi na kufikia hatua ya kuwa watu wazima nawaombeni Sana mjitunze msijihusishe na mapenzi yasiyokuwa na umuhimu wowote.Hakuna madhara yoyote utakayoyapata Kwa kujitunza.

Wengi wenu hamjaolewa sababu ya kutojitunza na kutochukua maamuzi sahihi katika maisha yenu.

Dada zangu Kwa yeyote atakayesema anakupenda Fanya zoezi la kumnyima penzi mpaka utakapoona unafunga harusi na yeye.Siku hiyo baada ya kukiri atakupenda Kwa raha na shida ndiyo umuachie.

Usidanganyike na vizawadi zawadi vya hapa na pale na maneno ya uongo sababu mwisho wa siku atakutumia na mwisho atakapomaliza haja zake atakuona takataka.

Wanaume wasio na nia na wewe na wenye mihemko na tamaa watashindwa hii ligi mapema sababu walifuata kitu kimoja tu kwako na ukitoa hicho kitu hawakupendi Tena.Jifunzeni kutofautisha tamaa na mapenzi.Wanaume wengi wamejaa tamaa.

Pia kitu kikiwa kigumu kupatikana kinakuwa Cha thamani Sana.Jifunzeni Toka Kwa wanawake wa kale.Miili Yao yote ilikuwa Ina dhamani Sana sababu walikuwa wanavaa nguo za kujisitiri na hawadangi ovyo ovyo.

Maamuzi sahihi mengi huja na malalamiko kutoka Kwa watu, watu watakuchukia,watakusema vibaya, mwanaume ataona humpendi, lakini hapo ndipo yalipo matokeo mazuri ambapo utachuja katika ya kondoo na mbuzi waliovaa ngozi ya kondoo.

NB; ONYO WADADA MKITAKA KUFANIKIWA KATIKA HILI MSIPOKEE KABISA PESA ZA MWANAUME AMBAYE HAJATOA MAHARI KABISA KWENU.NA AKISHATOA MAHARI KATAA PESA ZOZOTE ATAKAZOTAKA KUKUPA MPAKA ATAKOPOKUOA RASMI AKAKUFANYA UWE MKE KUEPUKA HUU MTEGO.
Bora utafute pesa uwe na uhakika wa Maisha ndio uwe na nafasi ya kuchagua au kukataa mwanaume maana wengi ni Washenzi.

Lakini Ukiwa unataka Mwanaume Kwa njaa na Kwa sababu za ubinafamh uko kwenye risk mara 2.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom