Samboko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2011
- 5,421
- 7,877
Habari ya weekend wana jf,
Tangu nikiwa mdogo kijijini hukoo nilikua najiwazia siku nikipata ela nitanunua gari kwanza, wala sio nyumba, nilitamani siku moja na mimi niende na gari kijijini naendesha mwenyewe, maana nilikua naona wivu sana baadhi ya majirani zetu wakija na magari yao kule,
Nikaja mjini kutafuta baada ya miaka kadhaa ya kutafuta nikaweza kununua gari,
Sasa hapo ndio nikajua wadada wanapenda wanaume wenye magari, hata waliokua hawanisalimii wakawa na heshima, hakuna kutongoza tena gari tayari ni kitongozeo tosha na vituko vingivingi hivi kwao.
Sasa huyu wa juzi j5 ndio kaniacha hoi,
Nimetoka zangu kkoo jioni nipo kwenye daladala nikakaa na dada mmoja baada ya stori za hapa na pale nikaomba namba akanipa nikamtext palepale tushuke wote nna maongezi nae, akajibu sawa.
Tukashuka wote pale africa sana nikashangaa mwenzangu huyooo anatokomea zake nikamfuata kwa nyuma akawa anaongeza mwendo ili nisimfikie na njia aliyokua anaelekea na mimi naelekea hukohuko, nikafika kwa dada nkaingia ndani nkachukua funguo za gari nililokua nimemwachia tangu j2, kutoka nje nikawasha gari kuangalia mbele yule dada anarudi kumbe alikua ananikimbia mimi,
Nkamfuata kumfikia nikapunguza mwendo nikamuuliza ulikua unanikimbia nini? Akasema hapana, nkamwambia ingia kwenye gari akaingia, nikamuuliza nyumbani kwao wapi nimpeleke akaniambia nikampeleka hadi kwao wala sikumsemesha tena chochote nikaondoka,
Jana jioni kanitumia sms "mambo, ushaondoka kkoo?" mi wala sikumjibu,
Nikabaki najiuliza tuu, kuona gari urafiki uendelee akasahau alinikimbia pale kituo cha daladala.