wadada hawa kweli wataoleka...?

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,259
117
Habari JF!
Wanajamvi msaidieni hiyu ndugu yetu!
Amenieleza kwa urefu shida yake kuhusu dada mmoja ambae anachukua degree yake chuo kimoja humu Tanzania.
Mambo yao yalikua kama hivi:
Dada alimthibitishia lazima ataolewa nae kwa kua hana jamaa mwengine kwa muda huo. Hivyo alimuonesha dhahir shahiri kua yupo nae karibu kwa muda wowote. Hali hiyo ilimfanya jamaa ajihakikishie amepata mwenza wake.
Sasa ikatokea dada akasafiri kwenda mkoa mwingine. Hapo ndipo mashaka kwa jamaa yalipomuanzia...ikawa akipiga simu haipatikani,sms akituma hazijibiwi...hata ule ukaribu ulokuepo umekua hakuna.
Jamaa akaona amueleze ukweli kua yeye na huyo binti iwe mwisho lakin binti hakukubali...akamjibu asiwe na hasira.
Lakini mambo ndio hayo hayo...na hapo mwanzo jamaa alikua anahudumia gharama za hapa na pale...sasa jamaa amemshitukia hata ile misaada amezuia ..anahofu isiwe anakamuliwa huku mwenye mali rasmi yupo.
Je amvumilie huyo dada au aachane nae.
Nawakilisha kwenu. Tupate mawazo yenu!
 
kuna kitu kinaitwa intuition.....

wanasema follow ur ow intuition.....

mpenzi ni kama nyumba hivi au kiatu,
wewe unaevaa kiatu au kuishi kwenye nyumba ndo unajua hasa ni vipi...
 
Mwambie aongee nae amwambie hatoweza kuvumilia kama mambo yataendelea hivyo.
 
Hiyo Title imenichanganya.

Wadada wangapi??

Ushauri mwambie huyo rafiki yako aongee na mwenzake ajue shida iko wapi na kama hatakiwa aambiwe kuliko kupoteza muda.
 
Hawa wasichana wa kuwatongoza wakiwa chuo kwa ajili ya kuoa ni hatari tupu, nadhani tabia za wasichana wa chuo tulishawajadili hapa JF. Ni vizuri wasichana wa chuo uwasubiri wamalize chuo/watoke mazingira ya chuo ndipo uwaambia habari ya uchumba na ndoa. Chuo maisha ni ya ushenzi sana lakini akitoka chuo ndipo akili zao huwa zinaanza angalau kutafakari kibinadamu na hapo ukipeleka ombi la ndoa atakalokujibu atakuwa amelitafakari kiutu uzima kwa kiasi chake
 
Hiyo Title imenichanganya.

Wadada wangapi??

Ushauri mwambie huyo rafiki yako aongee na mwenzake ajue shida iko wapi na kama hatakiwa aambiwe kuliko kupoteza muda.
Pole kama umeona inakuchanganya!
Wapo wa dada wengi wenye tabia kama za huyo dada!
Naamin huyo dada si wakwanza!Lol.
 
haiharibu. Kwanini aishi kwa kubahatisha? Aongee nae ajue moja. Maisha yenyewe mafupi. Sio vizuri kupotezeana muda.
Halafu mara nyingi nawasikia akina dada wakisema ''umenipotezea muda wangu'' lakini akina kaka sijawahi kuwasikia maneno hayo.
Kupotezewa muda Husninyo ndio vipi?
 
Hawa wasichana wa kuwatongoza wakiwa chuo kwa ajili ya kuoa ni hatari tupu, nadhani tabia za wasichana wa chuo tulishawajadili hapa JF. Ni vizuri wasichana wa chuo uwasubiri wamalize chuo/watoke mazingira ya chuo ndipo uwaambia habari ya uchumba na ndoa. Chuo maisha ni ya ushenzi sana lakini akitoka chuo ndipo akili zao huwa zinaanza angalau kutafakari kibinadamu na hapo ukipeleka ombi la ndoa atakalokujibu atakuwa amelitafakari kiutu uzima kwa kiasi chake
Kweli hapo umenena!.
 
Alikuwa anamtumia huyo jamaa sababu alikuwa chuoni matumizi ya hapa na pale na yale mashindano ya wasichana chuoni. kwa sasa karudi kwa mpenzi wake anaempenda. hiyo ndio goodbye.
 
Nafikiri jambo liko wazi kuwa jamaa alikuwa anatumiwa. Unajua utu uzima dawa na akufukuzae hakwambii toka ila utaona mambo yanabadilika. Unajua nonverbal communication speaks louder than verbal. Huyo binti hata kama utamuhonga mbingu itakuwa bure. Chapa lapa tafuta mwingine
 
kupotezewa muda ni pale ambapo wewe unafikiria future zaidi wakati mwenzio hana hiyo habari kwamba atakuwa na wewe kimaisha.
Umeelewa au unahitaji darasa zaidi?
Nahtaj darsa zaidi.
Kwann iwe kwa akina dada peke yao?
 
Alikuwa anamtumia huyo jamaa sababu alikuwa chuoni matumizi ya hapa na pale na yale mashindano ya wasichana chuoni. kwa sasa karudi kwa mpenzi wake anaempenda. hiyo ndio goodbye.
Mhh!
Mambo hayo!.
 
Nafikiri jambo liko wazi kuwa jamaa alikuwa anatumiwa. Unajua utu uzima dawa na akufukuzae hakwambii toka ila utaona mambo yanabadilika. Unajua nonverbal communication speaks louder than verbal. Huyo binti hata kama utamuhonga mbingu itakuwa bure. Chapa lapa tafuta mwingine
Mh!.
Jamani hivi huyo dada hawezi kubadilika?
Labda anampima tu!.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom