Wachungaji wa kilokole hawana umoja kabisa

Wachungaji wa kilokole hawana umoja kabisa

Umoja wa nini sasa,?? Ni Mungu aliyeahidi kwa kusema "Nitakuwa nawe wakati wa taabu" hakusema wakati wa taabu utakuwa na wachungaji wenzako. Mambo ya Umoja wa namna hiyo ni huko katoliki, sisi hatuna desturi kama hizo. Pengo angepooza mngembeba mzobe mzobe Queens hospital Washington, sisi tunakuacha usimame kwa imani yako

duh! hii ya kwako kali ya mwaka
 
duh! hii ya kwako kali ya mwaka
ila kusema ukweli, jamaa wamemtosa sana. hata kwenda kupooza kwa kova na picha kwa ahadi kwamba wataenda kumuonya jamaa asirudie tena, wao wamemwacha anagaragazwa peke yake.hahahha.
 
kusajili kanisa ni takwa la kisheria kila mtu analijua takwa hilo, sasa kama hakusajili wachungaji wenzake wamsaidiaaje ?
 
YAANI just kwa kuangalia sakata la gwajima, na inavyosemekana leo ameambiwa aende akalete hati ya usajili wa kanisa lake, hiyo wanamfanyia psychological torture mbaya sana na wanataka kumpoteza mapema kabisa afe kabisa.

Ajabu yake ni kwamba, wachungaji wenzie wa makanisa ya kilokole na hayo sijui ya CCT na mengine sijui majina, hawana umoja kabisa wamemwacha gwajima anapambana peke yake wakati wakiwa kwenye mikutano yao hiyo walikuwa wote pamoja.

Hata Arusha walikuwa wote pamoja lakini hapo wamemwacha peke yake apambane peke yake. nilichokuwa nategemea ni kwamba hawa wachungaji wangejaribu ku reconcile na serikali ili suala hili liishe kwa amani kwasababu hakuna ubishi kwamba wakristo wengine tunahisi kuwa christianity is being attacked here, na wengi wetu tumeshasali sana pale kwa gwajima na serikali tunaona inatuumiza mioyo.

Ninajua hata kama hawatasema chochote lakini kitakachotokea kwenye kura mwaka huu itakuwa siri ya CCM.

Pengine suala hili ni mpango wa Mungu ili walokole wote wapige kura upinzani kwasababu ukristo unanyanyaswa hapa, walokole tunanyanyaswa.
umoja wao hauonekani ila wewe subili wamunyang'anye hati ya usajili harafu tuone kama CCM itabaki salama
 
ila kusema ukweli, jamaa wamemtosa sana. hata kwenda kupooza kwa kova na picha kwa ahadi kwamba wataenda kumuonya jamaa asirudie tena, wao wamemwacha anagaragazwa peke yake.hahahha.

wenyew pia huwa wanawivu ndio maana wanamuangalia tu kuona nguvu yake itaishia wap!!
 
Kwa matusi yale, huyu mchungaji nahisi akiwa mdogo alipatwa na Malnutrition ambayo ikamsababishia Mental Retardation And Over Secreation Of Matusi Hormones.
 
Wachungaji wawe na umoja kwa lipi ndugu? Umoja wa kushabikia matusi ya gwajima aliyomtukana pengo? Wachungaji wangekuwa na umoja kwenye hili la gwajima sio tu waumin wangewashangaa bali hata roho mtakatifu angewaacha. Wanatakiwa kwa umoja wao walaan matus aliyotukana gwajima.
 
ameambiwa aende lini tena polisi? hivi ccm wana under estimate walokole ehee, mbona wanakuwa biased against them sana au kwasababu wanatandika na kuchoma moto mahirizi yao na waganga wao katika ulimwengu wa roho?
 
kusajili kanisa ni takwa la kisheria kila mtu analijua takwa hilo, sasa kama hakusajili wachungaji wenzake wamsaidiaaje ?

Unaweza kukuta na hao wengine hawakusajili sasa wamekimbilia kwenda kusajili yao.
 
wachungaji wameshaanza kuhubiri kimyakimya waumini waikatae ccm jumla. pitia kwenye makanisa jumapili usikie mwenyewe. hakuna mlokole Tanzania aliyefurahi unyanyasaji anaofanyiwa gwajima utafikiri ameua mtu? kumbe ni maneno tu amerushiana na askofu mwenzie na hakuna gasia yeyote kati ya wakatiliki na walokole iliyotokana na maneno hayo, sasa polisi ndio hayo maneno yamewauma sana? hata pengo mwenyewe hayajamuuma ila polisi? au walikuwa wanamsubiria aingie kwenye anga zao, ccm inavizia sana walokole wakati wameshaenda sana pale kuomba kura.

Nape nauwe ameshaenda pale kwa gwajima, lowasa ameenda pale, sita ameenda pale, mwakyembe ameenda pale.....kumbe wanajifanya rafiki ili wamvizie kwenye kosa wammalize kabisa. mkimmaliza gwajima waumini wake bado wapo. mtammaliza mtu lakini imani ya watu itabaki palepale.
 
Kwa matusi yale, huyu mchungaji nahisi akiwa mdogo alipatwa na Malnutrition ambayo ikamsababishia Mental Retardation And Over Secreation Of Matusi Hormones.

AISEEE!!! Ngoja akusikie akakuhubiri kanisani kwake kama hajakuweka msukule kabisaa
 
Mtoa mada akili yako haina umoja na siyo Watumishi wa Mungu Mosi sidhani kama unafahamu maana ya Wachungaji,maana ya Umoja,Umoja wa Wachungaji na mambo yanayowafanya kuwa na umoja. Naushuku sana uelewa wako wa kuchambua masuala kwa kina na sidhani kama ulisikiliza kwa makini kauli za Gwajima katika clip iliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii au redioni na kwenye runinga tunapaswa tufike mahali pa kutambua kuwa yapo mambo yanayotuweka pamoja na vilevile yapo yanayotutenga,Kama uliisikiliza kwa makini Gwajima aligusa mihimili ya Serikali kwa kuonesha haihofu(haitii)wakati Biblia yenyewe inasisitiza kutii mamlaka hapa na maanisha hakupaswa kuzungumza yote aliyoyazungumza na ninadiriki kusema alishindwa kutawala hisia zake na hivyo hisia zikaitawala akili yake na wewe unayoyasema hapa ni hivyohivyo umeshindwa kutawala hisia zako zimeiingilia akili yako ndiyo maana hoja yako imejawa na hisia kuliko uhalisia na nguvu ya hoja
 
Ukiona wamekaa kimya basi elewa walitambua mwenzao alibugi,sasa kama kabugi mwenyewe to that extent ulitaka wakasimame nae kutetea uovu? acha aingie mwenyewe si alianzisha ligi mwenyewe akajidai mjuaji was kutukana na kusema
 
Koma kabisa wewe chezea makristo wenzio usijumuishe wote
Kupulizwa hainihusu, hiyo ni mambo ya Mkweli Mwaminifu Bukhari alisema hayo baada ya kusikia kwa aliye sikia kutoka Mtume na Nabii wa Allah. Nyie hamjui kwanini mnatawazwa kabla ya swala? Ni kutayarishwa kabla ya kupulizwa.
 
Wachungaji umoja wao ni wakiroho na huapimwi kama mnavyopima umoja wa siasa.wachungaji huenda walikuwa wanakesha kumuombea Mchungaji mwenzao had aliweza kupata na mafunuo ya kutumia mawakili watafasiri sheria za nchi.maana
 
Back
Top Bottom